Tunamsahihisha Nyerere, watanzania siyo mabwege ila CCM ni pango la wezi wa mali ya umma!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Katika moja ya hotuba zake Nyerere alimfananisha mtanzania na bwege mmoja na tumemnukuu alichosema lakini siyo kweli mtanzania ni bwege bali CCM ni pango la wezi wa mali ya umma. Nyerere kwenye hotuba yake alisema yafuatayo na ninamnukuu:-

"Mtanzania ninamfananisha na bwege mmoja ambaye aliokota almasi kubwa lakini chafu chafu. Mjanja mmoja (mwekezaji) alipoona hivyo naye akaokota kichupa akakichonga na kukisafisha na akamfuata bwege (Mtanzania) na kumshawishi wabadilishane. Bwege (Mtanzania) alipoona kichupa mbona kinang'aa akakubali akapewa kichupa tu ili mradi kinang'aa na mwekezaji akaishia na almasi akaenda kuiosha na kuichonga na ikang'aa zaidi ya kile kichupa...bwege alipoona almasi yake imeng'aa akakitupa kile kichupa kikavunjika vunjika na yule mjanja (mwekezaji) akamwambia ukitaka almasi yako itabidi unifidie kwa uwekezaji wangu na gharama ya fidia ni kukuuzia hii almasi kwa bei ya soko.....bwege alipigwa na butwaa....hakuamini alivyotapeliwa." - J.K. NYERERE (Mwisho wa kumnukuu).

Mfano hai.

Mtanzania (bwege) alimwuuzia Kaburu NBC kwa bei ya kutupwa ya dola milioni 300 baadaye bwege akagundua alimwuuzia benki mbili kwa bei ya benki moja. Bwege huyu Mtanzania alipotaka arudishiwe benki ya NMB kaburu (mjanja) akamwambia amerudishie zile dola milioni 300 alizonunulia benki zote mbili ili amwuuzie NMB.

Bwege (Mtanzania) akakubali na hivyo akauziwa benki yake mwenyewe kwa hela aliyouzia benki mbili na hivyo kaburu akawa kajinyakulia NBC bure bila ya kulipa hata senti moja.

Kama hilo halitoshi baada ya miaka nenda rudi kaburu akamwuuzia mwingereza NBC kwa bei ambayo hadi leo haijulikani na kuinyima TRA mapato ya kodi.

Kama hili halitoshi, bwege sasa kauza bandari kwa bei ya kutupwa yaani hata sumni hatalipwa na kuna siku atashtuka kaingizwa mkenge na kwa sababu wako waliohongwa wakachukua hela sasa mwekezaji mwarabu atadai fidia ya mabilioni ya dola sawasawa na bei ya sokoni ya bandari zetu na wengi leo wanaopigia upatu wizi wa mali ya umma watakuwa aidha hawako madarakani au watakuwa wametulizwa kwenye makaburi yao na kuwaachia vizazi vijavyo mgogoro mkubwa wa kimkataba
 
Babu kamaliza mjadala tatizo siyo watanzania bali CCM sasa ni kimbilio la wezi na wabadhirifu
 
Nakataa uliposema pango la wezi ni CCM Kwa sababu:

Wizi haupo Tanzania tu, upo Kila nchi na nchi zenye Teknolojia kubwa wizi upo Tena Kwa kiwango kikubwa. Nchi hizo CCM haipo ila wizi upo. Nimekupa picha kubwa kwamba kama Teknolojia ingeweza kidhibiti wizi basi tusingekuwa tunasikia japani au wapi.

CCM inabeba lawama ya wizi unaofanywa na Kila mtanzania bila kujalisha itikadi yake ya kisiasa Kwa sababu ndio iliyoshika Dola. Tungechambua wezi waliopo serikali Kwa itikadi zao za kisiasa inawezekana wengi wa wezi hao wangekuwa ni wanaCHADEMA.

Tunapojadili wizi na wezi tusiache kujadili matumizi ya ruzuku ambayo ni Kodi ya mtanzania. Kimsingi tunaweza kuiacha CHADEMA tunapojadili wizi lakini kwenye suala la matumizi ya Ruzuku linatoa picha kubwa ya wizi ambao ungetokea kama CHADEMA wangeshika Dola.
 
Katika moja ya hotuba zake Nyerere alimfananisha mtanzania na bwege mmoja na tumemnukuu alichosema lakini siyo kweli mtanzania ni bwege bali CCM ni pango la wezi wa mali ya umma. Nyerere kwenye hotuba yake alisema yafuatayo na ninamnukuu:-

"Mtanzania ninamfananisha na bwege mmoja ambaye aliokota almasi kubwa lakini chafu chafu. Mjanja mmoja (mwekezaji) alipoona hivyo naye akaokota kichupa akakichonga na kukisafisha na akamfuata bwege (Mtanzania) na kumshawishi wabadilishane. Bwege (Mtanzania) alipoona kichupa mbona kinang'aa akakubali akapewa kichupa tu ili mradi kinang'aa na mwekezaji akaishia na almasi akaenda kuiosha na kuichonga na ikang'aa zaidi ya kile kichupa...bwege alipoona almasi yake imeng'aa akakitupa kile kichupa kikavunjika vunjika na yule mjanja (mwekezaji) akamwambia ukitaka almasi yako itabidi unifidie kwa uwekezaji wangu na gharama ya fidia ni kukuuzia hii almasi kwa bei ya soko.....bwege alipigwa na butwaa....hakuamini alivyotapeliwa." - J.K. NYERERE (Mwisho wa kumnukuu).

Mfano hai.

Mtanzania (bwege) alimwuuzia Kaburu NBC kwa bei ya kutupwa ya dola milioni 300 baadaye bwege akagundua alimwuuzia benki mbili kwa bei ya benki moja. Bwege huyu Mtanzania alipotaka arudishiwe benki ya NMB kaburu (mjanja) akamwambia amerudishie zile dola milioni 300 alizonunulia benki zote mbili ili amwuuzie NMB.

Bwege (Mtanzania) akakubali na hivyo akauziwa benki yake mwenyewe kwa hela aliyouzia benki mbili na hivyo kaburu akawa kajinyakulia NBC bure bila ya kulipa hata senti moja.

Kama hilo halitoshi baada ya miaka nenda rudi kaburu akamwuuzia mwingereza NBC kwa bei ambayo hadi leo haijulikani na kuinyima TRA mapato ya kodi.

Kama hili halitoshi, bwege sasa kauza bandari kwa bei ya kutupwa yaani hata sumni hatalipwa na kuna siku atashtuka kaingizwa mkenge na kwa sababu wako waliohongwa wakachukua hela sasa mwekezaji mwarabu atadai fidia ya mabilioni ya dola sawasawa na bei ya sokoni ya bandari zetu na wengi leo wanaopigia upatu wizi wa mali ya umma watakuwa aidha hawako madarakani au watakuwa wametulizwa kwenye makaburi yao na kuwaachia vizazi vijavyo mgogoro mkubwa wa kimkataba
Wewe ndio bwege watanzania tuna akili, mbwa we
 
Back
Top Bottom