Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Mar 7, 2010.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Mar 7, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  - Ndugu zangu wananchi wote wa Tanzania mnaoishi mjini New york na vitongoji vyake, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Muda Ndugu Khaji, ninaomba kuwatangazia tangazo la tangulizo kuhusu kusajiliwa kwa chama kipya chenye lengo la kuwajumuisha Wa-Tanzania wote katika maeneo ya New York na vitongoji vyote vya karibu.

  - Sasa hivi chama hiki kipya kipo mbioni pia kuanzisha mtandao wake, yaani Website na pia kupata katiba yake kwa mujibu wa makubaliano ya wanachama, pia chama hiki kina viongozi wa muda ambao ndio hasa waliojitolea katika kuweka msingi wa hiki chama, ambacho baada ya kukamilika kwa usajili wake, tutasema rasmi ni lini kutakuwa na mkutano wa Wa-Tanzania wote, ili kuweza kupanga agenda za kujiaandaa na uchaguzi wa viongozi, pamoja na kupitisha katiba ya chama, ninarudia tena kwamba nia na madhumuni ni kuwajumuisha wananchi wote bila kumbagua yoyote yule.

  - Tungependa kupokea mawazo na new ideas zaidi, kuhusiana na chama kilipo sasa na mwendo wake mbele ya safari, ingawa kwa sasa tayari chama hiki kimeshapata baraka za Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa NY, ingekua vyema pia tukasikilzia mawazo na the new ideas za wananchi wote wa New York na wengineo pia, wote mnakaribishwa sana.

  Tutaendelea kufahamishana yatakayojiri mbele ya safari yetu, inshallah.

  Ahsanteni.


  William (CO) : Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano (Interim)
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nawatakieni kazi njema na wale wanaoishi maeneo mengine ya Marekani inakuaje kama mid west Kama Chigaco na Colorado
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Hiki ni chama cha siasa au ni chama cha kijamii kwa wakazi wa New York?. Kama sio chama cha siasa, hii post haijawekwa sehemu sitahiki!!!!

  Tiba
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  Ok,naunga mkono hiyo idea ya kuwaunganisha watanzania bila ubaguzi.

  Swali langu,ni kwa nini wameenda kupata baraka za balozi wa Tanzania umoja wa mataifa na si kutoka kwa balozi wa Tanzania Marekani?
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Khe khe khe kazi kwei kwei. Hiki ni Chama cha siasa au Chama cha namna gani?
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  Yaani mkuu hapo ni kipi cha kuchekesha,sijakuelewa bado

  Anyway,sidhani kama kuna chama cha sisa ambacho ni makini kitakachoanzishwa huko majuu.Nadhani labda ni chama cha jumuiya za watanzania.Lakini sijui kwa nini hawa wakuu wamepewa baraka from UN Ambassador and not from Tanzanian ambassador in Washington
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Kitazinduliwa na Dr Bi Majaar Sinare?
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  ???????
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Hapo cha kuchekesha ni kwamba hufahamu ni aina gani ya chama then unauliza kwa nini wamepata baraka kutoka kwa balozi wa UN na sio balozi wa USA anayetuwakilisha..
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Unashangaa nini?Hujasikia rumours kuhusu Ambassador Sinare wa UK kuhamishiwa US?
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  Mkuu usipende ligi za mchangani.Hebu soma hayo maelezo ya malecela kwa ufasaha,kasema chama cha kuwaunganisha watanzania wote bila ubaguzi.kwa uzoefu wangu ina maana havina tofauti na jumuiaya mbali mbali za watanzania.ndo maana nimeuliza mbona wameenda kwa mahiga ni si kwa Ombeni Sefue

  Otherwise angejibu kitu kingine tofauti na hapo
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hongereni,je ni nini lengo kuu la chama hiki?kinahusu nini hasa?
   
 13. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  1. Kwani ni lazima balozi atoe baraka za kuanzisha chama cha kijamii nchi ya ugenini? Mbona ukiritimba unaanza kabla hata chama hakijaanza?
  2. Kama ni hivyo ina maana serikali ya JK/CCM n.k. itakuwa na influence kwenye chama?
  Ingekuwa vema wale wote wenye kufanya kazi ubalozini na ndugu zao wasiwe viongozi kwenye chama ili kuondoa uwezekano wa serikali kukiingilia.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,634
  Likes Received: 9,129
  Trophy Points: 280
  This is a simple issue of proximity.

  Ubalozi wa Tanzania UN uko New York, na huyu balozi wa Tanzania UN, Dr. Mahiga, ni mmoja kati ya Watanzania wanaokaa New York, kwa hiyo mimi sioni shida as far as kumtaja yeye instead of Sefue, wewe ulitaka waende mpaka Washington DC kumtafuta Sefue wakati next door neighbor Mt. Vernon hapo kuna Dr. Mahiga? In any case hii endorsement si kwamba ni muhuri fulani wa kiofisi unaotakiwa kupitia protocol za kiserikali, ni kama vile unavyosikia Brad Pitt ame mu endorse Obama or some shyt like that, hakuna sehemu yoyote kwenye requirement kwamba chama cha Watanzania abroad lazima kisajiliwe na balozi. As far as I am concerned William anatumia jina la balozi ili kukipa chama chake legitimacy, gravita na legitimacy. Hakuna formal requirement.

  Now this brings me to my next point.

  Ningeona una point kama ungesema kwa nini hivi vyama vyama vya Watanzania vinapapatikia wanasiasa na ma bigwig period, kwani watu hawawezi kufanya shughuli za chama mpaka kupata "baraka" za balozi?

  Mnaweza kufikiri kwamba kwa kumtaja balozi mnaonyesha uzito wa chama, kwamba kimepata endorsement ya balozi, lakini kuna mafyatu wengine tuko so steeped in unorthodoxy tunaona kushirikisha sana watu wa serikali ni kama kutaka kutu monitor vile.

  Na ndiyo maana siwezi kujishughulisha na vyama hivi, hakuna kitu kinachofanywa na mkono wa wananchi wenyewe, kitu kidogo tu mpaka kipata baraka za balozi.

  Fvck serikali.

  Mwambieni Fred Nyaki or somebody like that atwange ngoma utaona wabongo wanakuja wenyewe.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,634
  Likes Received: 9,129
  Trophy Points: 280
  Mazee tunaandika pamoja, umeniwahi kidogo tu kwenye hiyo point ya ukiritimba.

  Kumbe na wewe umeiona siyo? Kitu kidogo, balozi.

  Wengine tunaojua ma espionage stratagem tunaweza kufikiri kuna some Orwellian ombudsmen pilfering our lines.
   
 16. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,367
  Likes Received: 1,953
  Trophy Points: 280
  Baraka za Ubalozi?he kazi ipo hizo baraka za nini au ndio mambo ya karibu na uchaguzi,shukeni tu huku jamani tupige kampeni
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  - Wakuu samahani sana nimezidiwa na shuguli, lakini nimefikisha mawazo yote yaliyotolewa hapa kwa Mwenyekiti wa Muda, ambaye leo nilikuwa naye Airport akiondoka kuelekea nyumbani, nitakapopata nafasi nitayajibu maswali yote bila kukosa hata moja, isipokuwa kwa leo nitagusa hoja moja tu ambayo naona imesemwa sana ya baraka za kiongozi wa serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hapa New York, yaani Balozi wetu wa kudumu kwenye umoja wa Mataifa:-

  - Kwanza tumesikia kuhusu kutafuta baraka pia za Balozi wetu DC, ila kwa sasa ilionekana na Mwenyekiti wa muda kwamba ni vyema kupata baraka za kiongozi wa juu sana hapa wa taifa hapa mjini, ingekwua kijijini tungetafuta baraka za wazee wa kijiji au Mwenyekiti wa kijiji, lakini kwa vile tuko ugenini basi baraka za kiongozi wa juu wa jamiii zilikuwa ni muhimu, kabla ya kuanza kutafuta baraka za wazee na watu wengine muhimu katika hii jamii, ikiwa ni pamoja na kupata nasaha zao kuhusu namna ya kuanzisha chama cha jumuiya ya wananchi.

  - Isipokuwa la kumjulisha Balozi wetu DC, tumelisikia tena kwa moyo mkunjufu sana tena kwa unyenyekevu mkubwa sana, inafurahisha sana kuona mawazo yenu wananchi mkitushauti namna ya kusonga mbele, badala ya mawazo ya kurudi nyuma, ambayo kwa kweli hatutayajibu kabisaa maana tunataka kusonga mbele.

  Tukipata nafasi tena tutaendelea na tulipoachia leo.

  Ahsanteni na Usiku Mwema.


  William Malecela: (Community Organizer).DI&R.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Mar 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,285
  Likes Received: 40,519
  Trophy Points: 280
  Nasikia Alhaj Abbas Byabusha atakuwa mwenyekiti...lol
   
 19. T

  Tom JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa ujumla hiki chama kimepata baraka za CCM, kwa kua Mabalozi wote hao wametokana na uteuzi wa serikali ya CCM. Sheria za huko zifuatwe, lakini kwa nini kisianzishwe tu bila baraka za hao mabalozi, mabalozi wanaweza tu kua wanachama kama watu wengine. Ukifanya hivyo hapo hata Wanacuf watajisikia kweli si chama cha kibaguzi.
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu Malecela,
  Naona na kakiburi tayari kameshawapanda hata kabla ya chama kuwa hai. Inaelekea mnataka kujibu maswali mnayoyapenda tu maana nyie ni above all others. Tufahamisheni basi ni maswali yepi ni ya kuwarudisha nyuma ambayo hamtaki kuyajibu ili tujue jinsi ya kuwauliza maswali.


  Sijui hizi tabia za baadhi ya watumishi wa ubalozini/serikalini wanaotegemea kinga za wazee wa CCM zitaisha lini ili kila ubongo wa Mtanzania uweze kutumika kwa manufaa ya nchi.

  Kama mnataka kuunda chama kwa ajili ya waTanzania kisichofungamana na siasa za nyumbani, basi inabidi kwanza muache hizi tabia zenu za kufikiria kuwa nyie wa ubalozini ni bora zaidi kuliko wengine. Otherwise msikiite chama cha waTanzania bali kiiteni cha watumishi wa ubalozini na wapambe wao.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...