Chemsha bongo hapa wapi nchini tanzania?

Chemsha bongo hapa wapi nchini tanzania?

4.JPG

ikijiandaa kutua uwanja wa ndege
 
Hivi ni watanzania wangapi wanatumia huo usafiri wa ndege acha ziwe ivyo ivyo coz bado miundombinu kama barabara stil ni mibovu boresha kwanza huku chini halafu ndo unakuja huko
 
KIA UKO SAFI KWA UBORA NA UZURI!

Hivi siku hizi kuna ndege inaenda Mpanda? Ndege ya Abiria au ya Pinda??

Kiwanja kila mahali can we afford at this time??

Where are our priorities?
 
Tayari tumeshajua kuwa mmesafiri sehemu nyingi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ndo uwanja pekee tulio nao Bongo tunaojivunia nao, ambao ukilinganisha na viwanja vya wenzetu huu unakuwa uwanja wa kata..... Hii nchi bana.

Si mmeona lakini serikali makini imezungushia uzio mkubwa sana pale kipawa pembeni ya JNIA mwaka wa tatu sasa?!?..mtaona kinachotoka hapo ni zaidi ya Heathrow Airport...lol
 
[TABLE="class: contentpaneopen, width: 540"]
<tbody>[TR]
[TD="class: contentheading"]Uwanja wa Ndege Mwanza ni aibu[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[/TR]
</tbody>[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen, width: 540"]
<tbody>[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Watumiaji wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza watakiri kuwa uwanja huo ni kiungo muhimu sana kwa shughuli za kibiashara, kijamii na hata kisiasa.Ni kiungo muhimu sana kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa

na mataifa yote ya Maziwa Makuu. Kama tungekuwa makini, Mwanza ndiyo ingestahili, pasi na shaka yoyote, kuwa “hub” ya Afrika Mashariki na Kati.
Pamoja na kusuasua kwetu katika kuifanya

Mwanza kuwa “hub”, yenyewe imejihalalisha kuwa na sifa hiyo. Bahati mbaya ni kwamba viongozi wetu, ama kwa kutojua au kwa uzembe, wameuacha Uwanja wa Ndege wa Mwanza uwe kama kituo cha daladala! Nimewaona wageni wengi wakishangazwa na hali ya uwanja huo.



Mara kadhaa tumesikia mipango kabambe ya kuufanya uwanja huo uwe wa kisasa. Upanuzi au uboreshaji uwanja huo umebaki porojo. Hakuna dalili za wazi zinazoonesha kama kweli tumedhamiria kuufanya uwanja huo kuwa uwanja wa kimataifa - wenye hadhi inayolingana na umuhimu wa Mkoa wa Mwanza kama “hub” ya Afrika Mashariki na Kati.


Kila uchao kunajengwa vibanda mithili ya vile vya kina mama ntilie mitaani. Kama Jumatatu ulikuta kunajengwa kibanda upande huu, Jumatano utakuta kunajengwa kibanda upande ule! Kumekuwapo


ujenzi wa vibanda visivyokuwa na hadhi wala mvuto unaoendana na umuhimu wa uwanja huu.
Kwa haraka haraka unaweza kuamini kuwa kinachofanywa na waliopewa mamlaka ya kuuendeleza uwanja huo, ni mbinu tu ya kufuja fedha. Kibaya zaidi, uwanja huu unatia aibu mno sehemu ya kupokea mizigo. Hakuna mashine wala utaratibu mzuri wa kupokea mizigo.

Kilichofanywa na “wahandisi” wetu ni kutoboa mashimo makubwa ukutani ambayo yanatumika kupenyezea mizigo ya wasafiri. Hakuna utaratibu kwa abiria kupanga mstari kupokea mizigo yao,

badala yake mwenye nguvu ndiye anayeanza kuchukua mzigo unaomhusu. Kwa mgeni ambaye ni mara yake ya kwanza kufika Mwanza, kitendo cha kupokea mzigo kwa staili hiyo kitakuwa kimempa taswira na kiwango halisi cha kufikiri cha Watanzania. Uwanja mkubwa, ulio ‘bize’ kiasi hicho hauwezi kuwa na sehemu ya kipuuzi ya kupokea mizigo ya aina hiyo.


Kinachouma zaidi ni pale unapobaini kuwa Mkoa wa Mwanza ni wa pili nyuma ya Dar es Salaam, kwa kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa (GDP). Unachangia Sh trilioni 3 kwa mwaka. Dar es Salaam

inaongoza kwa kuchangia Sh trilioni 5.4.
Nje ya uwanja, kuna vibanda vingi vya kipuuzi vilivyojengwa kwa mfumo wa uyoga. Hivi ni vile vinavyotumiwa kuuza vocha za simu, vyakula na huduma nyingine ndogo ndogo.Nini kifanyike? Kasi ya maendeleo kwa ukanda huu wa Afrika

Mashariki na Kati ni kubwa mno. Nchi zinazotuzunguka zinasaka maendeleo kwa udi na uvumba kwa kasi ambayo si rahisi kuielezea. Tukishindwa kwenda na kasi hiyo, ni wazi kwamba tutaachwa nyuma.


Tusipoifanya Mwanza kuwa “hub” ya ukanda huu, fursa hiyo itachukuliwa na wenzetu hata kama kijiografia hawana sifa hiyo.


Uwanja wa Ndege wa Mwanza tunapaswa kuuboresha ili uwe na hadhi ya kupokea ndege na wageni wa aina mbalimbali. Uwe uwanja ambao “mwekezaji” akifika, atatuweka kwenye kundi la watu makini,

badala ya sasa ambako kwa kuuona uwanja tu, atajua hawa ni watu wa kuhongwa na kuruhusu chochote wanachotaka.
Rais Jakaya Kikwete alipozuia ujenzi wa stendi ya muda mkoani Dar es Salaam, alifanya jambo la maana. Aliagiza litafutwe eneo, ijengwe stendi yenye hadhi na ambayo itakuwa imekamilisha jambo hilo.

Ujenzi wa vibanda katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni dalili ya uchovu wa fikra, na hauashirii kama kweli tumejiandaa kwenda na kasi ya wenzetu katika suala zima la maendeleo.

Kuendelea kung’ang’ana na vibanda kama vya waganga wa kienyeji, ilhali wenzetu wanajenga majengo ya kudumu na yenye hadhi, ni kujidhalilisha. Ukitazama miundombinu iliyojengwa na Mzee
Mwai Kibaki kwa miaka yake mitano ya mwisho, halafu ukatazama Uwanja wa Ndege wa Mwanza, unashawishika kuamini kuwa sisi ni mahodari wa porojo tu.
Kwa jinsi tunavyopenda kuunda tume, si ajabu tukasikia inaundwa tume kupata sababu za uwanja huu kuwa duni kiasi hiki![/TD]
[/TR]
</tbody>[/TABLE]
Uwanja wa Ndege Mwanza ni aibu
 
niko macho ndio maana naweza kuchati na wewe nakuuliza kwani ndege hazitui au wewe mpaka uone majengo mazuri ndio utajua umefika airport.
sio kwa serekali hii yenye surakali na serakali
yaani sirikali nyingine ikiingia madarakani sijui itaanzia wapi maana elimu ccm wamekwishaimaliza madini wametuachia maandaki afya ndio ukiwa na kitambi unaonekana una afya bora, kilimo ndio hicho kimekuwa kwanza, twiga wanapandishwa ndege, maji tunalipia lakini ukifungua bomba zinatoa hewa na sisi hatujalipia hewa, umeme nao tunalipia ukitoka kununu vocha ya luku ukifika nyumbani huwei kuweka maana umeme hakuna.
wewe unataka tukajenge majengo mazuri airport wakati watu hali zao ni mbaya hospitali watu wanalala chini hakuna vitanda wla madawa wala vifaa tiba mashule walimu wamechoka wanajinunulia chalk na kuuza vitumbua hatuna hata mtaala wa elimu walimu hawana nyumba za kuishi baadhi ya shule hazina hata matundu ya choo au wewe hujasikia kuna shule inafugwa kwakukosa chakula? wewe unataka majengo ya kurushia twiga? usafi wenyewe kwenye miji umekuwa kwa hisani ya watu wa marekani

We have a long way to go and we don't know where are we heading to

Mkuu kusema kweli nimecheka sio kwa kufurahia maisha uliyoyaongelea bali umahili wako wa kufikisha ujumbe. Kwa kweli hali ni mbaya, inasikitisha!
 
Mkuu kusema kweli nimecheka sio kwa kufurahia maisha uliyoyaongelea bali umahili wako wa kufikisha ujumbe. Kwa kweli hali ni mbaya, inasikitisha!

Hali ni mabaya ndio hawahawa nayapamba makaburi nakuyapiga chokaa ili yangae wakati ndani yameifadhi miili iliyoharibika. hakuna haja ya kuosha kikombe kwa nje ili kionekane kisafi ilihali ndani ni kichafu. eti wageni wanaokuja nchini watusifie kuwa nasisi tuna majengo mazuri kwenye viwanja vyetu vya ndegu wakati kwenye hosipitali wakina mama wanaenda kujifungua wamelazwa chini hakuna hata pamba, na viwembe yanini majengo ya kurushia twigwa??

CC MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi kilakitu kinawezekana! Sintashangaa aliyeandika hapa ndio rubani anerusha ndege!

Kigoma%2BAirport%2B1.JPG
 
Back
Top Bottom