Chanzo kikuu cha ajali za barabarani sio mwendo kasi (kwa mtazamo wangu)

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,274
Baada ya kufuatilia kwa karibu ajali zinazotokea mara kwa mara hasa zinazohusisha magari makubwa nimegundua kuwa, zaidi ya nusu zimesababishwa na overtaking (kupita gari la mbele bila kuchukua tahadhari. Mara nyingi mwendokasi umeweza kusababisha ajali pale dereva anapoacha kufuata taratibu na sheria za barabarani ikiwemo hiyo ya overtaking

Hivyo basi, nashauri kuwepo na kampeni ya kukumbusha madereva uhatari wa overtaking na wapi hawatakiwi kabisa kufanya hivyo au niseme kuovertake kwa kupiga ramli
Mimi napenda kukumbusha yafuatayo;
  1. Usi overtake kwenye kona kwani huwezi kujua kama kuna gari nyingine
  2. Usioveratake kwenye bonde kwani huwezi kujua nini unaweza kukutana nacho (gari/ Wanyama nk)
  3. Usiovertake kama gari la mbele limepunguza mwendo au kusimama kabla ya kujua kwa nini lipepunza
  4. Usiovertake kama gari lako halina nguvu ya kupita gari lililo mbele yako kwa haraka (mf malori mengi yana hii changamoto)
  5. Usiovertake kwa kufuata mkumbo au kufuta gari la mbele yako bila kujihakikishia usalama wako kwani yaweza kuwa mwenzako amejipimia umbali wake anaoweza kumaliza
  6. Usioveratke sehemu iliyokatanzwa hasa kama haujui kwa nini imekatazwa
  7. Usiovertake kama uko karibu na njia ya mchepuko au kusimama au kushusha abiria
  8. Usiovertake kwenye vivuko vya miguu/ bumps
  9. Usiovertake kwenye daraja
  10. Usiovertake kwenye Barabara nyembamba za nje yamji
Nawasilisha
 
Chanzo cha Ajali nyingi Ni kutokujali mkuu madereva wengi Wana hizo tabia SAsa Hapo ndipo hayo mambo mengine hutokea na upande wa Boda Boda nao Ni hivo hivo tabia zao za kutembelea mstari bila kufata tahadhari zozote na unakuta SAA zngne saa12 jioni au Kuna wingu na mvua Hapo Mara nyingi bodaboda ningumu kuzispot na tabia zao zakutembelea ubavuni na taa hawashi Sasa Kama dereva ukicheza kdg tu ushamgusa sababu anakua haonekani kirahisi na taa hawashi so Ajali nyingi Ni hio KUTOKUJALI
 
Binadamu wanatakiwa kukumbushwa kila wakati kwani kila leo kuna madereva wapya na wengine ni mara yao ya kwanza kupita hizo barabara

Lengo langu sio kukupinga bali wahusika aidha ni wazembe au hawajali au hawajui sheria za barabarani

Barabara zote lazima ziwe na Alama kila sehemu kuanzia speed kila baada ya mwendo lazima kuwe na ishara au signs ziwe za speed, kona na hata mteremko lazima kuwe na alama kuonyesha kuna mteremko au kuna kigongo

Lazima kuwe na alama kila sehemu mbona wenzetu wanaweka kila kona na hii husaidia sana madereva kujua kama kuna hatari mbele na aende kwa mwendo gani

Bongo barabarani unakuta alama moja ya speed zaidi ya maili 20 moja tu

Hata kama watasema wanaweka ila zinavunjwa sawa weka tena hata zege mwaga ili mradi kupunguza ajali
 
Vyanzo vikuu vya ajali kwa hapa nchini ni;
1. Ufukara
2. Barabara
2. Uchovu/Usingizi
3. Polisi
4. Uzembe
5. Mazoea

Asante.
 
Chanzo ni barabara mbovu na nyembamba,serikali ipanue barabara uione kama ajali hazitapungua
 
Nini kifaNyike?
1. Ubinafsi ukomeshwe
2. Umelo wa mali za umma utungiwe sheria za kifo, kifulisi na kufungia kizazi chochote.
3. Mfumo ufanye kazi, sio majina!
4. Walafi wasiachwe hai wala kwenye nafasi za utendaji au maamuzi.
5. Maslahi ya wanasiasa yashushwe au kutolewa kabisa!

Yakishindikana yote hayo, MAGUFULIFICATION ifanyike!

Ni punguani aina ya msoga ndo anaweza kubisha kuwa MAGUFULUFICATION haijatufunza jambo positive especially ukifanya comparison na ukiziiii-kazi.
 
Back
Top Bottom