Masi Lambo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 532
- 360
- Thread starter
- #61
Sikiliza kijana, mie sikutoa mada hii kujadili rais yeyote ila sie wote waafrika na ujinga wetu wa sayansi na tachnolojia tunaoukimbia kwa kuwatupia lawama viongozi wetu na kucheza siasa, siasa haitajenga madaraja na reli ila mchina kama sio siye. Ukileta hoja ya Magufuli sikujibu wala sisomi kama nilivyodharau jibu lako refu baada ya sentensi ya kwanza, sina muda huo wa kuongelea hayo.Kwa taarifa yako maswali ninayouliza haimaanishi nakulazimisha uyajibu. Hii ni mitego ya kujenga hoja ambazo huwezi kuzijibu na ukijaribu kujibu lazima utapotea.
Kiufupi tu ni kwamba nilitaka kukuonesha lwamba haihitaji kutoa muda zaidi kwa uongozi wa JPM ili tuhukumu kama hali ya uchumi itatengemaa au umasikini utaendelea kutamalaki kwasababu tayari anawekeza kwenye ujenzi unaoteketeza matrilioni ya shilingi badala ya kujikita kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba hadi sasa ambapo muhula wake wa kwanza unaelekea ukingoni, hakuna hata mradi mmoja uliokamilika ua hata nusu. Hii maana yake ni kwamba miradi hii itaendelea kuteketeza fedha hadi muhula wake wa mwisho na hakuna kitakachokamilika. Kwamaana hii nikisema JPM amechemsha na kwamba hataweza kuvunja rekodi ya kikwete ya kukuza uchumi kwa zaidi ya 8%.
Zaidi nataka nirekebeshe pale uliposema uimara wa thamani ya sarafu ndo kigezo cha hali nzuri ya chumi na eti kwavile kasi ya kushuka kwa thamani ya shilingi chini ya uongozi wa JPM ni ndogo ukilinganisha na enzi za JK maana yake uchumi umeimarika, si kweli.
Kwa taarifa yako tu ni kwamba sarafu (Dinar) za Kuwait, Bahrain na Oman zinaongoza kwa kuwa na kuwa na thamani kubwa duniani na zinashika nafasi tatu za kwanza katika orodha ya sarafu 10 zinazoongoza kwa thamani hapa duniani. Je, unatakata uchumi wa nchi hizi uko juu kuliko Marekani, China na Japani, Ujerumani na Uingereza nchi ambazo ni nambari moja kwa uwezo wa sayansi na teknolojia?
Naomba uwasiliane tena na rafiki zako wanaosomea uchumi Uingereza wakuelekeze vizuri kuhusu uchumi.