Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Lampard kocha mzuri usitake kuwaaminisha watu ushubwada wako we unazani Mpira ni kitu cha kukurupuka inatakiwa kocha avumiliwe atengeneze timu yenye ushindani humuoni klopp alivoanza kazi aliteseka sana na kikosi alichokikuta tatizo lenu nyie mnataka matokeo ya mapema kitu ambacho hakiwezekani kwenye mpira
 
Nyekundu, unatuabisha, mko nafasi ya ngapi vile? Shefield kutufunga ni hasara kwako ndugu, au hujui nini hata Europa utaikosa
Potelea karibu, mimi timu yangu sio nzuri kwasasa hata nisiposhiriki huko ndio vizuri nipate muda wa kujenga timu,
 
Vp kuhusu mchezaji wako Abraham?
 
Pamopja na 74% ya ball possession, jana Shefield United walikuwa na touches nyingi kwenye final third kuliko Chelsea
Wote walikuwa na shot on target 4 ila Shefield walizitum ia vizuri 3 kati ya hizo 4
Wao walikuwa rigid nyuma na well organized sisi tulikuwa tunafunguka mno. Mfano goli la kwanza, James, Christansen na Zouma walibaki kushangaa badala ya kuwahi kumsaidia kipa. Goli la pili walicha nafasi kubwa upande wa kulia au upande wa winga wa kushoto wa Shefield na hivyo kumpa mpiga krosi nafasi na uhuru wa kuchagua ampigie nani. Christensen's alitakiwa azibe hiyo nafasi wakati Willian na James wanamkaba jamaa. Goli la 3 hilo ni la Rudiger, kacheza fyongo kabisa. Hata kama alikuwa na presure huo mpira kuutoa kona haikuhitaji uwe na nguvu kubwa, badala yake CB mzoefu kama Rudiger unamrudishia mfungaji ambaye hakuwahi kufunga tangu ligi ianze goli la zawadi kama lile
 
Utajenga team yako mpaka lini?Maana nyinyi kila season mnajenga team
Tunaijenga kidogokidogo,hatuna haraka kabisa...tumeshayafanya mengi yenye faida kwa timu ikiwemo kujenga uwanja n.k sasa tunajenga timu ya ushindi taratibu.
 
Huwezi ukasajili tim nzima mkuu

Kingine kutawala possession sio ajabu mbona pep huwa anafungwa ila ukiangalia bado kapiga passes nyingi tu

Wachezaj tulionao sasa hawawezi kucheza katika viwango vyao katika mech zaid ya 3

Kuna magoal tunafungwa je unataka lampard ndio aingie akadefend hapan
Kwa mfano christensen na zouma walicheza vizuri mech ya watford wakafanya vizuri mech inayofata ya crystal palace zouma alicheza vizuri jana combination hiyonhiyo ya zouma na christensen ilikuwa iko hovyo 2nd goal mcburnie anapiga free header hakuna hata mmoja aliyekuwa anamkaba

Mechi na city christensen na rudiger walicheza vizuri mechi na west ham kilichotokea kila mtu anakijua

Endapo tim yetu ingekuwa inawachezaji wazuri blame zote angekuwa anatupiwa lampard na sidhan kama mpk sasa hiv angekuwepo ila kwa kuwa wachezaj tulio nao sasa ilitubidi tuwatumie tu kulikuwa hakuna namna
Tuangalie sajili anazofanya lampard na wachezaj anaowataka ndio utagundua kuwa lampard player waliowepo sasa ilimbidi tu afanye nao kazi kulikuwa hakuna namna zaidi ya kuwachakua na wale waliokuwepo.
Na hata msim ulipoanza hakuna aliyetegemea kama tungekuwa hapa tulipo sasa

Tumjudge lampard msim ujao. Msim huu ni kama tunamwonea vile kwa upande mwingine na ndio maan board imempa bck up kwenye usajili ni tofauti na makocha waliopita

Lampard ana mapungufu yake ila mpk hakuna aliyedhani kama anaweza fika hapo alipofika kutokana na wachezaj tulionao kwa sasa.
 
Usiende kw klopp kwanza Ole tu ni mfano sahihi
 
Nimekuja na swali moja tu! "Yuko wapi yule Abraham tuliyesifiwa kwa kila mapambio kuwa apepatikana mwenye Jezi namba 9 iliyowashinda wengi?"
 
Nakuunga mkono kocha gani hana first eleven ya kudumu karibu mwisho wamsimu hana wining team anatapatapa tu, tunahitaji kocho muzoefu kama conte sari nk lampard anafaa kua msaidizi
Vuteni subira wakuu, Hata OGS hakuwa na first eleven kwa muda mrefu now kaipata na anaendelea kuiboresha.
Mnapitia katika kipindi cha transition, hivyo endeleeni kunywa mtori taratibu nyama mtazikuta chini ya chungu.
 
Uko sahihi, naunga mkono ulichokiona. Tukishambuliwa tunakuwa vulnerable sana, tukienda mbele tunakuwa butu hatuna creativity yeyote
Overall possession jana ilikuwa 74%, Harvertz ni wa muhimu sana asaidiane na Ziyech na Willian na Pulisic
Msimu uliopita Ziyech alikua linked na Arsenal, nikasema sasa hapa tunapata winger madude gani sijui yakatokea akaja Pepe. Kwa Ziyech pale mmepata mtu
 
Nakuunga mkono kocha gani hana first eleven ya kudumu karibu mwisho wamsimu hana wining team anatapatapa tu, tunahitaji kocho muzoefu kama conte sari nk lampard anafaa kua msaidizi
Hapo kwenye 1st eleven ya kudumu, mtukuwa mnamuonea Frankie,

Mfano, kati ya Zouma, Christensen na Rudiger. Utamchukua nani, maana wote makosa yao ni yaleyale.
 
Yaani unacheza na timu inayochezea(possess) mpira kuliko wewe, halafu uanze na viungo wasio wakabaji???
 
Tafuta comment yangu ya mechi ya juzi tuliyoshinda 3-2, nilicomment kwamba HONGERNI CHELSEA KWA USHINDI WA POINT 3 MUHIMU, ila tunahitaji engineer kutoka lamasia aje asuke kikosi upya.
Utabadilisha kocha mpk lini

Kwa kikosi kilichopo hata aje pep,zidane or klop bado atastruggle

Kama tu pep wakati anakuja city ilikuwa na akina nasri,nevas,negredo,yaya toure na bado akastruggle unategemea kwa chelsea hii iliyopo ata kocha gani akija atafanikiwa

Kocha aliyepo asajil wachezaj wa maana wakati huo huo kidogo kidogo tunapunguza hizo middle table player waliokuwepo baada ya hapo ndio utajua kocha huyu ni mbovu na hna mbinu
 
Sio lazima wao waripoti. Ila ukweli ni kuwa hiyo taarifa ata mm nimeiona mahara. Ila huyo Ugurcan Carik si mzuri kivile maana kwenye michezo 31 ana clean sheet 4 tu. Kwann tusichukue Nick Pope ama Dean Henderson
Dean Henderson ni kipa wa United na sio wa kuuzwa yule..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…