Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,124
Moja ya mwasisi wa Tanu na mwana CCM huko mkoani Mbeya amelaani kitendo cha viongozi wa CCM kutumia kodi za wananchi kuzunguka nchini na nje wakisema wanakodisha bandari kwa sababu watanzania ni wezi. Amewakumbusha viongozi wetu kwamba wakati wa mwalimu Nyerere tulikuwa hatukaguliwi huko nje ya nchi ila kwa kauli hizi maana yake tunafanya kila Mtanzania huko Duniani asiheshimike akihisiwa ni mwizi.
Kwa upande mwingine ameeleza kwamba vita kubwa Duniani zinatokana na ardhi pamoja na uchumi na anatokea mfano wa Israel na Palestin; ameeleza pia kwamba tulikwenda vitani Uganda kwa sababu ya ardhi hivyo tuilonde ardhi yetu sana.
Mzee huyu amewalaani viongozi wa CCM wanaotengeneza mazingira ya wizi na kisha kuwatumia polisi wapambane na wote wanaopinga wizi ikiwemo kuwatumia polisi kuzima mjadala wa bandari. Polisi ni watoto wetu tusiwagombanishe na jamii.
Swali, je wana CCM wenzake watamwelewa?