domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,588
- 1,760
Ngonjera ndefu hamna la maana uliloandika
Sasa wanachadema wameona kusiwe na ukomo wa uenyekiti kwenye katiba yao na mbowe ametumia hiyo haki kikatiba na alipigiwa kura nyingi na wanachama ili aendelee kuwa mwenyekiti sasa nyie kelele kuwa ni dikteta zinatoka wapi ilihali sisi wanacham tumeridhika na uongozi wake
Nimeshasema kama anafuja ruzuku mbona CAG anakagua na hajawahi wapa hato chafu kwa hoja hiyo??? Nyie mnaosema anakidai chama sijui anafuja ruzuku mnatoa wapi msingi wa madai yenu
Twende mbele turudi nyuma mbowe ndio kiongozi wa upinzani imara zaidi hapa Tanzania ukitaka kujua hilo angalia CUF na ACT na NCCR zilipopata migogoro zimetikisika ila CHADEMA imevuka yote ipo imara sasa kma hamlioni hilo mnakalia propaganda hazitowasaidia chochote
Itakuchukua muda mrefu sana kama unajifunza lakini ni mwanafunzi unayeelewa taratibu. Pia unaweza usijue kitu kabisa kinachoendelea kama unaamini unajua. Muda utakuambia yatakayotokea yatadhihirisha ukweli. Kwa taarifa yako Mbowe hajawahi kufikia hata nusu ya uwezo wa Augustine Mrema akiwa mwenyekiti active katika upinzani. Bahati mbaya sana nampigia mbuzi gitaa ambaye hata hajui k uwa kuna utaratibu wa kusajili vyama vya siasa na una masharti yake sio suala la wanachama tu kujiamulia. Wanachama wapmbavu wakiamua upumbavu chama kinafutwa.
Chama ni kwa ajili ya watanzania wote si kwa ajili ya wanachama tu mtoto. Kulielewa hili kunahitaji kujielimisha sio kuamini unajua.