CHADEMA wamkana Zitto

CHADEMA wamkana Zitto

hivi Zitto ambae ni naibu katibu mkuu wa CDM anamuomba nani hesabu za chadema? Zitto anakaa kwenye vikao vya sekretataliati ya chama na yeye ndie aliepaswa kupeleka hesabu hizo huko kunakotakiwa kama kweli hazijapelekwa ili ziweze kufanyiwa ukaguzi sasa kama alikua anajua sheria na hakuwashauri wenzake kufanya au hakuchukua jukumu yeye kama naibu katibu mkuu wa chama anatuambia sisi wengine ambao ni wananchama wa kawaida wa chadema kwamba chama hakijafanyiwa ukaguzi ili iweje? na kama kuna mtu alimzuia kutekeleza wajibu wake huo kwenye chama mbona hajawahi kuuuambia umma wa wanachadema ili tumsaidie?? suala la fedha ni nyeti na linaweza kuchafua image ya chama kwasababu ya upuuzi wa zitto na kutafuta sifa binafsi au kufanya kazi ya ccm kwa kuichafua chadema ionekane yenyewe ni kama ccm ili Watanzania wakate tamaa na waendelee kuichagua ccm inashangaza kuona hata magazeti ya mafisadi kama Rai na gazeti la uhuru la ccm yanaishambualia chadema wakati na ccm imetajwa haya yote yanafanyika kwasababu ya uhuni wa Zitto kukiweka chama chetu kwenye kapu mmoja na ccm wakati anajua kabisa kwamba chadema hesabu zake ziko kwa msajili na ametoa barua kuthibitisha hilo.Zitto anaekushauri anakupotosha sana na mwisho wake utakua kama Mrema Lyatonga.

Una unavyojichanganya kwa sababu ya chuki yako.
 
i dont trust zito kwa kweli.. honestly kama CDM hawata chukua mapema tutegemee damage kubwa sana.. unless kuwe kuna kitu kingine kimejificha..

HASA HIZI MOVEMENT ZAKE ZA ONE MAN ARMY KWA KISINGIZO CHA MASLAHI YA TAIFA VYAMA BAADAE ..
 
Huyu zito ni lazima achunguzwe kwa umakini mkubwa. Kila anapoibuka na hoja unakuta kuna swala zito wananchi wanasubiria ili kupata muafaka. Wakati huu wakati taifa zima tumeweka mawazo yetu kwenye swala la katiba mpya tunaona Zito anakuja na hoja zake mbalimbali.
  1. Mshahara wa waziri mkuu, Ikafell
  2. Mshahara wa rais, nayo ikefall
  3. Sasa ameamua kuja na hoja ya kutaka vyama vya siasa viwakilishe hesabu za matumizi yao kwenye ofisi ya CAG. Na jambo la kuuzunisha vyombo vya hapari vimekuwa washabiki bila kuchunguza kwa undani nini kinaendelea.
Hapa cha kujiuliza ni kwanini hii hoja yake ailete kipindi hiki na wakati kwa jinsi anavyodai hesabu hizo haijakaguliwa leo mwaka wa 4. Hapa kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia na kwabahati nzuri Watanzania walio wengi wameligundua.

Hiyo mishahara imefeli wapi? Kaahidi kuitaja na akatoa maelezo kuwa ishu sio mshahara ila ishu ni mishahara ikatwe kodi kama watumishi wengine. Halafu eti kisa kuna katiba ndio asizungumzie matatizo mengine yanayoathiri taifa? Acha chuki na nyuso mbili.
 
This is just silly; vyama havitakiwi kusema lolote sasa hivi. Wanaotakiwa kutoa maelezo ni CAG na Msajili. Wao ndio wanapaswa kusema kama vyama vimekidhi matakwa ya sheria au la. Ukimya wa vyombo hivi viwili ndio vitu vinavyonitibuaga mimi. Kamati ya Bunge imesema na kutoa maagizo CAG na Msajiri wanatakiwa waseme kama watakagua, wameshakagua au hawana mpango wa kukagua hivi karibuni.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, naomba nikuulize maswali machache .
Taratibu za kiuhasibu zinasemaje kuhusu umiliki wa taarifa iliyokaguliwa na iliyolipiwa;
1.Je ni mali ya mkaguzi ama aliyokaguliwa?
2.Nani anaitolea maelezo pindi shutuma kama hizi za PAC zinapotolewa?
 
Last edited by a moderator:
Nitakujibu swali No.1
Mara zote Dr.anaposafiri au kuwa nje ya Ofisi John Mnyika ndiye hua anakaimishwa, ingawa kiprotokali Zitto ndiye anayepaswa kukaimu nafasi ile Hapo usiniulize kwanini maana mi pia sijui ila kuna uzi flani hivi wa @Election Observer una kichwa habari "Ugaidi ndani ya Vyama vya siasa " unaweza kuunganisha dots

one bright guy!!!!!likes
 
Last edited by a moderator:
Chama mbali na bunge mbali.

Kama magufuli kuvunja vijiwe vya wafurukutwa wa CCM kando kando ya barabara.
 
Kuna wakati huwa nina mashaka hata na MBA ya Zitto!!

Kwangu binafsi bado haiingi akilini...otherwise Bw. komu atakuwa ameleta habari za kizushi na kizandiki!!!

ZZK anaingia kwenye mtego na mazoea ya Serikali yetu, maana Serikali ya TZ na vyombo vyote vinavyohusiana nayo, havijawahi kufanya kazi kuonyesha vi ndani ya serikali moja yenye rais mmoja!!

Any ways....ni maudhi tu kila kona.

Una uhakika Mh Zitto ana MBA?? Au unataka na wewe kujidai wamjua sanaaa ??

Kwani Masters in Economics nayo ni MBA??

Nifahamishee
 
Nape ndo alikuwa wa kwanza kutokwa mapovu... Chadema tumejibu kwa evidence sasa ni jukumu la Zitto kwenda kwa msajili kuthibitisha..

Kwa msajili kufanya nini??? Hizo taarifa zilizo kwa msajili ni barua tu na sio ripoti. Ripoti zinapelekwa na CAG. Huwezi kupeleka ripoti ya audit umejifanyia mwenyewe. Ripoti ya ukaguzi inayo kubalika ni ya CAG tu! Na CAG anasema yeye hajakagua chama hata kimoja sababu hana budget
 
Mnataka kutota kwenye mambo ya KATIBA MPYA na kutuhamishia huku. Zitto anajua anachofanya na CHADEMA wanajua nini Zitto anafanya au anataka kufanya.

Tuwaachie wenyewe watajua cha kufanya mimi na wewe ni porojo tu bora kuongelea Katiba mpya yenye maslahi yetu. Kama ni Kodi kutafunwa mbona tunaona hata huku uswahilini viongozii wanavyozitafuna bila uwoga?
 
This is just silly; vyama havitakiwi kusema lolote sasa hivi. Wanaotakiwa kutoa maelezo ni CAG na Msajili. Wao ndio wanapaswa kusema kama vyama vimekidhi matakwa ya sheria au la. Ukimya wa vyombo hivi viwili ndio vitu vinavyonitibuaga mimi. Kamati ya Bunge imesema na kutoa maagizo CAG na Msajiri wanatakiwa waseme kama watakagua, wameshakagua au hawana mpango wa kukagua hivi karibuni.

Uko sahihi mzee. Na CAG amesha sema hajakagua sababu hana budget. Kwa kutatua tatizo hili lazima bunge lipitishe budget. Hapo tunarudi tena pale pale. Bungeni ccm ina wabunge karibu 80% na ccm inatumia 80% ya ruzuku. Hao hao ccm hawajafikisha hesabu zao kwa sheria ya zamani wala mpya. Je watapitisha kweli hii budget?
The same goes for all parties maana wabunge wote walichangiwa campaign na hizo hela za ruzuku. Watakubali kukaguliwa?
 
Zitto ni kituko. mwanznoni ilitaka kumfagilia kama kikwete alivyo tukoga mwanzoni, lakini kama una upana wa kutosha wa kufikili katika kichwa chako unagundua zitto ni mtu wa aina gani! jamaa anazingua, blah blah blah
 
Tangu Zitto atake hesabu za Chadema zikaguliwe, chama chake kimemjengea uadui wa ghafla. Kwani hesabu kukaguliwa kuna ubaya gani? mnaficha nini kwenye hivyo vitabu?
 
Hiyo mishahara imefeli wapi? Kaahidi kuitaja na akatoa maelezo kuwa ishu sio mshahara ila ishu ni mishahara ikatwe kodi kama watumishi wengine. Halafu eti kisa kuna katiba ndio asizungumzie matatizo mengine yanayoathiri taifa? Acha chuki na nyuso mbili.

Mkuu Chamviga, kwanza napenda kujiweka wazi kuwa sina chuki na Mh. Zito, ila mtu alieamua kuwa mwanachama lazima awe na mitazamo inayofanana na wanachama wenzake na anapokuwa tofauti na wenzake ni lazima atiliwe shaka na watu kuwa makini na kila jambo alifanyalo na sio kuamini kiraisi kila analolisema.
N upande mwingi Mkuu Chamvinga nadhani uwezo wako wa kutambua jamboi kwa haraka ni mdogo na huwa unaongozwa na matukio. Na naomba nikuulize swali moja Je unajua majina ya watu walioficha pesa Uswiss ambao Mh. Zito aliaidi kuwataja?
 
Huyu zito ni lazima achunguzwe kwa umakini mkubwa. Kila anapoibuka na hoja unakuta kuna swala zito wananchi wanasubiria ili kupata muafaka. Wakati huu wakati taifa zima tumeweka mawazo yetu kwenye swala la katiba mpya tunaona Zito anakuja na hoja zake mbalimbali.
  1. Mshahara wa waziri mkuu, Ikafell
  2. Mshahara wa rais, nayo ikefall
  3. Sasa ameamua kuja na hoja ya kutaka vyama vya siasa viwakilishe hesabu za matumizi yao kwenye ofisi ya CAG. Na jambo la kuuzunisha vyombo vya hapari vimekuwa washabiki bila kuchunguza kwa undani nini kinaendelea.
Hapa cha kujiuliza ni kwanini hii hoja yake ailete kipindi hiki na wakati kwa jinsi anavyodai hesabu hizo haijakaguliwa leo mwaka wa 4. Hapa kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia na kwabahati nzuri Watanzania walio wengi wameligundua.
Pengine anayo tabia ya kudandia wakati mwengine visivyo muhusu, lakini hapa kuna kujikanganya na sheria/utaratibu, unatakiwa uheshimike wakati wowote. Vyama vya siasa vina taratibu zake na sheria zao za matumizi hilo linasimamiwa sijui na msajili na wakaguzi kama CAG or independent auditors to do with party finances law.

Kamati ya PAC hayo ya paragraph one haya wahusu sana wao kazi yao ni kukagua matumizi ya hela serikali inazotoa kwenye vyombo vya umma. Sasa kesho wanaweza amua embu tuangalie pahala fulani hela imetumikaje hapo ndio wanamfata mhusika as in this instance ambae sijui ni CAG or msajili bwana embu tupe ripoti ya vyama tuangalie ndio hapo labda sina au hii hapa.

Kwa hivyo alichosema Zitto CAG hana hizo ripoti walizoomba kulikoni, CAG au msajili angewepa kusingekuwa na kelele zote. Kwakuwa zinahitajika kwenye kamati kwa ukaguzi shurti wapeleke tu lakini sidhani kama kuna mtu mwenye nia mbaya unless watu hawajiamini wenyewe na wanajistukia tu (by the way thats how PAC works where i am, hawa wahuku ndio noma kila kukicha makatibu wizara kitimoto)
 
Z.Z.K V.S W.P.S ngoja nichukue pop corn zangu nisubirie hii movie.
 
Hesabu huwa zinapelekwa kwa CAG kwa barua,
na zikishakaguliwa CAG wanaandika barua
na hati ya kukaguliwa;

Watuoneshe hati za kukaguliwa kutoka kwa CAG
vinginevyo hayo wanayosema ni sawa na hadithi
njoo na uongo kolea.
 
Back
Top Bottom