Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Kwamba?

😂😂😂😂😂

Ndiyo maana Loliondo babu ana kikombe kutibu Corona.

Hiiiiii bagosha!
Yule mchato ni unfit physically and mentally since day one ndo maana alikuwa wa kwanza kwenda kunywa kikombe cha babu loliondo, ni uonevu mkubwa mtu aliyekuwa na file lake kubwa pale milembe kumsingizia eti kafa Sababu ya vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.
 
Nakumbuka mwanzo wa NIDA watu walikataa wakidai ni mambo ya uFirimasoni lakini serikali ilipata jinsi ya kuwabana mpaka kila mtu akakimbilia kujisajili. Na hili la corona litakua hivo hivo serikali inasema ni hiyari lakini najua kuna jinsi itawabana watu mpaka kila mtu atakimbilia chanjo

Mwanzo wa ngoma ni lele.

Hakuna mtu ana shadadia wengine kuchanjwa. Ila kutochanjwa kwa wajinga na wapumbavu (wawe wengi au wachache) hakuhalalishi kuwaweka wengine mashakani au hatarini.

Hiyo ni natural justice.

Mola wetu na akatujalie tusifike kwenye kulazimishana ili kila mmoja wetu na akabakie na m@vi yake.
 
Acheni ukuda wenu.
Mimi nikifa wewe unaumia nini? Lazima lazima ndio sitakufa au?

Acheni mambo ya ajabu bana. Hata wakisema leo lazima, sichanji ni bora waniue kuliko kuchanja.

Et unachanja kisa li ugonjwa la kutunga. Ujinga bana. Nikichanja then what? Sitaumwa? Sitakufa? I fear nothing to die when right time comes..
Nahisi wewe ni ndugu yangu! Salute mkuu
 
Yule mchato ni unfit physically and mentally since day one ndo maana alikuwa wa kwanza kwenda kunywa kikombe cha babu loliondo, ni uonevu mkubwa mtu aliyekuwa na file lake kubwa pale milembe kumsingizia eti kafa Sababu ya vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.

Usiyasahau mahaba niue ya Corona kwa wanaume, wazee na hasa wenye magonjwa mengine bila ya kuwasau waliowahi kupata kikombe cha babu enzi hizo.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Chanjo ndani ya mwaka mmoja jiulizeni tafiti ilichukua mda gani? Mpaka uhakika wa chanjo hiyo,,,,,Maisha ya watu hayawekwi rehani kiasi hicho tafadhal.
 
Mleta hoja,mbowe na wengine wote mnaleta ujinga wenu kusema chanjo eti iwe ni lazima, Ubongo wenu umejaa nduwi,

chanjo humlinda aliyechanjwa, hofu yako nini na wasiochanjwa?

Jinga kabisa
 
Unajipa umuhimu wa kichoko sana Wewe nyumbu wa Mbowe 🤣🤣🤣

images (4).jpeg

images (2).jpeg
 
Chanjo ndani ya mwaka mmoja jiulizeni tafiti ilichukua mda gani? Mpaka uhakika wa chanjo hiyo,,,,,Maisha ya watu hayawekwi rehani kiasi hicho tafadhal.

Ulitaka chanjo ndani ya muda gani mkuu?

Hata hivyo, hadi hapa tulipo ni hiari na inshallah itaendelea hivyo.
 
Tatizo sio chanjo tatizo ni hao waliotengeneza hiki kirusi kwa makusudi kabisa je wanalengo lipi na wanadamu???

Kama suala ni kifo mbona ni jambo la muda tu na kila mmoja atakionja!!

Ni kweli ugonjwa upo na unaua bahati nzuri ni kwamba kila kitu kimeshawekwa wazi juu ya madhumuni na lengo la hili gonjwa pamoja na chanjo yake

Hivyo kuanza kulazimishana chanjo ni upuuzi na kila mtu aishi maisha yake ilimradi hauvunji sheria na kanuni za nchi
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
Naomba unipe maana halis kwann mtu anachomwa chanjo?...tuanzie hapo...na chanzo maana yake nin...

Mfano mim nishaumwa korona.wadudu walishaingia mwilin mwangu...mwili ukatengeneza kinga ukapambana nikapona...maana yake nina kinga tayar..

Chanjo nijuavyo mim ni kwamba unaingiziwa wadudu mfu ili mwilk wako utambue na kutengeneza kinga dhid ya hao wadudu...

Sasa kwasisi ambao tushaumwa korona tukapona..mnatulazimishaje tudungwe chanjo?
 
Mleta hoja,mbowe na wengine wote mnaleta ujinga wenu kusema chanjo eti iwe ni lazima, Ubongo wenu umejaa nduwi,

chanjo humlinda aliyechanjwa, hofu yako nini na wasiochanjwa?

Jinga kabisa

Kutokuelewa kwako hakukufanyi wewe kuwa mwerevu na wengine kuwa wajinga kwa maoni yako tu.

No wonder babu Loliondo leo ana kikombe cha kutibu na kuzuia Corona na mamlaka zimeingiwa ganzi wasijue cha kufanya.

Yule babu mnyazi Mungu apishilie mbali ni muhimu kwa uhai wake apate chanjo, avae barakoa na awe mtumiaji mwaminifu wa vipikuzi haraka sana, vinginevyo atakuwa hatarini mno.

Ni bahati mbaya sana kuwa, kwa maslahi binafsi ya kisiasa, wanasiasa wameamua kuukumbatia ujinga wakiacha watu kufa mithili ya kuwatoa kafara.
 
Mkuu huo ni uchaguzi wako. Mapema kwa mwuungwana kama wewe niliandika hii:

View attachment 1860294

Kwamba sana sana Mbowe hakuwa na haja ya kuingia huku kisiasa, lakini si morally au kiuhalisia.

Kwamba hata aliingia huku inaonesha ni kiwango kipi huyu bwana ni a real selfless individual.

Cc: Salary Slip technically @erythrocytes
Haya mawazo yanatazamiwa yawe ktk kipindi cha miaka mingapi ijayo?

Je miaka kumi?

Kama ndivyo, basi haina maaana kabisa ya chanjo!

Unachanjwa na unaishi sawa tu wasiochanjwa kipindi cha miaka miiingi kiasi hiko, halafu bado unatazamia kuna watu wasio chanjwa watakufa, na wakati wewe mwenye chanjo ukiwa na hofu na chanjo yako ikiwa itakubakisha sawa kama ulivyokuwa kabla hujachanjwa ama la!!
 
Kutokuelewa kwako hakukufanyi wewe kuwa mwerevu na wengine kuwa wajinga kwa maoni yako tu.

No wonder babu Loliondo leo ana kikombe cha kutibu na kuzuia Corona na mamlaka zimeingiwa ganzi wasijue cha kufanya.

Yule babu mnyazi Mungu apishilie mbali ni muhimu kwa uhai wake apate chanjo, avae barakoa na awe mtumiaji mwaminifu wa vipikuzi haraka sana, vinginevyo atakuwa hatarini mno.

Ni bahati mbaya sana kuwa, kwa maslahi binafsi ya kisiasa, wanasiasa wameamua kuukumbatia ujinga wakiacha watu kufa mithili ya kuwatoa kafara.
Chanjwa ili usiambukizwe na wasiochanjwa, mbona unahasira kama siasa za Chadema bhana
 
Usiyasahau mahaba niue ya Corona kwa wanaume, wazee na hasa wenye magonjwa mengine bila ya kuwasau waliowahi kupata kikombe cha babu enzi hizo.

Au nasema uongo ndugu yangu?
Kuna magonjwa sugu ya miaka nenda rudi hayajaenda likizo ya kuua watu, nina babu zangu watano ktk mlela clan wamezaliwa mwaka 1928-1932 hawana habari na mibarakoa na wanapeta hadi Leo tangu ujio wa corona.
 
Haya mawazo yanatazamiwa yawe ktk kipindi cha miaka mingapi ijayo?

Je miaka kumi?

Kama ndivyo, basi haina maaana kabisa ya chanjo!

Unachanjwa na unaishi sawa tu wasiochanjwa kipindi cha miaka miiingi kiasi hiko, halafu bado unatazamia kuna watu wasio chanjwa watakufa, na wakati wewe mwenye chanjo ukiwa na hofu na chanjo yako ikiwa itakubakisha sawa kama ulivyokuwa kabla hujachanjwa ama la!!

Kama ni nia ni majadiliano ya hoja, basi shika kitu kimoja kimoja. Siyo kuruka ruka kama bisi kikaangoni.

Chagua tuanzie ipi?
 
Back
Top Bottom