Changamoto mbalimbali kwa watumishi wanaohama vituo vya kazi na utatuzi wake

notyfeky

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
673
664
Habari za muda huu ndugu watumishi wa Umma.

Naomba uzi huu Uwe maalum kabisa kwa ajili ya kupeana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali zinazo wakabili watumishi wa umma kabla, wakati na baada ya kupata uhamisho wa kikazi.

Mfano Mimi binafsi niliomba uhamisho wa kubadilishana kituo cha kazi nikafanikiwa kuhama mwaka huu japo mwenzangu bado hajapata barua, changamoto imekuja katika kuhamisha mshahara, A/utumishi anadai niende Dodoma kwani mshahara umegoma kuhamia h/shauri mpya.

Hapa nawaza sijui nianzie wapi, maana uhamisho nimefuata taratibu Zote kuanzia ngazi ya kituo, wilaya hadi mkoani na barua nikatumiwa kupitia mwajiri wangu na nikafungashiwa taarifa vizuri, sasa tena uhamisho siyo halali kivipi?

Kama yupo aliewahi kukutana na changamoto hii atusaidie, yeye aliitatua vipi. Wapo pia Maafisa utumishi humu, watusaidie tafadhali.
Naomba kuwasilisha
 
Jukumu la kuhamisha mshahara ni la halmashaur uliyotoka. Wanatuma taarifa zako tamisemi wanaprove taarifa zinakwenda halmashauri uliyopo
 
Jukumu la kuhamisha mshahara ni la halmashaur uliyotoka. Wanatuma taarifa zako tamisemi wanaprove taarifa zinakwenda halmashauri uliyopo
Ndo wamenijibu mshahara umerudishwa jina langu halipo wakati nimebadilishana na mtu na barua wamenitumia wenyewe kupitia mwajiri wa awali, kama naenda Dodoma naanzia wapi sifahamu
 
Kama umefanya kimchongo malizana na wakurungwa, au waombe wakuongezee muda wa kumalizana nao.

Kama umefuata utaratibu zinguana nao tu, uwe unatembea na barua zote, nakala za kutosha.
 
Habari, ninachofahamu mimi ni kwamba kwenye ofisi uliyotoka unamfuata HR anayehusika na mfumo wa mishahara, yeye ataitisha faili lako kujiridhisha kama kweli umepata kibali cha kuhama, kama kupatikana na faili itakuwa shida, unamuonyesha barua ya uhamisho then atakuuliza check namba yako, na atakuuliza ofisi yako mpya unayokwenda. Basi moja kwa moja anakuwa anakutoa kwenye mfumo wa mshahara.

Kama kwenye ofisi ya awali hujatolewa kwenye mfumo hata ukienda kwenye ofisi mpya HR wa kule akiingia kwenye mfumo anakuwa hakuoni, kwahiyo HR mwingine anakwambia urudi kwenye ofisi uliyotoka uonane na HR wa Mfumo akutoe kwenye mfumo. na wala siyo process ndefu ni kitendo cha dakika kadhaa tu hapo hapo
 
Habari za muda huu ndugu watumishi wa Umma.

Naomba uzi huu Uwe maalum kabisa kwa ajili ya kupeana uzoefu kuhusu changamoto mbalimbali zinazo wakabili watumishi wa umma kabla, wakati na baada ya kupata uhamisho wa kikazi.

Mfano Mimi binafsi niliomba uhamisho wa kubadilishana kituo cha kazi nikafanikiwa kuhama mwaka huu japo mwenzangu bado hajapata barua, changamoto imekuja katika kuhamisha mshahara, A/utumishi anadai niende Dodoma kwani mshahara umegoma kuhamia h/shauri mpya.

Hapa nawaza sijui nianzie wapi, maana uhamisho nimefuata taratibu Zote kuanzia ngazi ya kituo, wilaya hadi mkoani na barua nikatumiwa kupitia mwajiri wangu na nikafungashiwa taarifa vizuri, sasa tena uhamisho siyo halali kivipi?

Kama yupo aliewahi kukutana na changamoto hii atusaidie, yeye aliitatua vipi. Wapo pia Maafisa utumishi humu, watusaidie tafadhali.
Naomba kuwasilisha
Acha haraka watahamisha katgts kako
 
Back
Top Bottom