William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
- Thread starter
- #121
Soon nitaweka nia na madhumuni ya chama hapa,utaona kwamba hatuna mpango wa kujiingiza kwenye siasa za taifa lolote iwe US wala Tanzania, sio nia yetu hiyo[/FONT][/COLOR], una maana kuwa chama tayari kimezaliwa? Hayo si madhumuni, bali ni tentative tu hadi hapo wanachma watakapoyakubali.
- Chama kilishazaliwa tayari, na wanachi walijitokeza na kuchagua viongozi wa muda, kinachofuatia ni kukubaliana kuhusu katiba na how to go about it na ndio maana ya kuja kutafuta ushauri hapa na mawaidha, ila kama nilivyosema kwamba hakuna member hapa wala kiongozi wa muda, na kwa hiyo ni uamuzi wetu chama kuchukua mawaidha muhimu tu ambayo tutayaona yanatufaa kuendeleza chama.
Kulingana na usemi wako, website na katiba itatolewa. Je, kwa nini muanze kutengeneza website na kutunga katiba na hali chama hakijazaliwa?
- Chama kilishazaliwa tayari, na wanachama wapya walishakutana na kuchagua viongozi wa muda, kuna hela zilichangwa na wanachama na kufungua account ya chama tayari, website iko mbioni na Mwenyekiti wa muda amerudi leo asubuhi tayari, kwa hiyo tutatafuta siku na kuamua tunafanya nini next.
Itafaa sana kuwataja wale waliokutana hapo Harlem, sijui kwa nani na kuanzisha wazo la kuunda chama? Tupe majina yao. Ili chama kianze na unquestionable transparency.
- Hawatatajwa humu ndani ya forums, ila ukijiunga na hiki chama unaweza kuuliza kwenye vikao na utaambwia ni kina nani, hapa hatuko obligated kufuata amri yoyote ya wachangiaji, ila tuko hapa kupata ushauri tu!
Kwa nini hujaweka majina ya wanakamati ya kutayarisha kumuaga Balozi Mwakawago (marehemu sasa)? Ndio mlitayarisha hafla ya kumuuga Balozi Mwakawago. Je, mlimuaga Balozi Foum na kumkaribisha Balozi Chagula? Mlimuaga Balozi Chagula na kumkaribisha Balozi Nyaki? Mlimuaga Balozi Nyaki na kumkaribisha Balozi Mwakawago? Je, mlimkaribisha Balozi Mahiga? Je, mlimkaribisha Balozi wa ma-Balozi Asha Migiro?
- Tumewahi kuwaaga balozi Chagula, Mwakawago na kumkaribisha Mama Migiro ingawa nimeijibu hii haina uhusiano wowote na hiki chama kipya ila ilikuwa kuweka sawa tu the record.
Mwisho, ni lazima iwepo sababu ya kumuaga Balozi Mwakawago na hata kuomboleza kifo chake! Kuna wenye kuamaini kuwa sababu hiyo imejikita sana katika u-dini kwa baadhi ya Watanzania hapo NY
- Balozi Mwakawago alikua mtu wa watu, ndio maana aliagwa na wananchi karibu wote na majuzi pia aliombolezwa na karibu wananchi wote wa NY, binafsi nilikuwa ninamfahamu sana toka nikiwa mdogo.
- Mkuu kama nilivyoahidi nitagusa yaliyo muhimu tu kwa chama, yale niliyoyaacha yote ni kwa sababu hayana umuhimu wowote kwa chama chetu kipya.
Ahsante Sana.
William. (Community Organizer na Msemaji wa Chama).