LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 862
- 1,097
Kuna kitu hakipo sawa katika mitihani ya kidato cha nne na jinsi matokeo yalivyo. Nimeambatanisha matokeo ya shule moja ambayo wanafunzi wake wote wamepata daraja la kwanza lakini karibu wanafunzi wote wamepata pointi 7 ambazo ni Alama za juu kwa ufaulu kwa mwanafunzi.Na zipo shule nyingine za mfano huu...kama baraza la mitihani lilifanya makosa katika utungaji na upangaji wa maswali wahusika wachukuliwe hatua....haya siyo matokeo ya kawaida na kwa vyovyote vile utangazaji wa shule bora au wanafunzi ungefanya jamii kugundua hili....baraza la mitihani limenajisi elimu ya tanzania.