Chalamila alipotoshwa, Mhandisi Gabriel usikubali

Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila alipotoshwa na yeye akapotosha umma, wewe usirudie kosa hilo. Tafuta chapisho langu la June 9 lenye kichwa cha habari "RC Chalamila-Mwanza amepotosha au amepotoshwa!?", litakusaidia. Ukifika ofsini irudie taarifa ya ziara ya Rais Mkoani Mwanza. Itangazie Dunia, pamoja na mambo mengine Rais atatembelea na kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery) kinachomilikiwa kwa ubia baina ya kampuni tatu, katika hizo Kampuni ya STAMICO inaiwakilisha Serikali ya Tanzania kwa asilimia 25.

Taarifa ya Chalamila iliiondoa Serikali ya Tanzania katika umiliki huo, akaifanya kampuni ya Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa Kampuni binafsi (Sekta binafsi). Hili ni kosa, zilikua dalili za kuiba hisa za (STAMICO) Serikali kama ilivyofanyika miaka ya nyuma kwenye Kampuni ya Celtel. Kama sio JPM kuzirudisha ndio tulikua tumeliwa hivyo hadi sasa. Hata nilipomwandikia hapa kumuomba Chalamila abadilishe statement yake aombe radhi, hakunisikiliza.

Mhandisi Gabriel, irudie taarifa hiyo. Iweke Serikali (STAMICO) katika position yake, Rais wa nchi hawezi kufungua kiwanda kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali bila Serikali kutajwa. Haiwezekani! Usiwasikilize wanaosema hisa zetu ni kidogo (25%) hivyo hazina uamuzi katika Kampuni kwa hivyo kutozihesabu ni haki.

Hawa hawajui lolote kuhusu aina za umiliki wa biashara, wapuuze. Ingalikua wenye hisa kidogo hawatambulishwi katika umiliki, sisi tusingalitambulishwa katika umiliki wa kampuni ya kusafirisha mafuta ya EACOP ambapo tuna hisa 15% sawa na Uganda. Itambulishe Serikali katika umiliki wa MPMR utakuja kunishukuru baadae.

Usiwasikilize wenye kusema kuwa mabango ndio yamemuondoa Chalamila Mwanza. Hakuna Rais asiyependa Mabango kwa sababu ndio mawasiliano ya haraka kutoka chini kwenda juu. Mabango ndiyo yenye kumfahamisha Rais uwajibikaji wa watendaji wake, mabango yangalikua sababu Chalamila angaliondolewa baada ya mabango kusomwa.

Mabango hayaondolewi kwa kupigwa marufuku bali kutatua changamoto za watu. Kauli ya Chalamila kuhusu mabango ilikua ni ya uwajibikaji kwake na wenzake, sio kosa. Rais mwenyewe alisema mabango yasizuiliwe, kwa vyovyote vile hilo haliwezi kuwa kosa la kumuondoa Mkuu wa Mkoa. Nisikilize mimi, irudishe nafasi ya Serikali katika umiliki wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu halafu usisahau kuwa Katibu Tawala uliyenaye hapo ametoka Ikulu.

Utanikumbuka baadaye!

MenukaJr,

Da'slama-Tanzania.
Chalamila hana uwezo wa kuongoza hata mtaa. Yule uwezo wake ni wa vituko na ukanjanja. Akajiunge na "ze comedy".
 
Andiko halina mantiki.
Kwani Mkuu wa Mkoa ndio anahisa katika hicho kiwanda au Treasury Secretary wa Hazina?
Uliyoyaandika hayana msingi kwani Serikali haifanyi kazi kwa matamko yasiyoendana na uhalisia wakile kilicho katika umiliki wa serikali.
Na serikali haiwezi kuondolewa umiliki au hisa zake kwa tamko la Mkuu wa Mkoa.

View attachment 1815145
Mkuu wa Mkoa Chaamila kakosa adabu PERIOD.
Kwa kuhamasisha mabango ya matusi kamkosea sana Mama Samia na kutoheshimu madraka na heshima ya Mkuu wa Nchi.
😃😃😃 Alitumia neno TUSI sio matusi
 
Tiss ya retired kjkkjkjk bado iko kazn,chalamila alikuwa anawindwa muda tu,so wali plan wapi wakamtimulie ,so mwanza ilikuwa ndo targeted point ,ya ku mnasa chalamila.sema naye alijisahau kuwa anawindwa . Who is the next,
 
Back
Top Bottom