Chahali na Uenyekiti wa Mbowe CHADEMA

Chahali na Uenyekiti wa Mbowe CHADEMA

Kama hoja ni ukomo kivp nyerere asitajwe wakati alikaa kwenye uenyekiti wa chama zaidi ya miaka 25??? Ila mbowe hajafika hata nusu eti hakuna demokrasia

Ccm mnafurahisha
Mkuu Zitto, enzi zile kumbuka zilikuwa na enzi za chama kimoja na kitu kinachoitwa demokrasia hakikuwepo, hivyo majira yamebadilika.
 
Billicanas hajaporwa ni kujigeuzia mali ya umma kuwa ya kwake kwa kutegemea huruma za wananchi! Eti Mwenyekiti afu hutaki lipa kodi!
Suala la kujichukulia maamuzi ya kulima kwenye catchment area siliungi mkono hata kidogo.
Suala la muundo wa upatikanaji kiongozi lisikupe shaka ni desturi ya chama kupokezana vijiti kila ufikapo ukomo wa uongozi na inafahamika hivyo na iko wazi katika katiba ya chama!

HOJA: Niambie uongozi wa CHADEMA katika nafasi ya uenyekiti ni miaka mingapi mingapi kwa muhula mmoja?
Ni lini amewahi itisha hata uchaguzi wa uongo uongo ili mpige kura ya kuchagua au kupendekeza mwenyekiti?
NI muundo upi wa demokrasia unayoizungumzia mliyoitumia kumpitisha LOWASA kuwa mgombea wenu wa uraisi kupitia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla?
1. Hauna ukomo nafasi ya uenyekiti sababu wananchama kupitia katiba mpya walitaka hivyo na ndio demokrasia inatekelezwa

2 uchaguzi umefanyika 2004, 2009 na 2014 na alipigiwa kura nyingi na wanachama bila mgawanyiko

3. Lowassa alipitishwa kwa mashauriano na viongozi wa UKAWA maana cuf nld na nccr havikusimamisha mgombea urais hivyo basi yalifanyika maridhiano ya nani agombee na alipochukua fomu siku ya mkutano mkuu maalum wanachama wa chadema walimpigia kura ya wazi na kumuafiki bila pingamizi sasa hiyo sio demokrasia???
 
Mkuu Zitto, enzi zile kumbuka zilikuwa na enzi za chama kimoja na kitu kinachoitwa demokrasia hakikuwepo, hivyo majira yamebadilika.
Sasa kma katiba ya chadema ambayo wanachama hawakutaka ukomo wa mwenyekiti je mbowe akiitumia hayo maamuzi yao nayo sio demokrasia???

Kama wanachama kwa ''overwhelming majority'' walitaka kusiwepo ukomo je huoni anachokifanya mbowe ndio kuwasikiliza na kutimiza masharti ya demokrasia kwamba WENGI WAPEWE
 
"Kirefu cha CHADEMA ni Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo ambayo inaruhusu mwenyekiti mmoja kuwa madarakani milele? What if “uenyekiti wa milele” ni miongoni mwa vikwazo kwa maendeleo ya chama hicho?" Evarist Chahali

Asante sana kwa kuweka makala ya Evarist Chali inayoelezea kwa kina mwelekeo wa CHADEMA. Nanukuu machache, kutoka katika makala yaje kujenga hoja zangu:

Sasa bila hata kutumia jitihada kidogo tu za busara, chama kilichomwandama Lowassa kuwa ni fisadi, kwa miaka 9 mfululizo, yaani 2006 hadi 2015, kilionekana kituko kwa baadhi yetu tuliokuwa tukikiamini, kwa sababu, pamoja na mengine, isingewezekana kutumia miezi mitatu (Julai 2015 Lowassa alipojiunga na chama hicho hadi Oktoba wakati wa uchaguzi mkuu) kumsafisha vya kutosha. Lakini walifanya maamuzi ya kumsimamisha kama mgombea wao wa Urais. Hakuna shaka maamuzi hayo yatakuwa yamefanywa na mwenye chama, na siyo na wanachama.

Mwandishi anaelezea zaidi: Chadema na UKAWA kwa ujumla walikuwa na takriban mwaka mzima wa kujipanga; kuafikiana kuhusu mgombea urais kwa tiketi ya umoja huo, na kumnadi, huku wakitumia “advantage” ya “vita vya wenyewe kwa wenyewe” kati ya zaidi ya makada 40 waliokuwa wakichuana kuteuliwa na CCM. Swali kwa nini hawakufanya hivyo jibu ni lile lile mwenye chama alikuwa na maamuzi yake tayari.

Kwa kifupi tatizo la CHADEMA kama chama siasa, si la Katiba, Sera, au itikadi zake. Bila kumng'unya maneno, tatizo la CHADEMA ni kuwepo ombwe la ungozi. CHADEMA ni ya mtu mmoja ambaye ni Bw Mtei, mwanzilishi na mfadhili wake, kikisimamiwa na Mh Mbowe kama Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Kwa aina hiyo ya uongozi, CHADEMA inapoteza hadhi ya chama cha siasa. Inaongozwa kama taasisi yoyote ambayo wenye hisa ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. Hivyo basi, wanaojiita viongozi wa CHADEMA ni waajiriwa tu, ambao wanaweza kufukuzwa wakati wowote. Ushahidi ni yaliyomkuta Zitto, Mkumbo na wengineo. Pia matamshi ya Mh Mbowe kuhusu kitendo cha Lowassa kwenda Ikulu na kumsifia Magufuli, ni mwendelezo ule ule na kuwakumbusha viongozi wengine wa CHADEMA kuwa wameajiriwa, na ajira zao zinaweza kufutwa wakati wowote. Tofauti tu ni kwamba huenda Lowassa amekwisha nunua hisa za CHADEMA.

Katika mazingira ya aina hiyo, ya chama cha siasa kama taasisi, kamwe hapatakuwa na Mwenyekiti wake nje ya familia ya Bw Mtei, mwanzilishi wa chama hicho.
 
Kwa hiyo kwa kuwa Vyama vingine vimefanya makosa na nini mmehalalisha? Mbona hivyo Vyama vinapoisifia CCM nyie mnaviita vibaraka hadi mnataka kumtoa roho kipenzi cha wanamageuzi waliojaa huko eti tu kamsifia the real and only one @MagufuliJP?
Hamna anashangaa tu CCM alikuwepo nyerere alikaa miaka 25 kwenye uenyekiti baadae CUF tumeoma lipumba mwaka wa 20 sasa..... Kina cheyo mrema cjui dovutwa mwaka wa 20 sasa cha kushangaza kwa mbowe ambaye hajafika hata nusu ya miaka aliokaa nyerere eti ndio hana demokrasia sasa najiuliza hao wengine vp

Bora mngeweka list nzima ya waliokaa muda mrefu kuendana na miaka alafu nyerere awepo juu kabisa mseme hawa ndio madikteta wa tanzania sio unachagua mbowe kana kwamba yye ndio kakaa sana kuliko mbatia na lipumba au dovutwa Inashangaza
 
issu hapa ni maslahi binafsi nani anapata nini chama kina hela nyingi lakini kubwa inawezekana hakuna uwazi au majadiliano tunatumiaje hizo fedha mbaya zaidi kunauwezekano kampuni za watu zinalipwa kihalali kabisa kwa kazi walizofanya na hapa ndo wivu unapokuja.
Hizo fedha zinakaguliwa na CAG kila mwaka! Watu wangetafuta report za CAG badala ya kuongelea Uzushi na Propaganda!
 
"Kirefu cha CHADEMA ni Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo ambayo inaruhusu mwenyekiti mmoja kuwa madarakani milele? What if “uenyekiti wa milele” ni miongoni mwa vikwazo kwa maendeleo ya chama hicho?" Evarist Chahali
Labda Chahali anasahau au anajitoa ufahamu! Moja ya nguzo muhimu katika Demokrasia Ni Uwezo wa kuchagua na kuchaguliwa! Mbowe amechagulia! Waliomchagua Wana Uwezo wa kumuondoa kwa njia ileile ya kura! Kama Kuna Tatizo kwa uwepo wa Mwenyekiti Mbowe, wa Kulaumiwa Ni Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama!
 
Tatizo la kushabikia kuabudu watu badala ya kuimarisha na kujenga imani katika mfumo kutatufikisha mbali sana, maana tutabadilishia gia angani kila kukicha hatimae tutatalii dunia nzima na lengo letu la kuzurura zurura litatimia.
Nani kaabudu mtu??? Unataka asimsifie kiongozi bora zaidi wa upinzani Tanzania??? Kma ni mrithi atapatikana tu mbona nyie nyerere alikaa miaka 25 na hamkumuita dikteta?? Kma wanachama wanaona anatosha basi msiwapangie wenyewe ndio wataamua lini inatosha na watamtoa na kumuweka mwingine ila kelele zenu hazitosaidia lolote ilihali waliomchagua ni wanachadema wenyewe
 
"Kirefu cha CHADEMA ni Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo ambayo inaruhusu mwenyekiti mmoja kuwa madarakani milele? What if “uenyekiti wa milele” ni miongoni mwa vikwazo kwa maendeleo ya chama hicho?" Evarist Chahali
Kwani Mbowe kinachombakisha hapo kwenye kiti si ndio demokrasia yenyewe.

Mbowe hapo hayupo kwa kushikia watu mapanga, bali tulimrudisha hapo kwa njia ya kura ambayo wengi huamua.

Neno demokrasia wengi huamini ni kuachia tu madaraka, Mbowe anachaguliwa na wanaChadema wenye kwa mfumo wa kidemokrasia.
 
CCM tangu imezaliwa Mwenyekiti ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. hili watu hawalioni...
 
Hivi demokrasia ni ukomo wa madaraka au ni sauti ya wengi kutawala ???

Eti kwa kuwa Democrats au republicans hakuna ukomo wa muhula wa wenyeviti wao basi ndio ina maanisha hakuna demokrasia marekani?? Mbona unachekesha

Demokrasia ina misingi 11 ila sijaona wakisema UKOMO WA MADARAKA ni demokrasia zaidi Wanachosema kuwepo uchaguzi huru na haki kama watu wamekuchoka si watakukataa kwenye kura??? Sasa kivp mseme hakuna demokrasia ilihali uchaguzi ulifanyika na wanachama wakamchagua mbowe kwa kura nyingi mara 3 mfululizo

Sasa tukirudi CCM niambie ni lini wametoa fomu kwa wanachama kugombea uenyekiti wa chama au umakam wa bara na visiwani???
Misingi ya democracy ipo wazi ukomo wa madaraka, Uhuru wa kuongea, uwazi,utawala wa sheria na haki za binadamu

Usiwe funza dogo
 
Misingi ya democracy ipo wazi ukomo wa madaraka, Uhuru wa kuongea, uwazi,utawala wa sheria na haki za binadamu

Usiwe funza dogo
Misingi yote 11 naijua unaweza ntajia msingi namba ngapiu unataja ukomo wa uongozi kma ni msingi wa demokrasia?? Nachojua kuna msingi unaotaka ufuate katiba ssa kma katiba haina ukomo huoni ukiiheshimu katiba ndio msingi wa demokrasia??

Rwanda kuna ukomo ila kuna demokrasia ??? DRC congo kuna ukomo je kuna demokrasia??

Ukomo hauna maana kama huchaguliwa kwa uchaguzi wa huru na haki au kwa matakwa ya wengi hivyo ukomo uwepo au usiwepo as long as umechaguliwa kwa majority hiyo ni DEMOKRASIA ila sio eti kukiwa na ukomo ndio demokrasia

By the way katiba mpya isiyo na ukomo wa muhula wa mwenyekiti ilipitishwa na wanachadema je huoni anachofanya mbowe ni kutekeleza demokrasia yaani mawazo ya walio wengi waliopitisha katiba hiyo inayotumika sasa???

NB: badilisha avatar inanitia kichefuchefu
 
Demokrasia inataka uchaguzi sasa umefanyika na mbowe akapewa uenyekiti sasa demokrasia ipi hakuna

Unasema ukomo?? Kwa mujibu wa aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la mabadiliko ya katiba ya chadema mzee baregu alisema maoni ya wanachadema kwa mikoa yote waliopita hawakutaja ukomo wa mwenyekiti uwepo kwenye katiba mpya ya 2006 sasa kuheshimu maoni yao huoni ni demokrasia??

Katiba isiyo na ukomo wa mwenyekiti wanachama walipiga kura na kuipitisha 2006 sasa kma walikuwa wanataka kipengele hicho kiwemo si wangeikataa katiba cku ile pale diamond jubilee???

Embu msiwe na uchungu kuliko wanachama halisi wa chadema kma wao waliona inafaa wakapiga kura sasa demokrasia gani ambayo haipo wakati kma hoja ni ukomo wanachama wenyewe ndio waliamua kwa wingi wa kura???

Funny
Unakumbuka waraka wa mwigamba na hoja ya mbowe kuchomoa nyaraka kwenye katiba ya chama ,wizi wa Mali za chama hasa Yale mafuso ya majukwaa ,kujikopesha ruzuku

Tumia kichwa kufikili sio kufugia nywele
 
Kama hoja ni ukomo kivp nyerere asitajwe wakati alikaa kwenye uenyekiti wa chama zaidi ya miaka 25??? Ila mbowe hajafika hata nusu eti hakuna demokrasia

Ccm mnafurahisha
Unajua katiba ya ccm ilikuwa inasemaje kuhusu muda au na nyie bado mnatumia katiba ya mwaka 77
 
Back
Top Bottom