Bakayoko ameshindwa kuonyesha kile kilichotarajiwa kutoka kwake ingawa mchango wake kwenye timu bado ni muhimu, na Kante amemba Mfaransa huyo asaidiwe
Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante amesema kuwa timu yake ina jukumu la kumsaidia mchezaji mwenzao Tiemoue Bakayoko anapoendelea kuzoea maisha ya Ligi Kuu Uingereza.
Mfaransa Bakayoko, anahangaika kuonyesha tofauti Chelsea tangu atue London akitokea Monaco kwa £40m, alitolewa kipindi cha pili klabu hiyo ikifungwa 1-0 na West Ham Jumamosi.
Kante, ambaye ameshinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, ameitaka klabu kumsaidia Mfaransa mwenzake.
"[Bakayoko] anafanya mazoezi kwa bidii na anajitoa kikamilifu. Tunapaswa kumsaidia acheze katika ubora wake," Kante alikiambia Evening Standard.
"Je! Timu inawajibika kuweza kumsaidia kucheza katika kiwango bora? Naam. Lakini si Tiemoue pekee, kwa kila mtu. Ni budi tushirikiane kwa ajili ya mafanikio ya timu, kwa kujaribu kushinda mechi. Hilo ndilo tunalofanyia mazoezi.
Kama anahitaji ushauri, Naweza kumshauri. Lakini kama ilivyo kwenye kila klabu - jaribu kufanya mazoezi, elewa anachotaka kocha na ujitume dimbani. Ipo hivyo kila mahali."
Chelsea wataikabili Huddersfield Town Jumanne jioni wakitaka kurejea kwenye njia za ushindi baada ya kuangukia pua wikiendi.