Episode 12 B.
Koku.
Sikuweza hata kuangalia anayenivuta kutoka katikati mwa lile kundi la wakulungwa. Baadae aliyekua ananivuta akanisemesha, “inabidi ukakae kwetu kwanza, pale kwenu sio sehem salama tena", maneno yake ndo yalifanya nigundue aliyenitoa pale ni Habi. Kisha akaendelea kuniambia, “Hatukua tumefika mbali nikaona mmezingirwa na hao watu, ikabidi nirudi mbio kuwaokoa, bahati mbaya nimechelewa, pole sana", Habi aliendelea kunieleza huku akinipeleka kwao.
Pale kwa kina Habi wanaishi na mdogo wao wa kike ambaye kiasi tunaendana umri, so wakanisaidia nikapata nguo za kunisitiri. Nikikumbuka siku hii ilivyoanza na namna ilivyoisha naamini ule usemi wa kesho yako aijuaye Mungu tu. Nikiwa pale nikaanza kumuomba Habi anisaidie kuwapata mama na mdogo wangu, na akawa ameniahidi kufatilia. Bt kabla hajatoka baba yake akaingia.
Baba Habi akiwa na full magwanda ya polisi alionekana alikua kachoka, mawazo yangu alikua labda anasaidia kustopisha mauaji, kumbe yy ndo alikua kiongozi wa wauaji. Alipo niona pale cha kwanza kuuliza nafanya nn pale, “ww wazazi wako si ndo walikua wanawatetea hawa watusi, leo ndo mnaona nina faida kwenu!”, aliongea huku kanikazia mijicho. Habi akawa anajaribu kunitetea lakini mzee akawa kama haelewi.
Baada ya muda akaniambia niamke twende anipeleke alipo mama yangu. Sikua na namna nikaongozana nae. Gari yenyewe aliyokua kajimilikisha sasa ni ya akina Tall. Usiku ule tukakatiza mitaa kadhaa mpaka tukatokea nyumba moja kubwa. Baba Habi akamwambia mwanae ashuke afungue geti tukaingia ndani. Na kweli nikamkuta mama, she was tired bt alifurahi kuniona. Furaha yangu ilikua kumuona mdogo wangu. He was so innocent as if hakuna kinachoendelea. “kuanzia sasa nyie mko chini ya ulinzi wa polisi mkisubiri kusomewa mashtaka ya kuhifadhi magaidi", baba Habi alitupatia taarifa ambayo tangu mwanzo nlihisi. Maana angekua anataka kusaidia angetuweka pale kwake. Baada ya kuona kututetea hakuleti mafanikio, Habi akaomba walau aondoke na mdogo wangu. Baba yake naona hakupinga, so dogo akasepa na Habi.
Ile kuwa chini ya ulinzi ni kisingizio tu. Baba Habi alikua anataka kututumikisha kingono. Mwanzo alianza kuwa anamchukua mama anampeleka chumba kingine. Baadae kaanza kunibaka na mm. Nakumbuka the first time nilijitahidi kupambana nae bt he was so strong. Ikabidi nikubali matokeo. Baada kama ya wiki utaratibu ukabadilika. Hakua ana tuseparate tena, yaani nlikua nabakwa mbele ya mama yangu, nikimalizwa mimi anafata yeye. Kinachosikitisha zaidi, baada ya siku kadhaa mbele, akaanza kuleta maofisa wenzake wa polisi. Tulikua tunapigwa mande na watu hata watatu. It was sooooo painful. Kubakwa sio mchezo aisee.
Mpaka siku ya mwisho nlibaki kuomba Mungu aniondoe duniani. Nlikua nmeshahudumia wawili, mmoja ndo alikua juu yangu. Nikaanza hisi kama maombi yangu yanajibiwa. Mwili ulikosa nguvu, macho yakafunga, sauti nikawa ansikia kwa mbaliii sana. Baada ya muda ambao hata sikujua kiasi gani cha muda kimepita, nikasikia kama naitwa, then nikawa kama naona mtu mwenye nguo nyeupe akinibeba, nikajua ndo malaika wananipeleka zangu kwenye hukumu ya mwisho.
Nimekuja kuzinduka nipo kwenye gari. Kuangalia anayeendesha ni baba. I was so happy kumuona. Bt nliishia kulia tu. Baadae nauliza dogo alipo, baba akaniambia there was no time to get him, maana yeye yupo kwa kina Habi. Akitufikisha sisi atamrudia. Nlipomuuliza anatupeleka wapi, akanambia sehem pekee salama kwetu ni Tanzania.
Mara mbele tukaona roadblock, makundi ya wahutu yanasaka watusi. Mzee akasema, wakati wa kutuokoa ameua askari wawili, so huenda taarifa zake zimesambaa na anatafutwa. So ili kuwa safe inabidi tutembee kwa miguu. Tukashuka. Hakukua hata na ukaguzi wa maana, wanaangalia pua tu. Sisi tukapita ingawa wengi waliishia pale. Baada ya wmendo kama wa kilometa moja tukakutana na kundi kubwa la watusi wakitokea msituni. Nikajua walikua wanakwepa ile roadblock. Tukajiunga nao kutembea. Mara tukaona magari nyuma yetu, wale wenzetu wakawa washatambua ni wale wauaji, wakaanza kukimbia kutawanyika, ikabidi na sisi tufanye the same. Tukiwa tunakimbia polini tukaanza kusikia milio ya risasi.
Ndo ikawa utaratibu, tunatembea porini then tunarudi main road kama hali iko shwari. Muda wote tupo na lile kundi kubwa la wakimbizi wenzetu. Kufika usiku si wale wenzetu wakatugeuka. Kisa sisi wahutu wakatuhisi tupo pale kutoa direction yao na ndo maana tunavamiwa kila mara. Kukatokea ubishi pale, kuna baadhi walikua wanatutetea ila wengi wakataka tuuawe. Wakakubaliana watufunge kamba. Tukafungwa. Mida ya usiku mwingi, nikasikia kama inafunguliwa, kumcheki ni mmoja kati ya wale waliotaka tuuawe. Akanitoa pale kwa baba na mama kanipeleka vichakani. Kilichofata ni kilekile. Yaani both sides of the war fucked me.
Alivomaliza akanirudisha, then akamfungua mama. Nikawa kwa mbali nasikia tu sauti ya mgugumio wa yule mzee akimbaka mama. baada ya muda naona baba yangu akinifungua kamba. Kumbe muda wote alikua anajinasua. Akanipa maelekezo ya kukimbia, sikujua nielekee wapi so sikuenda popote. Yeye akasimama kwenda kumuokoa mkewe. Kabla hata hajamfikia yule mzee kuna watu washamuona, wakampigia yowe na kuanza kumkimbiza. Mzee nadhani alitaka kutupatia chance ya kutoroka, maana alikimbia kuelekea ndani zaidi ya msitu. Maza akaja tukaanza kuelekea uelekeo aliokimbilia mzee, bahati nzuri kuna mtusi mmoja akatuambia tukimbilie opposite direction na tusigeuke nyuma.
That was the last time nimemuona baba. Kufika road tukaendelea na safari kuelekea Tz. Mpaka kunakucha tukaanza kuiona nchi ya ahadi. Lakini ile tumekaribia kabisa, yaani geti tunaliona kaka mita 200 mbele, wakafika wahutu. Kwa kuwa tulikua tumeongozana na watusi baadhi, wakaanza kuwakatakata wale watusi. Bt kabla mauaji zaidi hayajatokea tukaanza kuona wale wauaji wanadondoka mmoja mmoja wakiwa na majeraha ya risasi za vichwa.
Baada ya muda, magari kama manne aina ya landrover na malori sita yaliyoandikwa JWTZ walifika tulipo, yakatupakia wakimbizi wote na kutuvusha mpaka. Nadhani walishindwa vumilia kuona mauaji yanafanyika mbele ya macho yao.
Kimsingi ndo nlivoingia tz. Baada ya miezi kadhaa ya maisha ya ukimbizi nikajigundua ni mjamzito. Wakati huo mama ashaanza kujitolea kama mhudum wa afya kwenye kambi ya wakimbizi. Sikujua mimba ni ya nani, ni wale polisi kule kigali, au ni yule mzee kule porini ambaye wakati huo tulikua nae pale kambini. Tena alikua na cheo kama mjumbe wetu. Alikua akiniona eti anatabasamu, he was pissing me off. Na ndo pale nilipoweka nadhili ya kuwaondoa duniani wabakaji wote walionipitia. Baada ya kujifungua mtoto nikamkabidhi mama. Nikatafuta cheti cha kuzaliwa kwa msaada wa mama na rafiki zake, na nikafanikiwa kuendelea na shule ingawa nilirudia form one kwa jina jipya Koku.
Nimekua naishi maisha ya siri. Hakuna ajuaye nilipo. Lengo langu ni kulipa kisasi. Ningekua na muda ningewasimulia namna nlivyomuondoa duniani yule mzee aliyenibaka porini. Bt itoshe kusema I will find them all.