Tatizo unakuta watu wote wako dar wanafanya safari kwenda kufanya kikao dodoma ili kuwafurahisha walevi wa udodoma, hizi ajali zitakuwa nyingi tu kwa ujinga huuView attachment 783211 View attachment 783214 View attachment 783211 View attachment 783214
Habari za usiku wadau kuna ajali mbaya iliyotokea leo usiku maeneo ya Chalinze na kugharimu maisha ya Mabosi watatu wa TANZANIA INVESTMENT CENTRE.
Mabosi hao walikuwa wanaelekea Dodoma kwenye mkutano/Kikao muhimu kilichokua kifanyike Kesho Jijini Dodoma.
Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).
Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus.
Mwenyezi Mungu aziweke roho za Marehemu mahali pema peponi na awaponye majeruhi wa ajali hii mbaya.