USHAURI KWA CHAMA CHA JAMII (CCJ)
HODI:
Mniwie radhi, naingia pasi hodi ya hishma maana nimesikia Tabibu yule ajaye anatembelea leo maskani haya.
Nimekuwa nasumbuliwa na radhi la kujitakia linalotibika tangu 2007, natamani hata nishike tu upinde wa kanzu ya Tabibu -CCJ. Nimenyanyasika, nimehuzunika, nimeahibishwa kwa muda mrefu nikatamani kumwona atakayeniokoa kutoka katika hili gonjwa ili nirejee siha yangu.
Jamani kwa wale tunaoamini kuwa ujio wa CCJ utaleta matumaini mapya na ukombozi wa kweli basi tunaweza kutoa ushauri uliokwenda shule nini kifanyike kimkakati ili
tuone mabadiliko ya kweli ya kumkomboa mtanzania.
MATUMAINI:
Niwatoe wasiwasi watu wanaofikiri kuwa pengine msajiri hawezi kutoa usajiri kamili au sijui CCM kamwe haiwezi kuondoka madarakani au sijui watu hawawezi kumeguka mpaka wapate pension au sijui CCM ikisigana basi kutakuwa na mtafaruku nchini na kuhatarisha amani.
Kinyume cha hayo yote yanawezekana na nchi yetu itapiga hatua kubwa kimaendeleo kiuchumi na kijamii!
Nguvu na Amani ya Serikali duniani, viko mikononi mwa JAMII (WANANCHI) period!
Si msajiri, wala Kamati Kuu ya CCM, wala fedha za Pension. Hata UWT, Majeshi yote, Mahakama na Bunge ni vyombo tu vinavyotekeleza matakwa ya JAMII. Ukiona vyombo hivyo vinaungana na kundi dogo kunyanyasa JAMII ujue kuwa JAMII hawajavinyesha waziwazi msimamo wao period!
Chukua sekunde kufikiri mifano miwili ya karibu kabisa na pengine katika mazingira yanayoshabihiana zaidi kijiographia na kijamii.
Ni nani hapa kwetu tunaweza kumlinganisha ubabe wake na ulivyokuwa wa mwanasiasa mzamivu mzee jirani yetu Daniel Toroitich Arap Moi (NYAYO). Je unaweza kulinganisha ukubwa na athari za ubadhilifu wowote wa hapa na na skandali zilizomuhusisha NYAYO na maswahiba wake kama vile Goldenberg scandal ambayo imeligharimu Taifa la Kenya zaidi ya 10% ya GDP yao na madudu mengi yasiyoorodhesheka hasi jamii ya kimataifa kuwapiga stop kupata visa na kusafiri kwenda mfano Uk. Mbona hayo ya BOT ni cha mtoto?
Je ni akina nani kwetu unaweza kuwalinganisha na matajiri kufuru na wenye mitandao ya chuma kama akina Ali Nasir, Kamlesh Pattin, Nic Biwott, waliokuwa tayari kufanya lolote kuziba kelele ya chura yeyote. Mbona hizo shule za akina Mh. Mkono sijui Chief Ihunyo ni Servant Quarters za ma-Sekondari, ma-Vyuo ya ufundi (Polytechnic), ma-Hospitali, Vituo vya Afya vingi sana alivyojenga Biwott na wa namna yake?
Mbona utajiri wa Rostam ni sawa na stock tu katika mizania ya hesabu za watu kama akina Sir, Charles Njonjo? Leave alone akina Kamlesh Pattin nk.
Watu wanalia na vimajengo sijui huko Pwani n.k hivi nani amefika katika kijiji cha Moi huko Kabarak akashuhudia matusi. Ninyi mnalia na wanaojengewa swimming pools, watu huko walikuwa waona kawaida mtu anajengewa kiwanja cha ndege katika makao yake si ya Serikali!?
Ni wapi hapa kwetu kuna suruba za kubinywa sawasawa kwa stahili za tocha za Nairobi Nyayo House na Nyati House? Pamoja na hayo yote mzee NYAYO aliponyanyua rungu lake tu juu katika halaiki, watu walikenua meno NYAYO! huku waki-bleed internally!
Eti mnaogopa kuanzisha Chama kwamba mtanyimwa pensheni? Enzi za Moi kunyanyua tu vidole viwili (alama ya upinzani) ilikuwa unasema kuwa unakubali kuurekebisha uumbaji wa Mola kwa kutoa sadaka vodole hivyo vikatwe bila dawa ya ganzi. Eti tunapigia kelele Kijana wake kuwa UVCCM na sijui mwingine Chipukizi mbona hizo ni chekechea za siasa? Je hamjui kuwa Watoto wa Moi walifanywa kuwa Wabunge tena wenye sauti na wafanyabiashara maarufu sana?
Swali sasa; pamoja na mtandao mkali na rungu la dora na fedha leo yuko wapi Kenya? Amebaki kuwa mzee wa chama cha upinzani siyo chama tawala! Yaani hata wakimbiaji wa Marathoni toka Kenya wanaweza kuwa nacoverage kubwa katika vyombo vya habari kuliko huyo mzee ambaye ilikuwa hakuna habari bila kuanza na 'Mtukufu..
Au mkitaka mfano zaidi basi nipeni ulinganifu wa yeyoye hapa na ngunguri ya IDD Amin Dadaa
. Je umaarufu na ubabe wake uliishia wapi; mbona hata mazishi ya kijana mwehu yeyote maskini wa kutupwa yanaheshimiwa na kukumbukwa kuliko yalivyokuwa ya huyu Nduli?
Ninacho jaribu kusema si kudharau mateso tunayopata au uongozi mbovu uliopo bali nasema pamoja na kuwepo MTANDAO tunaodhani kuwa una nguvu au UTABIRI FEKI wa kutishia nyau wa mzee YAHYA, JAMII tumeamua basi inatosha hao watabaki historia tu!
USHAURI:
Popote tulipo nawaita wale wote wanaojua kuwa wanasifa za uongozi bora na wasio na mawaa isipokuwa ya kupakaziwa kisiasa, kuhama na kujiunga na CCJ bila kusita. Msiogope chochote, mtakumbukwa katika kuleta mabadiliko chanya makubwa nchini mwetu kwa vizazi na vizazi.
Bila hofu nawaita wafuatao wainuke sasa na kutangaza waziwazi kuunga mkono CCJ na kutoka waliko ili kuleta ushindi.
Hawa ni waheshimiwa, S.Sita, Prof. Mwakyembe, Prof.Mwandosya, Dr. Silaa, Prof. Beregu, Magufuri,
Wengine ni Dr.Salim H. Salim, Prof. Lipumba, Lwakatare (Ex MP),Waryoba, Mama Mpiganaji (sote tunamfahamu), Dr. Shayo (Diaspora), Sanctus-Rais TPN, Kawawa (MP), Makongoro Nyerere, Dr. Chinuno (Ex DC), present RC Morogoro na timu yao ya wanahabari ikiwa na Jerry Muro, Michuzi, Kubenea na Mwanakijiji kama PR Officer.
Mkijitokeza tu tosha tutajiunga na chama mpaka mseme basi. Jamii ya Watanzania sasa imetamka kuwa imetosha na tunasema hatutalala hata kama ni kwa kuandamana kila kukicha mpaka hiki chama kisajiriwe kwa ukamilifu maana masharti yote yametimizwa.
Ni kutoka katika hao sita wa mwanzo hapo juu, mchakato mkali utafanyika kwa wazi kubakiza watu watatu tu na kupigiwa kura ya maoni nani agombee dhidi ya mtabiriwa wa mzee Yahya.
Wengine nawakaribisha pia kuchangia maoni yenu maana haya ni yangu.
Ni rahisi sana kumpata rais mwingine Tanzania 2010, kuliko mtu kufa kwa utabiri wa yahya!
Mwanachama wa CCJ