Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community

Mkuu Malecela,
Naona na kakiburi tayari kameshawapanda hata kabla ya chama kuwa hai. Inaelekea mnataka kujibu maswali mnayoyapenda tu maana nyie ni above all others. Tufahamisheni basi ni maswali yepi ni ya kuwarudisha nyuma ambayo hamtaki kuyajibu ili tujue jinsi ya kuwauliza maswali.

Sijui hizi tabia za baadhi ya watumishi wa ubalozini/serikalini wanaotegemea kinga za wazee wa CCM zitaisha lini ili kila ubongo wa Mtanzania uweze kutumika kwa manufaa ya nchi.

Kama mnataka kuunda chama kwa ajili ya waTanzania kisichofungamana na siasa za nyumbani, basi inabidi kwanza muache hizi tabia zenu za kufikiria kuwa nyie wa ubalozini ni bora zaidi kuliko wengine. Otherwise msikiite chama cha waTanzania bali kiiteni cha watumishi wa ubalozini na wapambe wao.

Tatizo la watu kama hawa na wengine wanaojipenyeza kupata connections za ubalozi wanapenda sana kujitia kuanzisha vitu vya waTZ waishio nje wakati lengo ni kujinufaisha wenyewe binafsi. Cheap popularity ndizo zinazowafanya waongee hata vitu visivyokua na mshiko. Wanafikiri mawazo yao tu ndio lazima yawe sahihi,wanalimit idea za wenzao,that's so unbecoming!
When we are talking of critical thinking today some one from the so called jumuia ya wabongo huko comes up with things like "mawazo ya kurudi nyuma, ambayo kwa kweli hatutayajibu kabisaa maana tunataka kusonga mbele"
Haya "kila lakheri ktk kusonga mbele" ndio nature ya majibu unayotaka.
 
- Ndugu zangu wananchi wote wa Tanzania mnaoishi mjini New york na vitongoji vyake, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Muda Ndugu Khaji, ninaomba kuwatangazia tangazo la tangulizo kuhusu kusajiliwa kwa chama kipya chenye lengo la kuwajumuisha Wa-Tanzania wote katika maeneo ya New York na vitongoji vyote vya karibu.

- Sasa hivi chama hiki kipya kipo mbioni pia kuanzisha mtandao wake, yaani Website na pia kupata katiba yake kwa mujibu wa makubaliano ya wanachama, pia chama hiki kina viongozi wa muda ambao ndio hasa waliojitolea katika kuweka msingi wa hiki chama, ambacho baada ya kukamilika kwa usajili wake, tutasema rasmi ni lini kutakuwa na mkutano wa Wa-Tanzania wote, ili kuweza kupanga agenda za kujiaandaa na uchaguzi wa viongozi, pamoja na kupitisha katiba ya chama, ninarudia tena kwamba nia na madhumuni ni kuwajumuisha wananchi wote bila kumbagua yoyote yule.

- Tungependa kupokea mawazo na new ideas zaidi, kuhusiana na chama kilipo sasa na mwendo wake mbele ya safari, ingawa kwa sasa tayari chama hiki kimeshapata baraka za Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa NY, ingekua vyema pia tukasikilzia mawazo na the new ideas za wananchi wote wa New York na wengineo pia, wote mnakaribishwa sana.

Tutaendelea kufahamishana yatakayojiri mbele ya safari yetu, inshallah.

Ahsanteni.

William (CO) : Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano (Interim)
William, hongereni kwa mtizamo chanya juu ya hicho chama, ndio maana watu wanasema penye wengi hapaharibiki kitu.

Mie niko Tz lakini napata shida kidogo juu ya hili hasa nikirejea mapema 2006-07 mheshimiwa Kikwete alipotembelea USA kama kujitambulisha kuwa ndie mwenye Tz kuna picha na utambulisho ambao waTz wanaoishi America waliwakilishwa na Yassin Njayagha aliyejitambulisha kama rais wa waTz wanaoishi America mbele ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Niliona malumbano wengine wakimpinga na kufikia kumtuhumu kuwa hana hata mahala pa kulala na hana shughuli genuine ndani ya USA iweje atambulishwe/ ajitambulishe kwa Mheshimiwa Rais Kikwete, kulikuwa na picha zilizopigwa akiwa na Matinyi, Mh.Ngasongwa na baadhi ya wana usalama wetu. Mkuu wa Medani aliendelea kumwaga nondo kuwa huyu bwana alitumia upenyo wa kumfahamu Dkt Ngasongwa ili kujipenyeza mbele ya Rais na kujitambulisha.

Kwanza namuomba mkuu wa jamvi anipeperushie ile thread na zile picha.
Pili Mkuu William naamini mmejiandaa kujiepusha na kadhia kama lile na ndio maana ya kutangaza ujio wa org. hii mpya na uwepo rasimu ya katiba kwa walio tayari kujiunga.

Mkjj, FMES na wengineo nipatieni rejeo lile la 2006-07 tafadhari.
 
- Mwenyekiti wa muda bwana Khaji, ameondoka jana kwenda nyumbani visiwani Zanzibar, sasa atakaporudi ameahidi kuwatembelea all prominent people wa hapa mjini, yaani wazee ili sio tu kupata baraka bali hata kupata nasaha zao, na pia akama ilivyoshauriwa atatembelea DC kuonana na balozi wetu wa taiafa kule ili kupata nasaha na ushauri pia.

Otherwise, ndugu zangu tunawasikiliza kwa makini sana mawazo yenu mazuri sana, na pia eleweni kwamba sasa hivi hiki chama kina viongozi wa muda tu na ndio kwanza kimeanza kutambaa kama kitoto kichanga kinapoanza kutambaa, ndio maana tupo hapa kutafuta mawaidha hakuna mawaiddha madogo katika mambo kama haya, tunashukuru sana kwa uelewa wenu ulitukuka katika haya mambo ya kuanzisha vyama unaoonyeshwa na mawazo yenu wengi hapo juu.

Tutaendelea tukiwa na nafasi na baada ya kujadiliana na viongozi wenzangu wa muda , tunawashukuru watawala Jamiiforums kwa kutupa nafasi hapa uwanjani, maana haya yetu ndiyo hasa mambo ya jamiii.

Ahsanteni.

William: Community Organizer na Msemaji Wa Chama.
 
Napata shida kuelwa mantiki nzima ya hiyo org.
maana nayaona mafungamano dhahiri ya kiorg hicho na chama cha Mapinduzi, nayaona mafungamano yakimtandao, nayaona mafungamano chanya yak kurise fund kusaidia chama hicho, mimi naona ni aina nyingine ya jumuia ya Ccm inayoibuka, maana naziona nguvu za wanaCCM mnaoishi NY na London.
 
Jamani community organiser ameshaorganise, nasubiri mapanga shashashaaa, maana hachelewi, jamaa sijui nduguze ni waza naki. Natanguliza samahani CO (sijui wa kuchaguliwa au kujipachika).
 
- Wakuu samahani sana nimezidiwa na shuguli, lakini nimefikisha mawazo yote yaliyotolewa hapa kwa Mwenyekiti wa Muda, ambaye leo nilikuwa naye Airport akiondoka kuelekea nyumbani, nitakapopata nafasi nitayajibu maswali yote bila kukosa hata moja, isipokuwa kwa leo nitagusa hoja moja tu ambayo naona imesemwa sana ya baraka za kiongozi wa serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hapa New York, yaani Balozi wetu wa kudumu kwenye umoja wa Mataifa:-

- Kwanza tumesikia kuhusu kutafuta baraka pia za Balozi wetu DC, ila kwa sasa ilionekana na Mwenyekiti wa muda kwamba ni vyema kupata baraka za kiongozi wa juu sana hapa wa taifa hapa mjini, ingekwua kijijini tungetafuta baraka za wazee wa kijiji au Mwenyekiti wa kijiji, lakini kwa vile tuko ugenini basi baraka za kiongozi wa juu wa jamiii zilikuwa ni muhimu, kabla ya kuanza kutafuta baraka za wazee na watu wengine muhimu katika hii jamii, ikiwa ni pamoja na kupata nasaha zao kuhusu namna ya kuanzisha chama cha jumuiya ya wananchi.

- Isipokuwa la kumjulisha Balozi wetu DC, tumelisikia tena kwa moyo mkunjufu sana tena kwa unyenyekevu mkubwa sana, inafurahisha sana kuona mawazo yenu wananchi mkitushauti namna ya kusonga mbele, badala ya mawazo ya kurudi nyuma, ambayo kwa kweli hatutayajibu kabisaa maana tunataka kusonga mbele.

Tukipata nafasi tena tutaendelea na tulipoachia leo.

Ahsanteni na Usiku Mwema.

William Malecela: (Community Organizer).DI&R.

Mkuu nashukuru kwa kujibu hoja vizuri maanke kuna wengine walidandia na kuanza debate za mchangani
 
Unashangaa nini?Hujasikia rumours kuhusu Ambassador Sinare wa UK kuhamishiwa US?

Mkuu JMUSH1,

Mimi na wewe tunatofautiana sana,wewe unafanyia kazi na kutumikia tetesi na gossips but mimi nafuata itifaki.So far balozi wa Tanzania Marekani ni nani? Yaani wewe ni kama vile kila Rumours una-assume ni kweli,una safari ndefu mkuu!
 
Wakuu kuhusu hii ishu mimi sipingi balozi Mahiga kuombwa baraka kuanzisha hiyo jumuiya but nilitaka kueleweshwa.

Pia,Mimi naona Balozi wa Tanzania kuhusishwa ni sawa kwani hiyo ni jumuiya ya watanzania.Kuna mdau kasema sijui wasingehusisha balozi ili watanzania wote i mean CUF,CHADEMA na CCM wawe huru kujiunga,lakini ni sahihi kwa balozi kuhusishwa kwani kwenye ile nchi balozi ndiye msimamizi wa maslahi ya watanzania.Kama hiyo jumuiya inataka kutambulika rasmi basi ni lazima/muhimu balozi wao ahusishwe ili mradi balozi asilete unazi wa chama katika hiyo jumuiya na viongozi pia wajikite katika hayo malengo makuu.Naona lengo ni kuunganisha watanzania bila kujali itikadi za vyama,dini kabila nk

Tukipinga balozi kuhusishwa ni sawa na tumekubaliana na na yale wanayofanya mabalozi wetu nchi nyingine kwa kuanzisha na kubariki matawi ya vyama vya siasa ambavyo vinawagawa watanzania walioko nje ya nchi badala ya kuwaunganisha kwani hilo pia ni moja wapo ya malengo ya balozi zetu nje coz huwezi simamia maslahi na haki za watanzania nje ya nchi huku ukiwa umewagawa.

Mkuu,Willium na Watanzania wa New York,nawapa hongera kwa hiyo move kama lengo kuu ni kuwaunganisha watanzania bila kujali itikadi zao
 
Hongereni,je ni nini lengo kuu la chama hiki?kinahusu nini hasa?

- Ndugu yangu naomba uwe na amani chama ni cha jumuiya chenye nia ya kuunganisha wananchi wote wanoishi New York City na vitongoji vyake, kuna misiba, kuna maafa, kuna mambo mengi sana ya kijamii na cha muhimu kuliko vyote ni kuwa pamoja.

Ahsante.

William. (CO)
 
  1. Kwani ni lazima balozi atoe baraka za kuanzisha chama cha kijamii nchi ya ugenini? Mbona ukiritimba unaanza kabla hata chama hakijaanza?
  2. Kama ni hivyo ina maana serikali ya JK/CCM n.k. itakuwa na influence kwenye chama?
Ingekuwa vema wale wote wenye kufanya kazi ubalozini na ndugu zao wasiwe viongozi kwenye chama ili kuondoa uwezekano wa serikali kukiingilia.

- Ni lazima kupata baraka za wazee wa kiserikali na kijamii pia, ndio maana baada ya kukutana na Balozi, Mwenyekiti wa muda alikutana na wazee kama Proffesor Mtui na Proffesor Lwiza, kupata baraka zao, mabalozi wanapomaliza muda wao wanarudi nyumbani, chama na wazee kama hawa ma-proffesor wapo hawaendi kokote, wananchi wote walioko New York wanatakiwa kisheria kujiandikisha ubalozini wanapofika tu nchi za kigeni, sasa siwezi kusema kwamba wanategemea kuishi ki-CCM au kuingiliwa na serikali wakiwa hapo kwenye nchi.

- Tutaendelea na kutafuta baraka na nasaha za wazee na viongozi wa taifa walioko nje, sio kuvunja sheria, ispokuwa ni kutafuta mawaidha tu. Kuja kwetu hapa haina maana kwamba chama kitakuwa cha JF, au kitaamuliwa anything na JF, otherwise ahsante sana kwa baadhi ya mawazo yako mengine.

Ahsante

William. (CO)
 
Mkuu JMUSH1,

Mimi na wewe tunatofautiana sana,wewe unafanyia kazi na kutumikia tetesi na gossips but mimi nafuata itifaki.So far balozi wa Tanzania Marekani ni nani? Yaani wewe ni kama vile kila Rumours una-assume ni kweli,una safari ndefu mkuu!

We yako fupi huh?Wewe ulipo qoute posting yangu kwa question marks ulikuwa na maana gani?Wewe ndiye uliassume kuwa nilimaanisha kuwa Balozi Majaar yuko tayari US?Ama na wewe unatafsiri word to word?Yani wewe uliassume kuwa nimesema kwa hakika kabisa kuwa Bi Majaar ndiye atakayefungua chama hicho,sasa tizama safari yako na wewe uone huo ufupi wake.
 
Mkuu ikiwezekana tuwekee memo na bylaws. Hicho chama and/or organization ni 501 C 3?
 
Mkuu ikiwezekana tuwekee memo na bylaws. Hicho chama and/or organization ni 501 C 3?

- Mkuu ahsante sana ndugu yangu, huko kote bado hatujafika ndio maana tunatafuta ushauri na mawaidha, na itawekwa siku maalumu ya kukutana ili kuyaangalia yote yanayoshauriwa, na kuwasikia wananchi wenyewe. Lakini ninakukaribisha sana maana wewe najua una uzoefu mkubwa sana kutokana na profesional yako, tunahitaji ushauri wako wa kazi zako za ki-CEO ili kuendesha chama.

- Na ni matumaini yangu kwamba utachukua fomu ya uongozi when the times comes ya kuchagua viongozi wa kudumu wa chama.

Ahsante.

William.
 
Mkuu Malecela,
Naona na kakiburi tayari kameshawapanda hata kabla ya chama kuwa hai. Inaelekea mnataka kujibu maswali mnayoyapenda tu maana nyie ni above all others. Tufahamisheni basi ni maswali yepi ni ya kuwarudisha nyuma ambayo hamtaki kuyajibu ili tujue jinsi ya kuwauliza maswali.

Sijui hizi tabia za baadhi ya watumishi wa ubalozini/serikalini wanaotegemea kinga za wazee wa CCM zitaisha lini ili kila ubongo wa Mtanzania uweze kutumika kwa manufaa ya nchi.

Kama mnataka kuunda chama kwa ajili ya waTanzania kisichofungamana na siasa za nyumbani, basi inabidi kwanza muache hizi tabia zenu za kufikiria kuwa nyie wa ubalozini ni bora zaidi kuliko wengine. Otherwise msikiite chama cha waTanzania bali kiiteni cha watumishi wa ubalozini na wapambe wao.

- Ahsante sana ndugu kwa ushauri wako mzito sana, ndio maana tukaja hapa kwenye Great Thinkers ni ili kupata ushauri mzito kama huu wako.

Ahsante.

William.
 
Tatizo la watu kama hawa na wengine wanaojipenyeza kupata connections za ubalozi wanapenda sana kujitia kuanzisha vitu vya waTZ waishio nje wakati lengo ni kujinufaisha wenyewe binafsi. Cheap popularity ndizo zinazowafanya waongee hata vitu visivyokua na mshiko. Wanafikiri mawazo yao tu ndio lazima yawe sahihi,wanalimit idea za wenzao,that's so unbecoming!
When we are talking of critical thinking today some one from the so called jumuia ya wabongo huko comes up with things like "mawazo ya kurudi nyuma, ambayo kwa kweli hatutayajibu kabisaa maana tunataka kusonga mbele"
Haya "kila lakheri ktk kusonga mbele" ndio nature ya majibu unayotaka.

- Haya tumekusikia sana mkuu na hii Great Thinking, I mean tuko at the right place, yaani kuja kutafuta mawazo ya kuendeleza chama hapa JF. ila sometimes mnahitaji kuwahurumia wananchi wa NYC waliokaa miaka 47 bila chama cha kuwajumuisha ugenini.

Ahsante.

William.
 
Napata shida kuelwa mantiki nzima ya hiyo org.
maana nayaona mafungamano dhahiri ya kiorg hicho na chama cha Mapinduzi, nayaona mafungamano yakimtandao, nayaona mafungamano chanya yak kurise fund kusaidia chama hicho, mimi naona ni aina nyingine ya jumuia ya Ccm inayoibuka, maana naziona nguvu za wanaCCM mnaoishi NY na London.

- Sawa sawa mawazo mazuri sana tutayawakilisha kwenye kikao cha wananchi wote tutakapokutana kuanza rasmi msingi wa chama.

Ahsante.

William.
 
Jamani community organiser ameshaorganise, nasubiri mapanga shashashaaa, maana hachelewi, jamaa sijui nduguze ni waza naki. Natanguliza samahani CO (sijui wa kuchaguliwa au kujipachika).

- Tunachohitaji hapa ni mawazo ya kuendeleza chama, kama unataka ya kunijua mimi binafsi, namba yangu ya simu ni 914-473-1033 tunaweza kuongea ninakufahamisha, nipigie anytime.

Naona signnature ya uCO umeshaivua. Naona umemwaga namba yako, thanks but no thanks.
 
Back
Top Bottom