Yawezekana siko sahihi,lakini habari za ujio wa chama kipya cha siasa, Chama Cha Jamii (CCJ), zimenipa hofu hasa kwa namna zilivyopokelewa mithili ya habari njema.
Kwanza,kuna ulinganifu unaofanywa kuhusu kuzaliwa kwa CCJ na utabiri wa Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM.Pamoja na heshima kubwa niliyonayo kwa Baba wa Taifa,lakini mie na wewe tunafahamu kuwa Mwalimu alikuwa binadamu na si malaika, hivyo utabiri wake haumaanishi usahihi wa asilimia 100. Lakini la muhimu zaidi ni mchango wa Mwalimu katika kutufikisha hapa tulipo sasa. Sote tunakumbuka kuwa Nyerere alimpigia debe la nguvu Ben Mkapa kuwa rais wetu. Sihitaji kuingia kwa undani kuhusu namna Mkapa alivyolipeleka mrama taifa letu, huku akijitengenezea utajiri mkubwa kwa mgongo wa kubeba wawekezaji.
Je Mkapa alivaa ngozi ya kondoo kiasi kwamba Nyerere hakujua kuwa huyo ni mbwa mwitu? Lakini si Mkapa pekee. Takriban kundi lote la mafisadi, with exception of kizazi kidogo kilichojitokeza baada ya utawala wa Mwalimu, ni watu waliokuwa karibu sana na Baba wa Taifa. Kingunge, swahiba mkubwa wa Mwalimu, ni mwanasiasa aliyetuaminisha kuwa ni Mjamaa halisi lakini sote sasa twajua kuwa lile lilikuwa changa la macho.Je Mwalimu alikuwa naive kuwaamini watu hawa?Nadhani hilo litakuwa jibu rahisi kwa swali gumu. Kitu kilicho bayana ni ukweli kwamba Mwalimu alikuwa akipenda sana kusikilizwa,na wakati huohuo akichukia sana kupingwa. Wajanja walilifahamu hilo,wakamsapoti kwa kila alilosema, naye akawaamini kama vijana wake. Kumbe wao walikuwa wakisubiri wakati mwafaka wa kutunisha misuli na kutoa makucha yao, huku wakishibisha akaunti zao nje ya nchi. Si kweli kwamba ufisadi ni phenomenon iliyochipuka ghafla bali ni matokeo ya mfumo uliolelewa kwa muda mrefu tangu tupate uhuru.
Kufupisha mjadala, kwa mantiki hiyo,hata kama kuzaliwa kwa CCJ ni kutimia kwa utabiri wa Mwalimu, haimaanishi kwamba tutarajie mapya sana kutoka kwa chama hicho kwa vile historia inatuonyesha kuwa si kila aliloamini Mwalimu lilizaa mema kwa taifa.
Pili,habari kwamba wengi wa waasisi wa CCJ ni vigogo wa CCM inapaswa kutufanya sote tukiangalie chama hicho kipya kwa jicho la mashaka. CCM, kama tunavyofahamu wengi, imegeuka kuwa kama Al-Qaeda. Imetanuka kutoka taasisi ya kisiasa na kuwa kama itikadi, na ndio maana leo hii ukijiuliza chama hicho kinafuata itikadi gani utapata majibu ya ajabu ajabu. Kama ilivyo kwa ujamaa,CCM imekuwa mithili ya mfumo unaoamini kiongozi yuko sawa muda wote, uheshimiwa wa kiongozi, kulindana, na kudumisha ufisadi in the name of umoja wa kitaifa. Je vigogo hawa wa CCM ambao sasa wameamua kuja na chama chao si sehemu ya mfumo huohuo tunaoupigia kelele?
Kinachonipa hofu zaidi ni ukweli kwamba vigogo hao wako mguu mmoja ndani mguu mmoja nje katika mahaba yao na CCM.Wanaogopa hata kujiweka wazi hadharani. Tayari baadhi ya wachambuzi wa siasa zetu (na wako wengi kweli hasa msimu huu wa uchaguzi) wanadai kuwa vuguvugu la CCJ ni shinikizo tu kwa JK kuchukua hatua dhidi ya mafisadi. Kwa lugha nyingine, uhai au ustawi wa CCJ unategemea actions from JK. Yaani hatma nzima ya chama mbadala inatarajia matendo ya mtu ambaye ni katika taifa la aina yetu tu bado yuko madarakani kwa uongozi wake hafifu na uliokosa mwelekeo. What if akiamua "kutuzuga" sie na hao jamaa wa CCJ kwa kuchukua hatua tulizokuwa tukipigia kelele kila siku? Kwa taarifa tu, wanasiasa wanaogombea nafasi za uongozi hupendelea kuja na ajenda za kuwaridhisha wapiga kura kwa mfumo wa ahadi au hata vitendo-vyote vikiwa ni vya muda mfupi, vitakavyomwezesha mwanasiasa husika kukubalika na hatimaye kuingia au kurejea madarakani. Na kwa vile katiba yetu haitoi upenyo mzuri wa kumwajibisha kiongozi huyo pindi akiamua kutotekeleza ahadi alizotoa wakati tunamwomba atuchague,basi ni dhahiri anakuwa na fursa nzuri ya kuendelea na usanii wake akishaingia/rejea madarakani.
Tatu, jambo moja ambalo wengi wetu hatulitilii maanani ni nafasi ya vyombo vya dola katika kuhujumu demokrasia.Na si kosa la makusudi kwa vile shughuli hiyo hufanyika kwa siri kama ambavyo nature ya vyombo hivyo ilivyo.Tayari kuna tetesi kuwa baadhi ya vigogo wanaosemekana kuwa waasisi wa CCJ wameshaanza kuhojiwa na vyombo vya dola. Changanya hilo na habari kwamba JK anadai hayuko tayari kuiona CCM ikimfia mikononi mwake, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na CCJ iliyopandikizwa vibaraka watakaopelekea yaleyale ya NCCR Mageuzi. Si ajabu pia CCJ ikawa kiini macho na usanii wa taasisi flani ku-deflect attention yetu kwenye vita dhidi ya ufisadi na kupata tumaini hewa kuwa "aaah sasa CCM lazima iwe tumbo joto kwa vile ikicheza tu inaondolewa na CCJ". Huu unaweza kuwa mchezo wa kuigiza, trust me!
Nne, hata kama CCJ is a real and genuine thing, si habari njema sana kwa akina sie tunaodhani kuwa kuna vyama pinzani, kama Chadema ambavyo angalau vimetuonyesha dhamira na uwezo wa kuchuana na CCM. I don't think CCM-B (tafsiri yangu ya CCJ) inaweza katika muda huu mfupi uliobaki kufanya yale tunayotarajia kutoka kwa chama cha upinzani. As I mentioned earlier, CCM ni zaidi ya chama, ni mithili ya mfumo uliotapakaa nchi nzima na hadi nje ya nchi. Kuna sehemu kadhaa hasa vijijini ambako ugumu wa kutenganisha CCM na serikali ni zaidi ya ule wa kutenganisha atom kijiweni (wanasayansi wanaelewa hilo). Kwa chama kinachozaliwa miezi michache tu kabla ya uchaguzi kujipanga kisawasawa kuung'oa mfumo ulio katika shepu ya chama (CCM) inaweza kuhitaji zaidi ya mbinu za kisiasa.Na kwa vile Tanzania ni quasi-military/security state, tutake tusitake ni lazima CCJ ikubalike miongoni mwa taasisi hizo vinginevyo itaendelea kuwa kwenye top list ya hujuma dhidi yake kutoka kwa taasisi hizo.Na hilo si rahisi kwa vile wengi kwenye taasisi hizo bado wanaishi kwenye fikra za chama kimoja,na kwamba upinzani au tishio lolote kwa CCM is tantamount to kutishia uhai wa taasisi hizo.
Mwisho, CCJ inakuja kugawa kura za Upinzani. Na hiyo si habari njema kwa wanaotaka kuona CCM inaondoka madarakani. Ni habari mbaya zaidi kwa vile umaarufu wa CCJ (kama itaupata) unaweza kuwa si kwa vile ni chama kinachotarajiwa kuleta mabadiliko ya kweli (forget the katiba thing, ni maneno tu kama yalivyo kwenye katiba ya CCM) bali ugonjwa unaotafuna Tanzania na pengine sehemu kubwa ya Afrika wa siasa za haiba. Kuna waliompigia kura JK kwa madaia kuwa ni handsome pasipo kuhoji uwezo wake.Ni katika mtizamo huohuo, CCJ inaweza kupata umaarufu kutokana na u-"kipya kinyemi" wake sambamba na majina yatakayotengeneza safu za chama hicho. As before, uwezo na commitment za viongozi zitakuwa overshadowed na haiba za viongozi husika na hivyo kurejesha kitu kilekile kinachotusumbua na CCM ya sasa.
As I said before, I might be wrong lakini....