Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Kumbe hatuwezi kuweka mikoa bila barua, haya wanangu ety barua tunaandika kwa mkono au ku-typing.? Nimejaribu kuwapigia tamisemi ili niulize ila simu haitoki inakata yenyewe.
 
Uzi huu unaonesha tuna wasomi wengi vilaza mno, wanateseka na vitu vidogo vidogo sana.
Ukweli mchungu huu...

Pia inaonesha si wasomaji wazuri sababu mambo mengi yamewekwa/kuelezwa kwenye tangazo.
Kuna vitu vichache hawajaviainisha kwenye tangazo ndio vinahitaji ufafanuzi.
Mf: Wamesema wanaofanya kwenye mashirika waambatanishe mikataba yao lakini hakuna sehemu ya ku upload.
👉Hawajasema tu verify vyeti
 
Nimefanikiwa kutuma maombi muda huu teaching subjects zangu ni Geography na Economics , ila kilichoniuma ni baada ya kutoiona economics kule ndani , nimesikitika kuona hilo somo halina uhitaji. Maana nilitegemea lingenisaidia kwenye kupunguza ushindani .

Imeniuma sana hasa kila nikikaa vile nilivyokuwa nateseka nalo huku nikipigwa mikuki mikali ya Dr oswald mashindano , Dr osolo , madam mkenda , Dr joel bila kumsahau mdadila kumbe somo lenyewe hata siyo marketable kwenye uwanja wa ajiraaa .
Sehemu ya taarifa za chuo umefanyaje hadi ukafanikiwa kupajaza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ndugu zangu walimu na manesi hapa kosa la mtu wa IT ni lipi jamani?

Mbona mnapenda kutoa lawama sana.Haya unataka mtu wa IT afanye nini cha ziada hapa?

Nakupa elimu ya bure ili siku nyingine kabla ya kuponda IT wa bongo ujue nini kiko nyuma ya pazia.

Ni kwamba unapoingia kwenye browser yako na kutype address yako kwa ajili ya page hiyo ya maombi.Browser yako ndio inakuwa mteja na mhudumu wake ni hizo servers ambazo zina hiyo page.Ombi lako linapochelewa kushughulikiwa ni kwamba unakuwa umewekwa foleni kwa sababu server inakuwa imepokea maombi mengi na kila ombi linalotumwa linakuwa na mda wake wa kusubiri kabla ya kujibiwa.Mda wa kusubiri unaokuwa umepewa ukiisha bila kuhudiwa wewe unakuwa umetolewa kwenye foleni.

Sasa kama kwa kifupi sana jambo liko hivi kosa la IT wa bongo ni lipi sasa hapa?
Nakataa sababu zako.

Hivi Amazon, ebay zilizotapakaa Dunia nzima na kutumiwa na mamilioni ya watu ulimwenguni, huu usumbufu mbona haupo huko? Kama ni wingi wa watumiaji basi Amazon ingekuwa na foleni isiyo na kifani kwani inawatumiaji wengi sana.

Mbona page ya Wizara ya Afya iko vizuri hamna tatizo kama huku Tamisemi. Ma IT wa Tamisemi wanakwama sana
 
Ukiandika tu index namba na mwaka uliomaliza system inakuletea information zote mpaka jina la shule ulomaliza
Pia system inaweza kuprove scanned doxc na kama zipo tofauti na taarifa ilizodisplay inaikataa? hili swali ndio msingi wa kuwa doxc zinakataliwa na system
 
Back
Top Bottom