Tanzania hatuelewi tofauti ya ajari na crush nyingi ni crush na si ajari
ajari hutokea pale ambapo dereva nina maana dereva aliyesomea udereva na sio kuchukua gari nyumbani na kuliendesha amechukua tahadhali zoote za barabarani na kufuata sheria lkn bado ikatokea hiyo senerio hii ni ajari.
Tofauti na hayo itakuwa crush
Angalia #12 hapo juu.Imekuwaje wakapanda gari moja? Hivi ndipo tulipofikia?
Kiukweli hata mimi huwa nakimbia sana na gari ila naangalia barabara na gari ninayoendesha.We unaweza kuendesha mdogo mdogo?
Niseme ukweli mi siwezi!
CHAL/TR/AR/11/2018 ILANI YA KWANZA:KOSA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO,MAJERUHI NA UHALIBIFU WA MAGARI HAYO: Mnamo tarehe 21/05/2018 majira ya saa 15:30hrs huko maeneo ya kijiji cha Msoga-chalinze ,barabara ya Msoga/Msolwa wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani, gari no STK.5923 aina TOYOTA LANDCRUISER mali ya Wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji ikiendeshwa na dereva aitwae PRISCUS s/o PETER,23yrs,mchaga,mkristo,mkazi wa Dsm, aligongana na gari no. T. 620AQV/ T.407DBY aina ya SCANIA ikiendeshwa na dereva asiyefahamika jina, jinsia ya kiume kwani alitoroka mara tu baada ya ajali
na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni MARTIN s/o LAURENCE@ MASALU,39yrs,msukuma,manajor wa kanda,mkazi wa Dsm na ZACHARIA s/o NALIGIA@ KINGU,49yrs,mnyiramba,mkazi wa Dsm
Poleni sana TIC na familia za Marehemu.Kuna taarifa zinasema waliofariki ni watatu.Kuna jina jingine siwezi kulitaja hapa wanadai naye kafariki (nimeambiwa na mtu wa karibu na TIC).Kuna haja ya kurudi kwenye mfumo wa zamani wa UMRI wa kazi ya udereva.
Upo sawa. Spidi yote hiyo kuwahi vikao Dodoma. Pengine ni vyema ofisi na watendaji wote Wakuu kuhamishiwa huko Dodoma na hivyo kupunguza safari hizi za mwendokasi za kuwahi kufika huko na pengine hata usifike kama ilivyotokea kwa hawa wenzetu. RIP.Gari la serikali mwendo wa serikali moto bati likitokea la kutokea eti wanasema AJALI HAINA KINGA nyoooo Angeendesha spidi ya 80 yote haya yasingetokea. TUSIMLAUMU SHETANI WAKATI UJINGA TWAFANYA SIE.......
Ajari - AjaliTanzania hatuelewi tofauti ya ajari na crush nyingi ni crush na si ajari
ajari hutokea pale ambapo dereva nina maana dereva aliyesomea udereva na sio kuchukua gari nyumbani na kuliendesha amechukua tahadhali zoote za barabarani na kufuata sheria lkn bado ikatokea hiyo senerio hii ni ajari.
Tofauti na hayo itakuwa crush
Pole sanaMartin Masalu.... My brother, Schoolmate mwana IPYA mwenzangu. Safari yako umeimaliza. Huu ni mshtuko mkubwa sana. Pole kwa wafiwa.
Heri wafao katika Kristo
NenoKwakweli nimeshitushwa na umri wa huyo Dereva, miaka 23 hata kama alipata leseni na miaka 16 bado ana uzoefu mdogo sana kuendesha viongozi. Atleast watu wakuanzia 35 to 45 wanafaa hizo kazi. Kwanza kichwa kimetulia show za kijinga hakuna, unampa miaka 23 VX V8 kamuaga demu wake na masela kuwa nipeni masaa matano nitakuwa Dodoma.
Dah walale kwa amani. Ila hizi gari nazo zinajifanyaga zenyewe ndio king of Roads, kwenye 50 kph wao wapo 170kph, wanaona baby walker kama kobe wana overtake gari hadi nane, wataacha kuua kweli? Serikali inapaswa kuliangalia hili juzi tu wabunge wa Zanzibar wamenusurika.
kweli kabisaMabosi 3 gari 1 vyuma vyuma vyuma ndio chanzo
Remembering jk
Hapa enzi za jk ingekuwa mabosi 3 gari 3 marehemu 1