Siku tatu za mapumziko.
Antonio Conte ameongeza siku mbili zaidi za mapumziko kwa wachezaji wake na kuhitimisha kuwa tatu baada ya kichapo cha 4-1 dhidi ya Watford katika dimba la Vicarage Road jana Usiku.
Watford walifunga magoli matatu katika dakika sita za mwisho za mtanange huo na kuwafanya Chelsea kupoteza mechi mbili mfululizo .
Mechi ijayo ya Chelsea ni katika dimba la Stamford Bridge dhidi ya West Brom siku ya Jumatatu usiku .
mzigo mkubwa wa mechi katika wiki kadhaa zilizopita zimepelekea kupatikana kwa majeruhi wengi katika kikosi ambacho Conte hapo awali aliwahi kuelezea kwamba ni kikosi kidogo na hiyo kuaminika kwamba moja ya sababu ya klabu hiyo kupata matokeo mabaya mwezi Januari na Februari.
Ross Barkley anakuwa mchezaji wa nane kuumia misuli ya nyuma ya paja msimu huu ndani ya kikosi cha Cheslea kabla ya mechi dhidi ya Watford ambapo David Luiz na Willian walirejeshwa haraka kikosini baada ya kutoka kwenye majeraha, hata hivyo Wabrazil hao walionekana hawapo kwenye kiwango kizuri.
Pedro naye anaonekana kwamba amejiunga katika orodha hiyo baada ya jana kutolewa nje akiwa ameumia akiunga na wakina Andreas Christensen, Alvaro Morata na Barkley katika chumba cha matibabu . Marcos Alonso aliachwa kikosini kwa sababu za tahadhari dhidi ya Watford lakini atarejea kikosini dhidi ya West Brom.
Lakini akiongea baada ya mechi Conte amekanusha kwamba maisha yake ndani ya Daraja yataamuliwa na wachezaji wake , ambapo mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameripotiwa kutua Jijini London kuangalia maendeleo ya klabu yake.
" Ni ngumu kwangu mimi kuhamisha fikra zangu. Ni matumaini yangu kwamba usiku huu mtanielewa, sina wasiwasi kuhusu kazi yangu . Nafanya kazi kila siku na najitoa kwa asilimia 100. Sina wasiwasi."
" Kila siku na kila mahojiano na waandishi wa habari naulizwa, lakini hapana. Kesho ni siku nyingine. Nafsi yangu ipo vizuri na naenda kulala vizuri. Najaribu kufanya kila kitu. Kama tatizo langu litakuwa la klabu basi sawa. Maisha yanaenda."
" Unadhani klabu itaamua kumfukuza kocha kama hakuna uungwaji wa mkono kutoka kwa wachezaji ? Nafikiri ni hapa tu , ni hapa tu ndio mnafikiria hivi. Mnafikiri kwamba wachezaji wana hii nguvu ? ndio ?. Hii sio sahihi.Sio sahihi kabisa. Kama ikitokea sawa."
" Lakini narudia katika maisha yangu nilivyokuwa mchezaji , nilikuwa nahodha wa Juventus, na sikuwahi kuthubutu hata siku moja kuongea kuhusu kocha na klabu yangu. Kama klabu ingejaribu kuniuliza, hilo sio tatizo langu."
" Jukumu langu ni kufanya kazi na hawa wachezaji na kuwa na wachezaji wakweli na wanafanya kazi kwa kujituma. tatizo ni kwamba nyie waandishi wa habari mnajaribu kutengeneza tatizo . nafanya kazi yangu. Na sina sababu ya kutolala vizuri."
" Matatizo - inabidi uyatafutie ufumbuzi kwa kufanya kazi. Hushindi kwa visingizio. katika maisha yangu napenda kuwa mshindi - na mimi ni mshindi."
Swea
*Sports Platform*