Chakula cha mama Mdigo Ubungo Kibo

Chakula cha mama Mdigo Ubungo Kibo

Hivi vitu sio vya kupuuza kule mwananyamala kuna baba mmoja alikuwa anauza lungs za ng'ombe (mapupu) bandama figo nk nk kama soup ya jioni.....huwezi amini mazingira yalikuwa chini ya mti kuna gogo lkn ukifika pale kuna foleni unapewa kibakuli cha plastic kavu then unapanga foleni ya kupakuliwa mapupu wazee wa posta walikuwa lazima wapaki magari pale wapate mapupu then waendelee na hamsini zao
Mapupu bandama matamu bwana sema inabidi uwe na maji pembeni ,kipindi na hustle na elimu nilikula sana supu ya mapupu/bandama uswahilini

Sio uchawi ufundi tu wa mpikaji
 
Hili eneo kwasasa sio maarufu kama miaka ile ya 80- 90... Hapa ilikuwa ndio kama kituo kidogo cha abiria wa mikoani... Wale wauza mikate wa stendi ya mkoa zamani walikuwa wanauzia pale kibo... Ilikuwa ni lazima mabus na hata magari makubwa yasimame kwa ajili ya kununua mikate
Upande wa pili wa kituo kwa juu kidogo kulikuwa na banda maarufu sana la mama ntilie... Akijulikana kama mama Mdigo... Huyu mama alikuwa hakai mbali na hapo... Alikuwa anakaa pale msikiti wa Kibo kwa bondeni kidogo
Wajihi wa huyu mama ulikuwa wa aina yake.. Mrefu mnene kiasi mweupee, kisha mashaulah akajaaliwa nyonga na mguu... Mama Mdigo kwenye banda lake alikuwa anasaidwa na mabinti zake wawili, Mishi na Ashura.. Hawa ilikuwa ni C&P toka kwa mama yao kuhusiana na swala zima la wajihi na maumbile (shape) kiuno nyonga ya nyigu nakazalika mbili... Alikuwepo pia binti mwingine wa kazi.. Binti wa kizaramo
Banda la mama Mdigo lilikuwa linafurika kuanzia asubuhi kwenye kifungua kinywa mpaka mchana lunch time.. Jioni alikuwa hapiki.. Madereva wa mikoani walikuwa wanapaki ili wale kwa mama Mdigo kabla ya kuendelea na safari... Watu walipasifia na kupapenda sana kwa mama Mdigo kutokana na chakula chake kitamu halafu bei poa
Menu yake ilikuwa wali wa nazi, samaki sangara au nyama vilivyoungwa na nazi pia.. Mboga ya majani na maharagwe ya nazi.. Yalikuwa matamu mno... Utamu mpaka utosini... Ladha mpaka kwenye kope...!!! Ugali wa kukoboa, usafi wa vyombo na banda bila kusahau uchangamfu wa mama na mabinti zake... Menu yote hiyo ilikuwa shilingi za kitanzania 300 ugali na 350 wali na mboga yoyote kati ya nyama ama samaki... Maharagwe ilikuwa ni must iwe umekula ubwabwa au iwe umekula ugali
Nikiwa naishi geto mtaa wa Rombo kama unaenda bondeni kwa Doctor Mgaya enzi hizo... Nikajikuta nakuwa mteja mkubwa wa chakula cha mama Mdigo... Nilikuwa mteja mzuri kiasi kwamba ilifika mahali nikawa nalipa kwa wiki.... Na ikafika mahali hata weekend nikienda kuwatembelea ndugu labda niende baada ya lunch lakini nikienda kabla ukikaribia muda wa chakula nitatoa visingizio nisile ili nikale kwa mama Mdigo
Baada ya mwaka nilihamia Mtoni kwa Aziz Ally karibu na uwanja wa Sifa... Lakini huwezi kuamini ilikuwa siwezi kumaliza wiki lazima nitoke Mtoni kwa Aziz Ally mpaka Ubungo kibo kisa tu kufuata chakula cha mama Mdigo... Yani kile chakula kilikuwa na mvuto wa ajabu.. Cha kushangaza tu ni kwamba kilikuwa hakinenepeshi

Miaka ile ya 93/94 ndio tulianza kuwa na vituo vya luninga, wakati huo vikiwa ni DTV na CTN... na wamiliki wa tv walikuwa wachache mno.... Ni kipindi hicho pia ishu za kutolewa uchawi na chumaulete zilikuwa maarufu sana
Jioni moja tukiwa tumekusanyika bar moja inaitwa Zebra kwa mzee Mushi tunaangalia luninga... Bar yake pekee maeneo hayo ndio ilikuwa na tv.. Mara kupitia DTV habari namuona mama Mdigo eti katolewa uchawi.. Na ya kwamba alikuwa kazindika madawa ya mvuto kwenye banda lake (matunguli yakaoneshwa) halafu alikuwa anatumia mkono wa binadamu kama mwiko wake (tukaoneshwa mwiko wa kawaida) kubwa kuliko yote ni eti maharagwe aliyokuwa anatulisha hayakuwa maharagwe halisi bali mavi ya mbuzi... Mama Mdigo alikuwa na mbuzi wengi sana pale kibo nyumbani kwake
Huu ulikuwa ndio mwisho wa mama Mdigo na mabinti zake wawili.... Miezi michache baadae pale kwenye banda lake palivunjwa kupisha upanuzi wa barabara

Baada ya tukio lile nikaamua rasmi sasa nianze kuwachunguza mama ntilie.... Nikagundua wanasingiziwa mengi Lakini pia mengi yapo yenye ukweli
1. Wengi hawana elimu hivyo kwao suala la mvuto kibiashara sio usafi na huduma bora bali ni kutafuta mvuto kwa waganga wa kienyeji
2. Wengi hawajiamini hivyo kutafuta kinga kwa waganga ili biashara itoke lakini pia wasirogwe na wenzao
3. Wengi huogopa chuma ulete na kukopwa.. Hivyo hutumia tiba mbadala kujikinga na hizo hali
4. Wengi hupenda kupika kidogo lakini auze sana na faida iwe hata mara tatu.. Kumbukeni wali au ugali wa hamira.. Sasa hii ni cha mtoto

Wanafanyaje sasa
-kwenye mvuto ndio kama hivyo kupikia maji liyoogea
-kuweka vipande vya nyama sehemu za siri kwa muda kisha kuchanganya na vingine wakati wa kupika
-kuchanganya mboga na vitu kama mavi ya mbuzi nk
-kupikia wateja nyama tofauti na ya ng'ombe mbuzi kuku nk
Kwenye kinga
Kutumia viungo vya binadamu kupikia
Kuchanganya chakula na kitu kama yai viza nk
Kuchanganya kwenye chakula madawa yasiyoeleweka yametengezwa na nini nknk

Utagunduaje kama huyu mama ntilie sie
Unaona kabisa chakula chake ni cha kawaida kabisa lakini kinagombewa
Unaona kabisa banda lake halina hadhi na huduma za usafi haziridhishi Lakini utakuta watu wamepiga foleni
Utakuja hata siku moja sio yeye, familia yake au watu wake wa karibu wanakula hicho chakula... Wapishi wa chapati na vitumbua wana hizi sana

Mama ntilie asiyethubutu kula chakula chake hata ukimpa ofa jitenge naye ila yule anayejumuika kula na hata na wafanyakazi wake huyo si mbaya
Mpaka leo hii sijui ukweli kuhusu mama Mdigo na chakula chake ila tu kilikuwa na jambo la ziada.. Ni lipi? siwezi jua......
.Natoka Chukwan naenda Darajan( 10km) kufuata chakula mbaya zaidi kuna wengine wanaotoka mbali sio peke yangu.......Wakat mwingine huwa nahisi huyu mama sio ila nashangaa ndio naendelea tu.
 
.Natoka Chukwan naenda Darajan( 10km) kufuata chakula mbaya zaidi kuna wengine wanaotoka mbali sio peke yangu.......Wakat mwingine huwa nahisi huyu mama sio ila nashangaa ndio naendelea tu.
Mmh nilishafika Chukwani mara nyingi tuu ni nje ya mji si kule kwenye hifadhi ya kima wekundu?
 
nimesoma huu uzi nikamkumbuka jamaa mmoja anapika chapati maeneo ya sinza kwa remmy pale,mchafuuuuu ila chapati zake na maharagwe lazima usubiri kwenye foleni kupata!, sijui lakini kama yaliyomo yanafanana na bibi mdigo,bado kuna vitumbua vya bibi wa kwa mwinyi..
.....
 
Mkuu Mshanajr Kuna zile story kwamba wengine wanapika na kuuza wakiwa uchi Ila eti sisi wateja hatuoni eti tunaona wamevaa lakini wako uchi.sijui ni kweli haya hutokea au nayo ni simulizi za kweli?!
 
Mkuu Mshanajr Kuna zile story kwamba wengine wanapika na kuuza wakiwa uchi Ila eti sisi wateja hatuoni eti tunaona wamevaa lakini wako uchi.sijui ni kweli haya hutokea au nayo ni simulizi za kweli?!
Ni kweli kabisa japo ni ngumu kuthibitisha halafu kila mmoja anategemea alienda kwa mganga gani na akachagua aina gani ya mvuto
 
Ni kweli kabisa japo ni ngumu kuthibitisha halafu kila mmoja anategemea alienda kwa mganga gani na akachagua aina gani ya mvuto
Hahaha pale muhimbili enzi hizo tulikuwa tunaambiwa kuna mamantilie wako uchi, lakini sisi tunaona wamevaa hahaha story zingine noma sana.
Kuwa uchi si bora chuma ulete mkuu?!
 
Mkuu,nilianza kula migahawani nikiwa na umri mdogo sana mpaka hiv sasa nimekuwa Mzee...huwa sipend kuchunguza vyakula vya kwenye jumuia Kwa kuwa najua nitaelezwa mengi sana!
 
Hahaha pale muhimbili enzi hizo tulikuwa tunaambiwa kuna mamantilie wako uchi, lakini sisi tunaona wamevaa hahaha story zingine noma sana.
Kuwa uchi si bora chuma ulete mkuu?!
Hapana hakuna chenye afadhali hebu fikiri uchi ulivyo na sura mbaya halafu mtu akuhudumie akiwa mtupu.... Unaambiwa dalili zao utazijua ukishaaza kula atakubong'okea kwa pozi la kuosha vyombo.. Kumbe yuko uchi king'ora chote kinapiga miluzi... Si unajua akiinama chote kinarudi nyuma?
 
Hapana hakuna chenye afadhali hebu fikiri uchi ulivyo na sura mbaya halafu mtu akuhudumie akiwa mtupu.... Unaambiwa dalili zao utazijua ukishaaza kula atakubong'okea kwa pozi la kuosha vyombo.. Kumbe yuko uchi king'ora chote kinapiga miluzi... Si unajua akiinama chote kinarudi nyuma?
Hahaha we chizi sana Mshana, nani alikwambia uchi ni mbaya?! Hii miluzi ya kimya kimya au unaisikia?! Hiyo miluzi ndio mavumba yenyewe au kule kugonoka ndio msosi unanoga?!
Hahaha hizi story unaweza sababisha tukakosa wajasiliamali bure, nasi mjini hawa ndio wanatulisha.
 
Back
Top Bottom