Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,429
- 108,580
HM Hafif,
..as much as ningependa CDM wawe na wabunge wa kuchaguliwa toka pande zote za muungano, kupata wabunge toka Unguja au Pemba ni vigumu sana kwa wakati huu.
..itachukua muda mrefu na resources nyingi sana kuwabadilisha wananchi wa Unguja na Pemba kupigia kura vyama tofauti ya CCM na CUF.
..katika taaluma ya uchumi kuna kanuni inaitwa opportunity cost, sasa CDM wanapaswa kupima hasara na faida za kutafuta kura kwenye majimbo ya Zenj at the expense ya majimbo ya Tanganyika.
..mpaka sasa hivi chama chenye sura ya kitaifa[bara,visiwani,kaskazini,kusini,mashariki,magharibi,kati] ni CCM tu, sasa tujiulize chama hicho kimeweza vipi kufikia mafanikio hayo? pia vyama vyote vya upinzani havijaweza kuwa na sura ya kitaifa, je ni challenges zipi wanakutana nazo?
..bila shaka ili CDM waweze kushika serikali ya nchi hii wanapaswa kuongeza idadi ya wabunge na wapiga kura wao. now, how does CDM achieve that goal is up for debate. je, wanapaswa kujielekeza kwenye kanda chache zenye kura nyingi? au wajielekeze ktk maeneo mbalimbali na kuwa na support across the entire country?
Mkuu hauitaji degree kujuwa kwamba CCM ni muungano wa vyama viwili, yaani TANU na ASP, kwa hiyo ASP ikatowa wanachama upande wa Zanzibar na TANU ikatoa wanachama upande wa Tanganyika. lakini CHADEMA ni chama kimoja ambacho kinasimama kwa miguu yake na kinatafuta chenyewe wanachama wake pande zote katika mfumo mbovu wa kimuungano, ukumbuke vile vile CUF ni muungano wa vyama viwili, yaani CHAMA CHA WANANCHI cha James Mapalala na KAMAHURU cha Maalim Seif Shariff Hamad, ndio kikazaliwa Civic United Front CUF. ndio maana tunataka katiba mpya, sehemu kama Zanzibar iwe na vyama vyake yenyewe na wajitegemee kisiasa wao wenyewe.
Swali hivi tukianzisha shirikisho la kisiasa la East Africa kutakuwa na ulazima wa kuvunja hivi vyama tulivyonavyo ili kila chama kiwe ni cha East Africa nzima?