Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 16,055
- 27,460
Lampard katusaidia tumeingia top 4, tumecheza fainal FA yote hayo zingatia na ufinyu wa kikosi. Labda mlikua mnataka Lampard afanye maajabu gani?Mimi sifuati mkumbo na wala sisemi kisa amesema yeye. Mm nasema kile nakiona kwa Lampard, toka Mwanzo huw nasema kuna wachezaji hawafai kuwa Chelsea pamoja na Lampard wewe mwenyewe ni shahidi. Mtu kama takataka Abraham, Loftus kuku, muoka mikate na wengineo
Lampard bado Sana, kama kuna madogo huwa tunawatoa kwa mkopo ili wakapate uzoefu basi ata Lampard akafundishe vi timu vidogo huko ili apate uzoefu.
Tumetisha kinoma.Havertz tayari ni mchezaji halali wa Chelsea
Wewe ni kalabao tu hujui lolote, mbele ya wasomi unakuja na data uchwaraHawa ndio vichwa ngumu wanaoongelewa.
Linapokuja suala la kocha kutokuwa mzuri, hatuangalii kama bodi ya timu imempenda au la.
Leo zipigwe kura kwa mashabiki wa Chelsea duniani kote kuamua kama Lampard anafaa kuimanage timu kama Chelsea mpaka muda huu, tegemea 70% ya majibu kuwa HAPANA!
Ni kiasi cha muda tu, mtaanza kuzozana wenyewe kwa wenyewe humu.
Msimu ujao lazima abebe EPL na UCL kwa speed aliyoanza nayoNimeona kauli ya mtu mmoja humu kwamba "uyo Arteta sijui ana misimu mingapi EPL"
✓ana nusu msimu na vikombe kadhaa vya kuvimbia mtaani
✓hakuwa na timu tangu mwanzo wa msimu na hajafanya sajili yeye
[emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 1554499
Hayo ni maoni yako na kila mtu anamaoni yakeIpo siku watu wataelewa unachokisema! Kwa sasa hawawezi kuelewa ......... mi pia nina fikra kama zako kwa kile nachokiona, mi nasubir msimu uanze sijui atatetewa kwa lipi wakat amesajili, mana alikua anatetewa kwa kutokusajili. Ipo siku tutaongea lugha moja humu.
Lamps ni takatakaMpka hapo tulipo kaa ni juhudi za wachezaji tu na baadhi ya timu kutokuwa vizuri. Fikiria vizuri kama Arsenal wangekuwa na huyo kocha toka mwanzo hiyo nafasi wangekaa wenyewe.
Lampard hana mbinu zozote zile hakuna tofauti katika kipindi cha kwanza na cha pili, hakuna tofauti tunapo fugwa na pindi hatujafugwa. Nilicho kiona kwa Lampard ni kumiliki mpira tu
[emoji23][emoji23][emoji23]Msimu ujao lazima abebe EPL na UCL kwa speed aliyoanza nayo
Unasema hapo tulipo ni juhudi za wachezaji na bado unawaponda kina Tammy top score wa timu, unawaponda kina Barkley, RLC na kadhalika nashindwa kukuelewa umesimama wapi?Mpka hapo tulipo kaa ni juhudi za wachezaji tu na baadhi ya timu kutokuwa vizuri. Fikiria vizuri kama Arsenal wangekuwa na huyo kocha toka mwanzo hiyo nafasi wangekaa wenyewe.
Lampard hana mbinu zozote zile hakuna tofauti katika kipindi cha kwanza na cha pili, hakuna tofauti tunapo fugwa na pindi hatujafugwa. Nilicho kiona kwa Lampard ni kumiliki mpira tu
Umeongea vyema sana mkuuUnasema hapo tulipo ni juhudi za wachezaji na bado unawaponda kina Tammy top score wa timu, unawaponda kina Barkley, RLC na kadhalika nashindwa kukuelewa umesimama wapi?
Kama Lampard hana mbinu basi tusingekua hapa tulipo yawezekana tungekua Championship sa ivi. Shida ni kwamba hajafikia expectations zako ndio maana unasema ivyo. Nahisi bado unaamini kwenye mpira kuna kubahatisha ndio maana unasema wachezaji ndio wamechangia kuwa hapa tulipoishia msimu uliopita. Bro hakuna kitu kama hicho kwa sababu ingekua rahisi kwa Wolves kulingana na wachezaji walionao wangeweza ingia top four.
Usichukulie poa kocha ana mchango mkubwa sana mfano waliwahi kumsema sana Zidane anabebwa na wachezaji alionao kipindi kile anachukua UEFA mara 3 mfululizo aliondoka timu ikaanza kuboronga aliporudi baada ya muda mambo yamekaa sawa huku Ronaldo akiwa hayupo. Same kwa Pep akiwa Bayern alikua na utajiri wa wachezaji kibao lakini kila msimu kwenye UEFA anaangukia pua leo hii Bayern hao hapo UEFA wamebeba wakiwa na kocha mwingine mabadiliko ya wachezaji ni Roben na Ribery ndio hawapo sasa utasema hao ndio walimzuia Pep asichukue UEFA akiwa Bayern? Nadhani jibu ni kuwa mbinu zake zilifeli kulingana na wachezaji aliokuwa nao.
Hebu tumuache Lampard afanye kazi yake huu mtindo wa kubadilisha makocha kila msimu ndio unafanya kukosa consistency ya performance. Msimu huu tutaperform msimu ujao maji ya shingo. Yaan haijawahi tokea tumeenda zaidi ya misimu mitatu onform coz kila kocha anapokuja kila kitu kinabadilika. Though mtindo huo umesaidia kubeba makombe ila nahisi boss keshachoka ndio maana wamemuamini Lampard.
Super Frank. Our Past, Our Present, Our Future
Halafu Lampard karekebisha madhaifu mengi hasa yaliyoonekana kwenye mechi ya kwanza a Manure ya kupress high na kuacha void katikati mapaka viungo wa timu pinzani kupata mwanya wa kufanya counter.Kweli kabisa LAMPARD alipewa timu katika mazingira magumu kama:-
1. Hazard aliondoka
2. kuondoka Babu Sari (Kocha mpya kwa wachezaji)
3. Ban ya kutofanya usajili.
4. Uchanga wa Lampard Epl kama kocha
Tuseme ukweli Mungu anatuona, sidhani kama kuna shabiki yoyote wa Chelsea duniani alitegemea timu ingemaliza TOP 4, NEVER.
Mbio za kumaliza Top 4 zilikuja baada ya kuona tupo tupo top 4 muda mrefu, tukapata matumaini tunaweza maliza nafasi za juu.
Jamani Mnyonge mnyongeni haki yake tumpe. Kumaliza TOP 4 ni mafanikio makubwa sana kwetu kwa changamoto tulizopitia msimu huu.
Tumesajili wachezaji wapya msimu ujao ndio tutaanza kuupima ubora wa Lampard. Na hata hivyo tusitarajie sana ubingwa mi naona target iwe kumaliza ndani ya Top 2, Msimu ujao 21/22 tupambanie ubingwa.
Mid table mnajua kujifariji.