Mbona mnaiharakisha sana CHADEMA katika kusonga mbele jamani? Taratibu basi.. They need a break sometimes, wao sio marobot. There are a lot to come, but msitupelekeshe...
Ndugu yangu Hafif, nilitaka kushawishika na hoja yako. Lakini nimeiona kwamba ni baseless kwa kuwa haina research ya kutosha. Kwa nn katika hoja yako hujataja mikoa kama Kigoma,Iringa na Mbeya ambako hata huko pia kuna wabunge wa CDM? Mimi nahisi wewe unatumiwa na CCM kupractise devide and rule, ambayo ni propaganda ya CCM kuiua CDM kwa kutumia Udini na ukabila.
Soma historia ya Tanganyika vizuri anbayo imewekwa bayana sana mwanzoni tu wa mada hii.
Jiulize Kenya na Uganda kuna Ukabila mkubwa sna, Sisi Zanzibar kuna Uunguja na Uoemba, Vipi Tanganyika kwenye makabila zaidi ya 70?
Pitia historiia na kujua mbinu walizotumia wakoloni especially waingereza.
QUOTE]
Kwa hiyo unamaanisha CCM inatumia mbinu hizohizo kuugawa upinzani? Huko unakosema CHADEMA haiendi unahakika kuwa hakuna wafuasi? Ungekuwa wewe mwanasiasa ungetilia mkazo wapi kule amabako una hakika nako au kule kwenye mashaka zaidi?
Ndugu yangu nafikiri mada hii umeivamia katikati na unachokiandika wala hakina mantiki. lakini hata hivyo nitakusaidia kidogo tu na mengine soma vizuri katika fafanuzi zangu katika mada hii.Kwa mtazamo finyu waweza kusema hiyo ndiyo changamoto waliyonayo CHADEMA lakini hii si changamoto hata kidogo. Nataka niulize swali basic ili tuweze kuwa na mtazamo sawa katika hili. Ukitaka kuangusha mti mkubwa porini huanza kukata matawi ama shina lake?
Kwa mtazamo finyu mwingine atasema matawi, kwangu mimi nasema utaanza shina ili upepo utakapovuma hata kama bado shina halijafikia point ya mti kuanguka utakusaidia kuuangusha mti bila nguvu ya ziada kwa sabau mti huko porini in any direction waweza kuangushwa bila kuathiri chochote. Ninachotaka kukisema hapa ni kuangalia mikoa ile ambayo CDM imekubalika in three dimensional (3D) compared na mikoa ambayo mnasema haijakubalika in terms of education, financial, population, level of basic social services n.k. Kwa kuwa sasa jamii kubwa ya watanzania imeishaelimika kuhusu wajibu wa serikali kwa raia wake kuanzia mikoa ile mnayosema CDM wamejizatiti na kibaya zaidi ile mikoa iliyobaki hali ya kiuchumi na huduma za jamii zinakuwa ngumu zaidi ni dhahiri kabisa kuwa automatically CDM nako inakubalika zaidi ya vile mnavyofikiria nyinyi. Huwezi kumwimbia mtu ukabila, udini, au rangi wakati anaona kabisa unatumia vitu hivyo ili kumgawa na wenzake uzidi kumnyonya na kumkandamiza na hamna sehemu yatafanikiwa haya. Kwa tanzania changamoto ya ukanda, ukabila ama udini kama ambavyo inatumiwa na ccm as a propaganda ni kuishiwa vision na inaiangamiza ccm yenyewe! In summary ni kwamba CCM wanaimarisha matawi ya mti ambao CDM wako wanakata shina lake. Mikoa ambayo mnaisema kama changamoto are just a suplement in Tanzanian political environment.
Hali ya watu hao ki-elimu ikoje? Maana huenda CDM inaangalia welewa wa sehemu hizo zaidi. Kumbuka CDM si chama tawala chenye fedha nyingi, hivyo lazima kila move iwe a strategic move! Au siyo?
Unaandika kwa id moja, unaingia kwa nyingine unajigongea thanks na kukoment!
Very low.
Jina lenyewe HAFIFUHAFIF wewe ajenda zako ni chadema tuuu UMETUMWA!
Umejitahidi kushawishi ila umechemka CHADEMA si cha kidini....NINA WASIWASI NA WEWE kuwa ndo MDINI!
Jina lenyewe HAFIFU
HM Hafif said:Subiri subiri utamkuta mwana si wako. Vile vile Chadema iliasisiwa kama sikosei 1992 mpaka leo almost 20yrs bado hakijawa na mtazamo wa kitaifa je unahitaji muda gani tena?
Lazima ufahamu sisi hatuna serikali za majimbo. kwa hiyo msipobadili mitazamo yenu Chadema na kuwa na mtazamo wa kitaifa badala ule wenu wa sasa wa kikanda basi maisha yenu yooooooote hamta pata fursa ya kuitawala Tanzania kisharia.
Fikirieni hilo na liwe changamoto kwenu kuelekea uchaguzi wa 2015.
Jina lenyewe HAFIFU
Chadema ni chama cha siasa chenye changamoto nyingi sana hususan kukifanya chama hicho kiwe na sura ya kitaifa na sio kikanda, kikabila na kidini
Kwa sasa ni chama kilichoshika katika mikoa ya kanda ya ziwa, na kanda ya mashariki ambako ndio chimbuko na ngome yake kuu.
Lakini chama hiki mpaka leo kinatumia pesa nyingi sana kuelekeza sehemu hizo badala ya kuelekeza Tanga, Morogoro, Dar hususan temeke na kigamboni na ukonga , Mtwara, Lindi na visiwa vya unguja na Pemba ili kiwe na mtazamo wa kitaifa.
Najua wengi watauliza Chadema Dar ipo, lakini kwa mwenye akili utaona wazi waliposhinda ubunge ni ngome kubwa ya watu wa kaskazini. yaani watu wangi wa kaskazini utawapata mbezi, kimara, ubungo, chuo kikuu, sinza, samaki, mpaka boko. watu hawa ni very rare kuwaona temeke, mbagala n.k
Hiyo inazidi kuashiria kuwa chama hiki ni cha kikanda na kina harufu kali sana ya Udini ambayo kwa siri sana wanaitumia katika kupata majority support.
Mtazamo wangu ,CHADEMA ili kiweze kushika nchi yenu ni lazima kiwe chama cha kitaifa badala ya sasa kuwa Chama cha mikoa fulani au makabila fulani fulani.
Hiyo ni changamoto kwa Chadema.