Mwwnyekiti wa kwanza wa Chadema ni Edwin Mtei, Mwenyekiti wa pili ni Bob Makani, Mwenyekiti wa tatu ni Freeman Mbowe na ndiye mwenyekiti mwenye mafaniko zaidi ya wote, ni kwa nini huyu anawanyima usingizi?
Mmepora Billicanas hajaunga mkono juhudi za Magufuli, mmeharibu green house yake Hai bado hataki kuunga mkono juhudi za Magufuli sasa mnaingilia hata maamuzi ya chama chake, je mmewahi kuwauliza ccm ni kwa nini haifanyi uchaguzi kupata uongozi wa ngazi ya Taifa? Au yale maigizo yanayofanyika Dodoma ya mgombea mmoja kupata 100% kwa 100% ndio uchaguzi? Ni lini ccm itajifunza kwa ANC jinsi inavyoendesha chaguzi za kweli na za wanachama kushindana kugombea uongozi?