CHADEMA yatikisa Mwanza, Furahisha pamekucha

CHADEMA yatikisa Mwanza, Furahisha pamekucha

CDM nawakubali, ila bado hawajanifurahisha kwenye mkakati mmoja. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafanya hii nyomi inayojitokeza kwenye mikutano yetu kujiandisha kupiga kura? Hili ni jambo la muhimu sana kama tunapenda kuikomboa TZ kwenye makucha ya wanyang'anyi kama Magamba. Tuliona mwaka 1995 Mrema alikua na nyomi nyomi kwenye mikutano yake hadi akaamini anachukua nnji (siyo nchi) na kweli akachukua nnji yake akawaachia magamba nchi yao waendelea kuiba na kutufanya mazezeta wa elimu. Viongozi wetu wa CDM, anzeni kmikakati sasa ya kuutafsiri huu umati kwenye daftari la wapiga kura, hii inatakiwa iwe kauli mbiu ya kila mkutano. Vijana waelewe umuhimu wa kupiga kura na sio kushabikia tu halafu mwisho wa siku magamba wakiongeza na wanazoiba wanaibuka tena.
 
CCM endeleeni na kazi yenu ya kupiga lamri kuwa Chadema itakufa 2013.Kwa nyomi hii mtaki mnambwelambwela tu.
 
Leo naona Mtaka(Matata) meya wa CCM sijui alijificha wapi maana akiona watu walivyoitikia katika mkutano anajuta.
 
Leo naona Mataka(Matata) meya wa CCM sijui alijificha wapi maana akiona watu walivyoitikia katika mkutano anajuta.
 
Duuuh!! Imagine kama hii nyomi ndo ingekwa ichukuliwe na mabasi na malori kama wafanyavyo magamba, ni magari mangapi yangekuwepo? ingula mtaji. Lakini wote wamekuja weeeenyewe kwa miguu yao. Ndo safari ya ikulu hiyo. JK anza kufungasha.
 
Mungu lazima atakuwa upande wetu watetezi wa wanyonge na mali asili za nchi... bravo peoooooopleeeeeeza powweeeeeeeeer
 
CDM nawakubali, ila bado hawajanifurahisha kwenye mkakati mmoja. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafanya hii nyomi inayojitokeza kwenye mikutano yetu kujiandisha kupiga kura? Hili ni jambo la muhimu sana kama tunapenda kuikomboa TZ kwenye makucha ya wanyang'anyi kama Magamba. Tuliona mwaka 1995 Mrema alikua na nyomi nyomi kwenye mikutano yake hadi akaamini anachukua nnji (siyo nchi) na kweli akachukua nnji yake akawaachia magamba nchi yao waendelea kuiba na kutufanya mazezeta wa elimu. Viongozi wetu wa CDM, anzeni kmikakati sasa ya kuutafsiri huu umati kwenye daftari la wapiga kura, hii inatakiwa iwe kauli mbiu ya kila mkutano. Vijana waelewe umuhimu wa kupiga kura na sio kushabikia tu halafu mwisho wa siku magamba wakiongeza na wanazoiba wanaibuka tena.
Nadhani matokeo ya chaguzi mwanza yana majibu ya mashaka yako
 
Habari za uhakika ni kwamba mwenyekiti wa magamba mkoa amewekewa drip hosptali 1 maarufu jijini mwanza baada ya kushuhudia umati ule wa leo pale furahisha
 
Hawa jamaa hawana ustaarabu wa kujiuzulu,hata iweje nina uhakika atasema labda aliyenipa madaraka ndio aniondoe. Ikishindikana kabisa atahamishiwa wizara ya Fedha
 
Ni uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Magharibi, mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. Ni baada ya kuzindua Kanda ya Kaskazini jana Jijini Arusha leo ni Jijini Mwanza. Mkutano wa hadhara ndiyo umeanza baada ya kikao cha ndani kwa muda mfupi baada ya Mwenyekiti Mbowe kuingia jijini kutokea Kilimanjaro leo mchana.

attachment.php

M/kiti taifa (CHADEMA) akiwasili pamoja na viongozi wengine.

attachment.php

attachment.php

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutanao

attachment.php

attachment.php

Chini ni Alphonce Mawazo maarufu kama 'Kamanda Mawazo'
attachment.php

Hapa kila mtu katoa na zake mfukoni siyo malori kama kwa kina na Mwampamba Leo kama mwanza imezaliwa upya kwa sisi tuliokuwepo pale furahisha ilikuwa ni furaha kweli leo jiji la Mwanza Pia mmesahau wimbo wa leo wa wana Mwanza walikuwa wakiimba hivi "KIKWETE X1 (Wote), Bora Ukimwi (wote)" kwa kweli walikuwa wakiimba wanawake kwa wanaume ni wakati wanampeleka Mwenyekiti Taifa(Kamanda wa anga) kule hotel alipo fikia.
 
Leo majira ya saa nane na nusu adhuhuri kwenye viwanja vya wazi vya furahisha maeneo ya Kirumba kwenye mkutano wa hadhara wa kuzindua kanda ya magharibi kufutia maazimio ya kikao cha baraza kuu la CDM kutekeleza kwa vitendo sera ya majimbo kama walivyokuwa wameinadi kwenye ilani yao ya uchaguzi,kulikuwa na halaiki ya watu ambayo haijawahi kutokea waliohudhuria wakiwa na kiu ya kumsikiliza kamanda wa anga ambaye ni M/Kiti wa CDM Taifa.

Wananchi wakionyesha dhahiri kiu yao ya kumsikiliza mh.Mbowe wakazi hao wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake walikuwa wametulia tuli bila vurugu na kutoa ile dhana ya CDM ni chama cha vurugu.

Mkutano huu ulifunguliwa kwa Alfred Rwekatare kumkaribisha M/Kiti wa CDM Ilemela ambaye alimweleza M/Kiti wake wa taifa matatizo ambayo kwao wanayoyaona kama kero huku akisema wameamua kukaa kimya kwakuwa tu CDM ni chama kinachoheshimu utawala wa sheria vinginevyo wangekuwa wameshamtoa Meya wa Ilemela bwana Matata anayejinadi kama diwani wa mahakama.Baada ya nasaa zake alifungua mkutano ambao ulifuatiwa na utangulizi wa makamanda mbalimbali wakitoa salamu za chama.

Kamanda Mawazo ambaye wamekuwa mwiba mbaya kwa chama cha CCM toka alipoamua kujivua gamba aliwataka wakazi wa jiji la Mwanza kuhakikisha wanaungana na kuung'oa utawala dhalimu wa CCM,pia aliwashukuru wananchi wa Mwanza kuweza kuchangia harakati mabadiliko kwa kuweza kutoa michango yao hali na mali iliyopelekea kufanikisha malengo ya kuing'oa CCM kwa kazi kubwa ya kutoa elimu ya uraia wilayani Magu na kupelekea kupata ushindi mkubwa wa uchaguzi wa serikali ya vijiji na vitongoji kwa CDM kuibuka kidedea kiasi cha ziara ya wajumbe wa NEC ya CCM walioambatana na Mangula kuonekana kama ziara yao haikuwa na mafanikio.

Naye mkurugenzi wa mambo ya Bunge na halmashauri wa CDM bwana John Mrema aliishangaa sana serikali ya CCM na kuita maajabu inayoyafanya kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu meli inaungua ikiwa katikati ya ziwa na kusema kuelekea kifo cha CCM tutaona maajabu mengi ambayo yatatokea kama suala hilo la meli iliyosababisha waziri wa uchukuzi na naibu wake kushindwa kuzungumzia chanzo cha tatizo hilo.

Mh.Wenje akihutubia alifunguka kwa kusema,wakati mh. Mbatia anawasilisha hoja yake mitaala ya elimu yeye alipeleka schedule of amendment kwa kuongezea na kuiongezea uzito hoja ya mh.Mbatia lakini pamoja hoja zingine zilitupwa namheshimiwa Spika.Akilelezea kuhusiana na hatua za kumng'oa mkurugenzi wa jiji la Mwanza mara baada ya kupata ridhaa ya wananchi kwa kukusanya saini za wananchi,hoja hiyo ilitupiliwa mbali na Spika lakini bado anaendelea kulifuatilia ili kupata uvumbuzi ikishindikana atalirudisha kwenye mahakama ya wananchi ili wananchi watoe maamuzi.

Mweyekiti wa baraza lawadhamini wa CDM mzee Masinde aliwataka wananchi wawe watulivu kwa kila hatua na kusisitiza wasione kimya kutokana na vurugu zilizokuwa zinafanywa na waliokuwa wananchama wa CDM ambao walifukuzwa na kukimbilia,kwani kawaida mstaarabu humuacha mtu afanye vurugu zake akimaliza ndiyo hutoa maamuzi,akiwataka wananchi wasitishwe na vurugu hizo kwani CHADEMA ni chama imara na akitishwi na mtu
kitaendelea kitaendelea kuwa imara.

Mkutano huo wa hadhara ulihitimishwa kwa M/Kiti wa CDM taifa kukemea udini uliopandikizwa na CCM kwa kuona ndiyo njia bora ya kujijenga kisiasa,huku akimwambia rais Kikwete na chama chake kuwa kwa suala hili wamelikoroga ni lazima walinywe.Akizungumza kwa uchungu na hisia kali kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani aliyaita matatizo hayo ni msiba mkubwa kwa taifa,akiwataka Watanzania wadumishe mshikamano na umoja wa kitaifa mh. Mbowe alisema CDM ni chama cha Watanzania wote bila kujali itikadi zao na kusema ikitokea kiongozi wa CDM akahubiri udini na ukabila chama hakitamvumilia ikiwa pamoja na kumfukuza.

Akiinadi sera ya majimbo aliwataka wananchi wakatae ushawishi unaofanywa na serikali CCM kuwa majimbo yanawagawa Watanzania kwakuwa tu sera ya majimbo inapunguza madaraka toka serikali kuu na kuwarudishia madaraka.Mh. Mbowe aliishambulia serikali ya CCM kutokana na kutokuwa na sera elimu ambayo imepelekea Tanzania kuwa nchi ya kwanza duniani kwa mfumo mbovu duniani kutokana na kutoa kiwango kikubwa cha kufelisha ilihali waziri wa elimu akiendelea kukalia kiti hicho.

Mh. Mbowe amemtaka waziri mwenye dhamana ya elimu ajiuzuru mara moja akishindwa amempa wiki mbili vinginevyo wataandaa maandamano makubwa ya kumng'oa mh.Shukuru Kawambwa pamoja na wasaidizi.Msiba huu ambao ni janga la kitaifa si la wananchi kucheka ilihali kila mwaka zaidi ya wanafunzi laki nane wa shule za msingi wanaingia mitaani bila kuwa na uwezo wa kuajiriwa kutokana kukosa elimu,akizungumzia viwango vya ufaulu wa sekondari ameishangaa ni kwanini serikali imekaa kimya ilihali idadi ya waliofeli ni zaidi ya asilimia 90% kwa kuwa waliopata daraja la nne hawana sifa ya kuendelea na masomo.

Mwisho kamanda Mbowe alimuonya katibu wa bunge asibweteke kwa kutaka kuwanyima wananchi haki yao ya kupata habari kwa kuwaona live wawakilishi wao,ambao ndiyo waamuzi wa kuona yanayojiri huko bungeni.
 
Ni uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Magharibi, mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. Ni baada ya kuzindua Kanda ya Kaskazini jana Jijini Arusha leo ni Jijini Mwanza. Mkutano wa hadhara ndiyo umeanza baada ya kikao cha ndani kwa muda mfupi baada ya Mwenyekiti Mbowe kuingia jijini kutokea Kilimanjaro leo mchana.

attachment.php

M/kiti taifa (CHADEMA) akiwasili pamoja na viongozi wengine.

attachment.php

attachment.php

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutanao

attachment.php

attachment.php

Chini ni Alphonce Mawazo maarufu kama 'Kamanda Mawazo'
attachment.php

Wazee wa mafuso wataiga na hii!
 
CDM nawakubali, ila bado hawajanifurahisha kwenye mkakati mmoja. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafanya hii nyomi inayojitokeza kwenye mikutano yetu kujiandisha kupiga kura? Hili ni jambo la muhimu sana kama tunapenda kuikomboa TZ kwenye makucha ya wanyang'anyi kama Magamba. Tuliona mwaka 1995 Mrema alikua na nyomi nyomi kwenye mikutano yake hadi akaamini anachukua nnji (siyo nchi) na kweli akachukua nnji yake akawaachia magamba nchi yao waendelea kuiba na kutufanya mazezeta wa elimu. Viongozi wetu wa CDM, anzeni kmikakati sasa ya kuutafsiri huu umati kwenye daftari la wapiga kura, hii inatakiwa iwe kauli mbiu ya kila mkutano. Vijana waelewe umuhimu wa kupiga kura na sio kushabikia tu halafu mwisho wa siku magamba wakiongeza na wanazoiba wanaibuka tena.

Mimi hii kauli nimekuwa nikiipinga kusema ni kazi ya CDM kuwapa watu elimu juu ya umuhimu wa kupiga kura ....hii kazi ni yako wewe, mimi,na mwingine yeyote anayetamani mabadiriko na wenzako ndo kazi tunazofanya hata vyuoni na tumewapoteza na wengine kwa kufukuzwa vyuo kwa dhuruma ya kutokuwaunga mkono magamba
 
Waziri mkuu aanze,wengine wafuate kujiuzulu!Jee majimbo yatakua na maamuzi,majukumu yepi?
 
CDM nawakubali, ila bado hawajanifurahisha kwenye mkakati mmoja. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafanya hii nyomi inayojitokeza kwenye mikutano yetu kujiandisha kupiga kura? Hili ni jambo la muhimu sana kama tunapenda kuikomboa TZ kwenye makucha ya wanyang'anyi kama Magamba. Tuliona mwaka 1995 Mrema alikua na nyomi nyomi kwenye mikutano yake hadi akaamini anachukua nnji (siyo nchi) na kweli akachukua nnji yake akawaachia magamba nchi yao waendelea kuiba na kutufanya mazezeta wa elimu. Viongozi wetu wa CDM, anzeni kmikakati sasa ya kuutafsiri huu umati kwenye daftari la wapiga kura, hii inatakiwa iwe kauli mbiu ya kila mkutano. Vijana waelewe umuhimu wa kupiga kura na sio kushabikia tu halafu mwisho wa siku magamba wakiongeza na wanazoiba wanaibuka tena.

Hapo kwenye kijani ndiyo hasa maana ya kuanzisha mfumo wa Kanda. Viongozi wa kanda wana jukumu la kuhamasisha wapenzi na wanachama wasishabikie tu Chadema bali wajiandikishe na mwisho wa siku wajitokeze kupiga kura kwa Chadema
 
Majimbo yatakuwa na majukumu ya kuhakikisha madaraka yanarudi kwa wananchi,na rasilimali zao zitanufaisha kwanza ndani ya majimbo na kiasi kingine kitakwenda serikali kuu.Lakini yatafuta ukabila ambao leo ndiyo wimbo wa taifa wa CCM.Pia sera ya majimbo itainua uchumi wa maeneo mengi hapa nchini kwa kuwa kutakuwa na ushirikishwaji wa moja kwa moja juu ya rasilimali zao
 
Back
Top Bottom