Ni miaka mingi sasa tangu CCM na vibaraka wake wakitumia propaganda ya Udini na Ukanda Kujaribu kuwaaminisha Watanzania kwamba Chadema chama kikuu cha upinzani na kinachobeba matumaini ya Watanzania ni chama cha Kikabila [wachaga] na ni ya kanda ya kaskazini.
Kinachonishangaza ni kitendo cha hawa wanaoikosoa Chadema kuendelea kungangania kubaki ktk chama kinachodaiwa ni cha kikabila na Kidini.
Kama kweli wanaona Chadema kiko hivyo si waachane nayo na kuunda au kujiunga na chama ambacho sio cha kikabila na kikanda?
Kuendelea kwao kuwepo ktk chama wanachokituhumu kuwa ni cha kibaguzi ni dhahiri kwamba wanacho kisema ni uongo na kwamba nyuma ya agenda yao hiyo kuna siri iliyojificha na ndio maana hawaondoki na badala yake wanaendelea kutumika ili kutimiza malengo ya wafadhili wao.