Imeripotiwa kuwa Pochettino hachukulii maanani sana juu ya tatizo la uchezaji wa mpira (IQ ya mpira) wa Mudryk na tena hamwamini Mudryk katika safu ya ulinzi na anaamini hana akili nzuri.
Nadhani unaweza kudai kuwa ni kazi ya Pochettino kuboresha huo udhaifu, lakini tena tumesikia kuwa Pochettino hufanya vizuri sana katika kuboresha vipaji vya wachezaji wachanga. Hata ikitokea Mudryk akauzwa nadhani Pochettino atafurahia sana. hii itakuwa mbaya sana kwa kocha ambaye kakaa muda wote huo na mchezaji mwenye kipaji na aliyefanya vizuri kwa makocha wengine ila yeye akashindwa.
Ndiyo, ameshindwa kwa sababu Inaonekana kama matatizo ya Mudryk, sio ya Pochettino na hatapata msaada wowote wa kuendelezwa kimpira kutoka kwake au kwa wasaidizi wake. So hii dhana ya kwamba Pochettino ni mzuri kwenye kukuza viapji vya wachezaji wachanga ni upuuza uliotukuka na kwamba hata akina Harry Kane na Dele Ali walikua vizuri kwa uwezo wao binafsi na ndio uliwafanya wakafika hapo walipo.
Kufeli kwa Mudryk ni taswira ya wazi ya mapungufu ya Pochettino. Ni kama taswira ya jinsi kocha wetu anavyofanya kazi katika kukuza vipaji. Ikiwa hawezi kuwa na imani na mchezaji mchanga mwenye kipaji kama Mudryk, kwa njia kama hii, tutawezaje amini kuwa atakuza vipaji vya akina Palmer, Paez, Angelo, Santos, Carney, Colwill, Jackson, Omari na wengineo na wale watakaosajiliwa?