Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

EDI MENDY THE BEAST [emoji91]

[emoji871]Kuna siku mambo hayaendi, mpinzani wako anacheza vizuri sana , kwa kila kitu ..hapo ndio utamuhitaji golikipa wako aoneshe umahiri wake Edi Mendy alikuwa katika daraja la peke yake ...Golikipa huwa anashinda points kwa timu yake na leo Mendy naweza kusema kwa kujiamini kabisa ameshinda pointi 3 kwa Chelsea

[emoji871]Kipindi cha kwanza Chelsea walicheza vizuri hasa eneo la kiungo Kovacic na Loftus Cheek , walikuwa wanaishinda pressing ya Brentford sio kwa pasi bali kwa uwezo wao wa kuficha mpira na kukimbia nao kwa kasi sana ( driving forward ) na walistahili kufunga goli . Viungo watatu waliweka ulinzi mzuri kwa mabeki watatu wa nyuma

[emoji871]Kipindi cha pili kilikuwa ni Brentford tu , walikuwa bora kwa kila kitu, kasi, nguvu , pressing , passing , kutengeneza nafasi , second balls , hata mipira ya kwanza kilicho wakwamisha ni Mendy tu kwa saves zake za hatari sana . Mbuembo na Toney jinsi wanavyocheza wanatishia mmoja anaruka juu kushinda mipira na mwingine anakimbia nyuma ya safu ya ulinzi kwa mpira unaoanguka .

[emoji871]Thomas Frank kocha wa Brentford anajua kuona udhaifu wa timu pinzani na kuutumia ...alifanya dhidi ya Liverpool, Arsenal na leo kakosa tu pointi , lakini alijua Chelsea bila ya Silva na Rudiger ni kuweka mipira mingi ya krosi akijua vijana Chalobah na Sarr hawana uzoefu huo na uwezo wa kupambana mipira ya juu huku wakiwa na wachezaji kama watatu nje ya penati box kuokota second balls

NOTE

1: Matokeo kama ya leo kwa Chelsea umuhimu wake unaonekana wakati wa kuwania taji mwishoni mwa msimu

2: Ben Chilwell mechi 3 za mashindano yote kafunga mara 3 . Ushindani wake na Alonso kule pembeni ni afya kwa kikosi

3: Siku mbaya ofisini kwa Romelu Lukaku
 
Kosa la kumtoa Lukaku ambae alikua ameshikilia ma bekiwa sitoke kule nyuma lisirudiwe tena na TT, nina wakika TT amejifunza kitu, kuanzia dakika ya 60 tume ponapona tu, Mount hakubadili chochote, ila tume shida muhimu poiti 3. na first 11 yetu imepumzika kwa ajili ya Uefa, kwa sasa kombe la premier kwa 55% ni letu, sasa tuna kikosi kipana cha kubadilisha Big up TT
 
Edouard Mendy deserved a Ballon d'Or nomination [emoji122]

Extraordinary goalkeeper

@English_Premier_League_Update

Wajumbe hii agenda vipi, tuungane na Khalidou Koulibaly?
IMG_20211016_222129_762.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom