Chalinze: Mabosi watatu wa Tanzania Investment Centre, wafariki ajalini

DdyMwjkUwAAYNXU.jpg


Mabaki ya gari lenye namba za usajili STK 5923 ambalo lilipata ajali kwa kugongana na Lorry mkoa wa Pwani kijiji cha Msoga na kusababisa vifo vya maofisa watatu wa Serikali ya Tanzania Jumatatu jioni wakielekea jiji la Dodoma.

Maofisa wa Serikali waliofariki ni Wakurugenzi wawili na Meneja mmoja wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) na pia kusababisha majeruhi wawili akiwemo dereva wa gari hilo dogo.

Taarifa hii imethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Jonathan Warioba.
 
Kila nafsi itaonja mauti.
Safari Njema huko mnakokwenda.

Ugomvi wa mungu na shetani ndo sababu ya yote haya. Hawataki kukaa kumaliza mabifu yao binadamu tutuliee.
 
ukipata habari ya siro . BAshite " kupata ajali itakayopelekea kifo chao... usisite kutuletea pia Mkuu""
 
Nway,cjui chanzo cha ajali, ila nahisi mwendokasi utakuwa unahusika!Hawa jamaa wanaoendesha hizi LandCruza zenye namba STK, STL, SU, SM, DFP na nyingine za Serikali lakini zina namba za kiraia, aisee hawa jamaa wanakimbia sana bila kujali hali ya barabara zetu na ubora wa matairi yao!
 
Shida ya hizi gari za japani siku hizi wanaweka monster engine kwenye kitchen foil ndio maana mzinga kidogo tu mnajikuta mko nje.
 
Hii Ajali ilitokea bado mchana Around 12 jioni no giza Ila haya magari madereva wao wanatakiwa kuwa monitored
Jana nimeskia kwenye taarifa ya habar kuwa chanzo ni uzembe wa dereva wa gari la serikali.Uzembe huo ulipelekea hilo gari lihamie upande wa pili na kugongana na Lori
 
Kwakweli nimeshitushwa na umri wa huyo Dereva, miaka 23 hata kama alipata leseni na miaka 16 bado ana uzoefu mdogo sana kuendesha viongozi. Atleast watu wakuanzia 35 to 45 wanafaa hizo kazi. Kwanza kichwa kimetulia show za kijinga hakuna, unampa miaka 23 VX V8 kamuaga demu wake na masela kuwa nipeni masaa matano nitakuwa Dodoma.

Dah walale kwa amani. Ila hizi gari nazo zinajifanyaga zenyewe ndio king of Roads, kwenye 50 kph wao wapo 170kph, wanaona baby walker kama kobe wana overtake gari hadi nane, wataacha kuua kweli? Serikali inapaswa kuliangalia hili juzi tu wabunge wa Zanzibar wamenusurika.

...Miaka 23!... Atakuwa pia hana majukumu yoyote ya kimaisha ambayo yangemfanya aendeshe kwa Tadhari, akiwafikiria aliwaacha nyuma kama mke na watoto! Dereva kijana asiyekuwa na majukumu kama haya, atachukulia life for granted na hawezi kuwa muangalifu hata kidogo.......lingine, ambalo kuna mkuu ameliulizia hapo na hakuna jibu la uhakika ambalo limeishawekwa hapa...Ilikuwaje Mabosi wanne wakabanana na dereva wao kwenye V8 moja?? Hali imekuwa ngumu kiasi hiki???
 
Kuna habari kuwa mtumishi mwingine wa Serikali amefariki dunia katika ajali usiku wa kuamkia leo wakati gari lao limepata ajali wakitokea Tabora kwenye Dodoma kwenye mkutano. Ajali imetokea eneo la Bahi. RIP

Nadhani ifike wakati sasa serikali iweke sera zitakazozuia magari ya serikali kusafiri usiku. Ni kwa nini mashirika mengi binafsi yameweza kumudu kuweka sera za kuzuia magari kutembea baada ya zaa 12 lakini serikali haioni umuhimu? Ajali hizi zinapoteza wataalam muhimu kwa taifa letu lakini pia zinapoteza rasilimali za taifa. Viongozi mnaohusika okoeni maisha ya watumishi wa serikali, safari za usiku zinatokana na uzembe unaosababisha poor planning, sio kwamba watu hawa wana haraka
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom