Tamisemi lipeni Mishahara kwa vijana wa afya mliowapeleka katika Halmashauri mbalimbali Tanzania

Blackperson

Member
Feb 29, 2024
36
30
Kiukweli mimi ni miongoni mwa vijana wachache Tanzania.

Ambaye nimekubari kwamba mwanasiasa Amechukue Point Tatu katika utafutaji wa ajira niliopambana nao kwa muda mrefu.

Nikiwa katika lindi kubwa la mawazo baada ya mambo yangu kukwama kwa muda kidogo.

Mwezi wa kwanza Tarehe 26 mwaka huu katibu mkuu aliwatuita kazini kwa barua iliyowazi na kila mwananchi kuisoma.

Alitaka Tukaripoti katika Halmashauri zetu kama waajiriwa wa MKATABA na barua ilikuwa wazi kwamba mkataba utakuwa kati ya mwajiri ,Tamisemi na Halmashauri.

Mwezi wa pili Tulianza kazi kwa kupanga vituo vyetu vya kazi na kuamua kuanza maisha Maisha ya utumishi wa umma.

Matarajio Hayakuweza kuwa kama Tulivyotarajia na mambo yametuendea Kombo. Wanasiasa wamejipatia Point Tatu ya kwamba serikali imeajiri watumishi na kuwapeleka katika Halmashauri korofi na zenye vituo vipya vingi.

Hatujafanikiwa kuuona mshahara wowote hadi sasa na Tupo maeneo yetu ya kazi.

Tumevunja mikataba kwa waajiriwa wetu wa awali tukitarajia mambo mazuri lakini wanasiasa wametuacha tufe njaa.

Muda wametupotezea na hatma Yetu haijulikani

Kuanzia Halmashauri, Tamisemi Hakuna mwenye majibu yakueleweka na ukitarajia wao ndio waliotuita kazini.

Kiukweli Sisi Vijana Tunaomba Serikali wasitamani kujipatia kura kupitia sisi kwa kuonekana wameajiri watumishi wapya ilihali hawajali Utu wetu.

Mradi unaitwa Tanzania maternal and child health initiative (TMCHIP) mfadhili World bank serikali imeajiri watumishi wa mkataba 295 na kuwapeleka ka halmashauri zaidi ya 15 nchini ila imeshindwa kulipa mshahara.

Mambo kama Yamekuwa ndivyo sivyo wawaache vijana warudi majumbani maisha Hayakuwa magumu sana
Rai Yangu mwananchi usimwamini Mwanasiasa.
 
Shida ni kuwa mliajiriwa kimyakimya, ili wengine tusifahamu na Hayo ndio matokeo.. Hizo ajira za mkataba niliona tu mmechaguliwa lakini sikuwahi kuona tangazo la hizo ajira
 
Mchengerwa wizara yako kila siku inasemwa kwa mabaya tu.
Tuko kazini hatujalipwa na Tunafanya kazi maeneo korofi Tamisemi wamekaa kimya wanataka kutufanya sehemu ya kura za wananchi.
Tena wametupeleka kwenye vituo vya afya vipya ili waonekane wanafanya kazi lakjnj hakuna mishahara hadi leo kwa miezi miwili sasa?
 
Tuko kazini hatujalipwa na Tunafanya kazi maeneo korofi Tamisemi wamekaa kimya wanataka kutufanya sehemu ya kura za wananchi.
Tena wametupeleka kwenye vituo vya afya vipya ili waonekane wanafanya kazi lakjnj hakuna mishahara hadi leo kwa miezi miwili sasa?
Poleni sana mkuu, Halmashauri ni changamoto sana.

Inaumiza zaidi kama wengine walikuwa na kazi zao private wakaresign.
 
Poleni sana mkuu, Halmashauri ni changamoto sana.

Inaumiza zaidi kama wengine walikuwa na kazi zao private wakaresign.
Yes nimeresign sehemu nzuri sana na siwezi kurudi nimekuja kukutana na ujinga.

Halfu malipo yanatoka tamisemi HQ sio halmashauri
 
Back
Top Bottom