Kwa sababu kama ni kupaki basi then nyie ndo mlilipaki juzi esp second half maana pasi ziliacha kuwa zile fupifupi na kuhamia loong passes na ambazo zilikuwa zinafia kwa Valencia na RvP mwenyewe au Welbeck.
Kipindi cha kwanza, umiliki wa mpira ulikuwa ni 57% kwa United na 43 kwa Chelsea. Huku Carrick na Cleverley wakishika dimba ipaswavyo. Carrick alikuwa na pass completion rate ya 87%. Of course, Hazard aliongoza kwa 90% completion rate. Kwa game nzima possession ilikuwa 55% kwa United na 45% kwa Chelsea.
Lakini, unavyosema, United ilipaki basi 2nd half, unamaanisha 2nd half Chelsea walishambulia zaidi ama? Shots on goal na on target unajua zilikuwa ngapi? Jumla kulikuwa na shots on target 7, 3 kwa United na 4 kwa Chelsea. Shots off target zilikuwa 10, 7 kwa United na 3 kwa Chelsea. Sasa kupaki basi kwa United in 2nd half kuko wapi?
United ilikosa creativity katika kusukuma mpira wa mwisho kwa strikers. Carrick na Tom walimiliki sana mpira, lakini passes zao hazikwenda sana kwa strikers. Chelsea had all creative players in the midfield, Hazard, Oscar na Ramires, lakini kutokana na defensive plan, hawakuwa na natural striker. Hivyo creativity yao ikakosa kuonekana, zaidi ya shots 2 za Oscar.
Pia hauijui United wewe. Long passes ni style ya United way back. Pasi fupi fupi uwa United inacheza ikitumia diamond formation. Ambapo SAF alijaribu kuitumia kwa kuwatumia Kagawa, Rooney, RvP na Welbeck/Chicharito kwa panoja. United ni maarufu kwa long passes; hivyo kama uliona matumizi ya pasi hizo ndo dalili ya United kupaki basi, rudi tena ujipange chifu.
Again style ya Mourinho kucheza ni kutumia wing-forwards wenye speed amabo wanaweza kupanda na kurudi haraka ndiyo maana unaona hajaopt sana kumtumia Mata in most of the games..Mata ni mzuri akiwa na mpira but hana speed ya ku-track back kurudia mpira. Sasa kama hiyo tactic mnaiita bus parking u can as well go to hell complaining about it.
De Bruyne naye anaweza kuitwa 'wing-forward' mwenye speed? Ni mzuri zaidi ya Mata katika kuleta ushindi? Halafu, wing-foward ndiyo nafasi gani kwenye soka?!? Kuna left na right wingers ama zamani waliitwa outside forward. De Bruyne alikuwa right winger na Hazard left winger siku ile.
Kwa upande mwingine, Mourinho alitumia 4-2-3-1 huku Lampard na Ramires wakiwasaidia mabeki sana. Yaani naweza nikasema formation ni kama ilikuwa 6-3-1 ama 4-6-1. Sasa, formation hiyo si ndiyo kupaki basi chifu?!? Kwani kwa hiyo formation timu inakuwa defensive minded.
Unaonekana hufahamu style ya Mourinho. Yeye upenda kutumia deep-lying defensive tactical plan. Alipokuwa Inter, alitumia hiyo plan, mpaka akaomba msamaha kwa mashabiki. Alipoenda Real, alifanya hivyo mara nyingi kwa Barcelona, mpaka siku moja akasema, alipark ndege na siyo basi. Huyo ndiyo Mourinho; na katika hilo, hakuna anayefikia perfection kama yeye. Hata ubishe, huo ndiyo ukweli.
Sasa unamlaumu Mata nini? Unataka afanye kazi ya namba 6??? Mtazamo huo ndiyo parking the bus. Eti arudi nyuma! Arudi kufanya nini? Mata ni attacking midfielder ama central midfielder a.k.a playmaker. Unajua kazi za mchezaji wa nafasi hiyo?
We saw Cahill na Ivanovic wakipanda vizuri tu..ila attack ilipokuwa inarudi kwetu the speedy ones like Ramires na Hazard walikuwa washafika to counter the attacks. Oscar was there too to pick the saved balls kurudi kwao.
Mh! Labda mimi sikuwa naangalia mpira, Cahill alipanda mara ngapi na matokeo ya upandaji huo yakawa nini? Husilete upandaji wakati wa kona; kwanza game nzima mlipata kona 1 tu.
Ulivyoeleza, ndiyo alama ya 'parking the bus philosophy'. Ndiyo Mata hakuanzishwa kwani yeye ni attack-minded kuliko wote hao; na amekuwa one of the Chelsea's best players toka amefika hapo.
Kwa attack-minded formation, namba 6 ndiye atakayerudi kusaidia namba 4 na 5. Namba 8 yeye ni playmaker na vilevile anakuwa ni kama mshambuliaje. Ndiyo maana Kagawa akawa mchezaji bora wa Bundesliga, huku akifunga magoli. Lakini kwa Mourinho namba 8 naye anafanywa kama 6!! Si umeona juzi Oscar alivyofanywa? Oscar akiwa na Brazil anakuwa attacking midfielder, lakini kwa Mourinho anakuwa defensive midfielder!!
Problem ninayoiona ni watu wakishaona forwards wamerudi nyuma basi inaitwa kupaki basi...stupid as.s nig.gas...ni kukubali tu kuwa wewe unaspeed kuliko huyu so utarudi nyuma...before huyu hajarudi.
Hakuna haja ya kutukana chifu. Tujadili kama watu wa mpira; na si wa ngumi!
Sasa, siku ile forward alikuwa nani kabla ya Torres kuingia?!? Timu imeanza bila mshambuliaji halisi, halafu unasema haikupaki basi?
Kupaki bus on the other hand ni pale unapomuona R. Ferdinand 90 minutes hajavuka the half mark ya uwanja...think about it!!!!!
Duh! Kweli unazi noma?
Na kona zote zile Rio hakuvuka half mark?!?
Anyway, kazi ya centre back ni kuzuia timu pinzani isifunge magoli, kunyang'anya mipira kutoka kwa washambuliaji wa timu pinzani, na kumlinda kipa. Unataka avuke half mark ili afanye kazi za central midfielders?!? Right and left backs (full backs) wao ndiyo wanaweza kuvuka hiyo half mark mara nyingi; ndiyo maana katika modern soccer hawa right and left backs uitwa attacking full backs. Hao ndiyo kina R. Carlos, Lizarazu, Evra, Clichy, Marcelo, Maicon, A. Cole etc.
Ulishawahi kucheza hata mpira kidogo? Nimeuliza hivyo kutokana kusema Rio alipaki bus, huku ukisema Cahill alipanda vizuri tu, na ukisema Mata hawezi kutrack back mipira!! Inakuwa ni kama huelewi kazi za wachezaji kwa nafasi zao uwanjani!!
Mwisho, filosofia ya mpira wa Mourinho ni defensive game. Hiyo hata ubishe hadi kesho, ndiyo hali halisi. Chelsea ilikuwa ikicheza mpira wa kufunguka sana chini ya Di Mateo na Benitez. Chini ya Mourinho mtapaki basi sana mkikutana na timu kubwa. Tarehe 31 utajionea mwenyewe.
Soma hizi match analyses pia.
www1.skysports.com/football/live/match/295725/analysis
m.premierleague.com/en-gb/matches/2013-2014/epl.match-stats.html/man-utd-vs-chelsea