Chelsea Wana kasi Sana Katika eneo la juu kwamaana ya eneo la ushambuliaji, ukimuachia Olivier Giroud Basi washambuliaji wengine waliobaki lazima wakupe mtihani wakati wanakuja kwenye eneo lako la ulinzi.... Yes, Kama Conte ataanza na pure #9 alafu Willian na Hazard watokee pembeni Katika wale watatu wa mbele, hi inaweza kuwa na impact kubwa zaidi kwa Chelsea Katika eneo la kujilinda na kushambulia..... hapa wataalamu wanasema njia nzuri yakujilinda Ni kushambulia.
Barcelona wanaratibu mipango yao yote Katika eneo la kiungo, na hapo katikati ya uwanja ndipo wanapokuwa wamejikusanya Mara nyingi zaidi kabla ya kutawanyishwa na pasi miguuni mwao.... Bosqute ndiye kiranja mkuu wa eneo Hilo, huyu ndiye plan starter ya Erneste Valved...... Yes, Rakitic, Paulinho na mwalimu mkuu Iniesta Kama wakianza kwa pamoja wanaweza kuwa na hatari kubwa zaidi ya eneo la ushambuliaji chini ya Messi na Suarez.
Eneo katili Katika kikosi Cha Chelsea Ni eneo la kiungo. Yes, chini ya Kante na kwa aina hii ya mchezo Basi unaweza kumuona Mara nyingi sehemu mipira ulipo kuliko mchezaji yeyote Yule wa Chelsea Katika mchezo huu. Fabrigus na Luiz Kama watapangwa Katika kiungo ili kumsaidia Kante Katika mgawanyo wa Majukumu basi Sina shaka na kuendeleza ukatili wa eneo katili kwa Chelsea. Pressure ya mchezo sambamba na pressure ya mashabiki vinaweza kumharibia kabisa game mentality Bakayoko, nawaza Kama atatokea nje inaweza kuwa na faida Sana Katika plan ya kumalizia mchezo.
King Leonel Messi huyu anahitaji kuzuiwa Kwanza kwenye njia zote za kumfikishia mipira. Yes, kumkaba Ni ngumu Sana ila kuzuia njia za mipira kumfikia inaweza kuwa na ahueni zaidi kutokana na aina ya uchezaji wake....... Conte akimfanyia man making Leonel Messi hii itapunguza nguvu kubwa Sana kwenye eneo la kiungo na kutoa mwanya kwa Barcelona ambao hupenda kuwa wengi kwenye eneo la kiungo kuutawala mchezo sababu Mara nyingi Messi huwa free role na Hana Majukumu mengi Katika timu.
Nelson Samedo na Marcos Alonso Hawa ndio wachezaji hatari na muhimu Katika mchezo huu nyuma ya Messi na Hazard.... Alonso Ni mzuri zaidi kwenye Pace na kumwaga maji Katika box na mipira yake mingi inayoelekezwa kwenye final third ya opponent huwa na madhara kuliko pace zake, huyu ndiye mtu wa Kwanza wakuchunga kabla ya wengine...... Samedo amekuwa aiitumika vizuri zaidi Kama full back was kulia na amekuwa anamadhara Sana pindi anapokuwa na mpira miguuni, ubunifu, kujiamini pamoja na Kasi vimekuwa vikimfanya acheze juu zaidi Katika upande wa kulia wa Barcelona na v-pass ndio pasi zake nyingi zaidi anapokuwa amefanya pace ndani ya box. Kama Chelsea watafanikiwa kumzibiti wanaweza kuwa wamewadhohofisha Sana FC Barcelona.
Okay...! Kizuri ni kuwa Hawa wote wawili watakutana Katika upande mmoja wa mchezo huu.... Samedo upande wa kulia wa Barcelona na Alonso upande wa kushoto wa Chelsea.
Gerald Pique na Samuel Pamoja na ubora wao Katika kuijenga timu kwenye kusnzisha mashambulizi, bado wamekuwa Ni wahanga wa speed.... Mara nyingi wamekuwa wakiteseka Sana wanapokutana na wakimbiza upepo wenye zana Kama za Hazard miguuni. Bado Kama eneo la kiungo litashindwa kumzibiti uzuri hazard na zile zana zake Basi walinzi hawa wanaweza kuwa watumwa Katika upepo mwanadamu huyo kabla ya Aerials za Olivier Giroud.
Ninakiheshimu Sana kipaji Cha Christiansen, lakini kwa salama ya Chelsea leo basi Rudiger na Christiansen waanzie kwenye Mbao ili Luiz akatubu zambi za uzoefu alizozipata kule Paris sent German dhidi ya ushapu na uviziaji wa Luis Suarez.... Kuna wakati uzoefu unaweza kufanya kazi zaidi haswa Katika kuhakiki mipira yote Katika box la Chelsea sababu ya aina ya uchezaji wa Suarez.
Ter stergen amekuwa kwenye ubora Sana kulinganisha na Courtois ambaye msimu huu ubora wake umepungua sana kulinganisha na misimu miwili nyuma. Kama performance yake itaendelea kuwa chini Basi itawatesa Sana Chelsea tofauti na Te stergen.
Dembele, Denis Suarez, Pedro na Morata Ni silaha nyingine za Siri nyuma ya Sergio Roberto.
Chelsea vs FC Barcelona.....