Wanawake wachepukaji, jamani jaribuni kutunza heshima na siri za mambo ya ndani kwenu. Una mwambia mchepuko wako udhaifu wa mume wako ili iweje?
Nilikuwa nafanya udukuzi katika mfumo wetu wa mawasiliano ofisini kwetu. The Big boss aliniomba ni screen emails zote zinazoingia na kutoka nje ya domain ya ofisi. Basi weekend hii ndo nilikuwa nazipitia kufind out na kuna mambo ambayo boss alikuwa ana hisi.
Nikakumbana na mawasiliano ya dada mmoja na mchepuko wake. Tobaa dada kamponda mumewe ile mbaya. Yaani hata kama ni kuoza kwa mapenzi thats too much. Halafu na mjua mumewe kwani huwa anakuja kumchukua job mara moja moja.
He is a descent guy, nimepatwa hasira utafikiri mimi ndo nimedhalilishwa.
Halafu kwa nini utumie E mail ya ofisi kwa mambo binafsi? Unafikiri ndo salama?
Policies za kampuni na organization nyingi zina ruhusu kufanya udukuzi kwa employees bila kutoa taarifa, kama nilivyofanya.