Mechi za kirafiki
Mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Manchester City wataelekea nchini Marekani kwa ziara ya ambayo itashirikisha mechi za kirafiki dhidi ya wapinzani wao wa Uingereza Chelsea na Liverpool.
Klabu hizo tatu zitaungana na klabu za Manchester United, Arsenal na Tottenham katika mchunao huo wa mabingwa wa kombe la kimataifa
Shindano hilo la kila mwaka pia litashirikisha mabingwa wa Uhispania, Itali, Ufaransa na Ujerumani -Bercelona, Juventus, PSG na Bayern Munich - pamoja na Benfica na Atletico Madrid.
Southampton ilikuwa timu ya kwanza ya ligi ya Uingereza kucheza mechi za kirafiki baada ya kutoka sare ya 3-3 dhidi ya klabu ya ligi ya Bundesliga Schalke nchini Ujerumani kabla ya kuelekea nchini China kwa ziara ambayo ilikamilika na ushindi wa 3-2 dhidi ya klabu ya Jiangsu Suning.
Mechi za kirafiki kabla ya msimu wa ligi ya Premier kuanza:
Chelsea
23 Julai: Perth Glory v Chelsea (Optus Stadium, Perth)
28 Julai: Chelsea v Inter Milan (Allianz Riviera Stadium, Nice)
1 Agosti: Arsenal v Chelsea (Aviva Stadium, Dublin)
5 Agosti: Chelsea v Manchester City - FA Community Shield (Wembley)
7 Agosti: Chelsea v Lyon (Stamford Bridge