Jibu rahisi la waafrika wote ambalo wamepewa na mabeberu, la kwanini Afrika ni masikini, ni 'ubaya na kasoro za viongozi wetu'. Lakini jibu sahihi ni ukosefu wa ujuzi wa kisayansi na teknolojia, kuzalisha na kutengeneza bidhaa kwa kutumia malighafi na madini yetu. Kwa sababu sio rahisi kupata teknolojia za magharibi, walio wengi wana kimbilia kuamua ni viongozi wetu wenye kasoro.
Kwenye nchi yenye matatizo ya uongozi hat vita, ndipo mabeberu wanapopata mwanya wa kuingilia na kunyonya chochote mbele yao hata kuiba, kama walivyofanya Libya. Hivyo mabeberu kila siku watawarubuni muone viongozi wenu ni wabaya, watawapa silaha mpigane kama Congo, silaha zote zinatoka kwa mabeberu wa magharibi na mashariki.
Kwanza tuanze na ujuzi wa magharibi tuliokwama kuupata, mfano mdogo ni nguo za jeans. Nguo hizi zinatengenezwa na asilimia mia ya pamba ambayo tunazalisha hapa kwetu, lakini hatuwezi kutengeneza jeans, hivyo tunaagiza kutoka Ulaya kwa bei kubwa mara mia ya bei ya pamba tulio wauzia.
Hatuwezi kugoma kuwauzia pamba kwa bei wanayo tupangia kwa sababu itatuozea, hivyo tunauza kwa bei ya chini ambayo haikidhi mahitaji ya mkulima hata ya kununulia mbegu mpya na madawa ya mimea, wengie hata chakula.
Mfano wa pili ni madini yetu, wenzetu magharibi wanayatumia kutengeneza ndege, meli, magari, ndege zisizo na rubani, games for kids, simu, computers etc. Kwa hiyo madini kwao ni kitu ghali sana kukipata, ingawaje wanao wauzia wananunua kwa bei nafuu na rahisi sana kutoka kwetu, hata bure, wajinga wengine wanabadilishana na silaha za kuuana wenyewe kwa wenyewe, na kuvuruga nchi.
Wananunua bei rahisi toka kwetu sababu kwanza hayajasafishwa wanaponunua, pia matumizi yake kwetu ni kuvaa tu, hivyo thamani yake kwetu ni ndogo ingawaje tunaona mwenye madini ni tajiri sana. Yakifika Ulaya madini haya ni bei ya kununua nchi ya Afrika. SIjui kama tunaelewana kwenye hili somo la kidato cha kwanza?
Kuna malighafi nyingi tu ambazo Ulaya zinahitajika sana, kama glass, plastic, Sisal, wood etc, lakini kwetu vitu hivi vina matumizi madogo kulinganisha na wao wenye viwanda vya magari na majumba makubwa hata barabara na madaraja. Hawana cement Ulaya inatoka Afrika na Asia, lakini ni wajengaji wakubwa duniani baada ya China.
Mashariki ya kati na mbali wameishiwa mchanga wa kujengea madaraja na majumba, sasa China inatoa mchanga toka nchi jirani, ilichukua hata kwetu wakati wa Kikwete, ambaye namuweka katika kundi dogo la viongozi walio sababisha umasikini ukuwe Afrika, ila sio sababu kuu.
Ubunifu ni utamaduni wetu sio wazungu. Tuna wasomi ambao hawabuni chochote cha kusaidia jamii na hata wakibuni hawasifiwi. Tunathamini wanasiasa ambao ni walaji badala ya wabunifu na wafanyabiashara. Korea, Japan zimeendelezwa kwa ubunifu na biashara