CHADEMA 'walishinda' uchaguzi katika kata zote 27!

CHADEMA 'walishinda' uchaguzi katika kata zote 27!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,197
Reaction score
27,817
TATHMINI YA UCHAGUZI MDOGO KATIKA KATA 27

Matokeo ya uchaguzi katika hizi kata 27 ambapo CCM ilishinda kata 23 , CHADEMA kata 3 na NCCR kata 1, yanaonekana kuwa mazuri kwa CCM lakini ni mazuri zaidi kwa CHADEMA kwani kura walizopata si haba hasa ukizingatia kwamba kata ambazo CHADEMA wameshinda zilikuwa zinawakilishwa na CCM. Lakini pia wakazi wa maeneo mengi ambayo CHADEMA walipata kura chache wana elimu duni ya uraia na uelewa hafifu juu ya madhambi ya serikali na chama tawala dhidi ya maisha na ustawi wao kwa ujumla.

Kwa CHADEMA kupata kura nyingi kiasi hiki, ijapokuwa hawakushinda katika kata hizo, ni sawa na ushindi wa kishindo. Katika kata nyingi CCM walishinda kwa tofauti ndogo sana ya kura. Hii inaonyesha kwamba wananchi wameanza kujitambua kidogo kidogo kuhusu udhalimu wa CCM na serikali yake. Kadri muda unavyokwenda, wananchi watajitambua na hatimaye kuachana kabisa na chama tawala kwani kimeshindwa kuleta maendeleo ya maana tangu nchi hii ipate uhuru.

NGUVU YA CHADEMA
Nguvu ya CHADEMA katika Kata zote inakuwa siku hadi siku na kadri wananchi wanavyozidi kujitambua, ispokuwa wale wazee wenye mawazo ya kihafidhina na ambao wasiotaka kubadilika licha ya kwamba wanaishi maisha duni chini ya utawala dhaifu wa CCM. Lakini ni jambo la kumshukuru Mungu kwa hizi kura walizopata CHADEMA kwani uchaguzi uliopita waliambulia kura chache sana. Hivyo nawaasa makamanda wasikate tamaa bali waendelee kuchochea kuni za madadiliko hadi kieleweke. Nina imani kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakapoitishwa mwishoni mwa mwaka huu, CHADEMA watafanya vizuri kuliko sasa hivi kwani uzoefu unaonyesha kuwa kuna maendeleo ya kuridhisha katika suala zima la kuungwa mkono na watu wengi.

IDADI YA WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hapo juu, ni idadi ndogo sana ya wananchi waliojitokeza kupiga kura (25% ya wapiga kura wote waliojiandikisha kupiga kura katika Kata zote). Hizi takwimu sio nzuri hata kidogo kwa maendeleo ya demokrasia na mageuzi ya kiuchumi kwa wananchi wanaotamani kujikomboa kutoka makuchani mwa CCM. Katika vituo vyote vya kupigia kura katika Kata, asilimia kubwa ya watu waliojitokeza kupiga kura (>90%) ni wazee na vikongwe (vigagula). Vijana waliojitokeza kupiga kura ni wachache sana ukilinganisha na wazee wenye umri mkubwa (wahafidhina). Haikuweza kufahamika mara moja ni nini kilichowasibu vijana hadi wakashindwa kujitokeza kupiga kura na badala yake wakajitokeza wazee na vikongwe! Hapa ndipo CCM ilipoipigia bao CHADEMA. Kumbe inaonyesha (ijapokuwa sijalifanyia utafiti) kwamba vijana wengi waliokuwa wakijitokeza kwenye mikutano ya CHADEMA ama hawakujiandikisha kupiga kura au walikuwa wanakuja tu kuishangaa chopa!

Hiki ni kitendawili ambacho kinapaswa kuteguliwa na tume ya uchaguzi, vyama vyote vya siasa pamoja na serikali kwani haiwezekani kwamba vijana wenye nguvu na uelewa wa kisiasa washindwe kuja kupiga kura na badala yake wawaachie vigagula wahafidhina waichague CCM. Kimsingi wazee na vigagula ndio walikuwa mwarobaini wa ushindi wa CCM katika Kata hizi na katika majimbo mengi ya uchaguzi. Ifike wakati sasa vijana wanapohudhuria kwenye mikutano ya vyama waombwe kuja na kadi zao za kupigia kura na kuzionyesha kwa viongozi wao badala ya kufanya unafiki wa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya siasa halafu hawaji kupiga kura. Utaratibu huu utasaidia kuwatambua wanafiki na wasaliti wanaoonekana kushabikia upinzani wakati hawakujiandikishi kupiga kura. Huu ni unafiki na uzandiki mkubwa sana wanaouonyesha vijana tunaowategemea kuikomboa nchi hii kutoka kwenye ukoloni wa CCM. Ni jambo la kusikitisha kwamba vijana hutoka nyumbani kwao na kuvizingira vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kulinda kura wakati wao wenyewe hawajitokezi kupiga kura. Sasa kama hujapiga kura unakuja kulinda masanduku yaliyojaa kura zilizopigwa na wazee na vigagula wa CCM unategemea ushindi kwa chama chako (CHADEMA) utapatikanaje?

Vijana tuache unafiki jamani! Tukiwa wanafiki ujanani, uzeeni tutakuwa wachawi. Tujitokezeni kwa wingi KUJIANDIKISHA, KUPIGA na KULINDA kura. Haya mambo matatu sharti yaende kwa pamoja—haya ni sawa na mafiga matatu ya ushindi. Vinginevyo tutaendelea kumtafuta mchawi hadi Yesu akirudi bado hatujampata. Vyama vya siasa vinapaswa kufanya jitihada za ziada katika kuwahamasisha vijana kushiriki siasa kawa maana ya kujiandikisha, kupiga na kulinda kura. CCM wakijua kwamba eneo fulani wana uhakika wa kushinda hawafanyi fujo wala kuwatumia POLICCM kuchakachua kura.

MWAMKO WA KISIASA MIONGONI MWA WANANCHI
Katika maeneo mengi ya nchi, mwamko wa kisiasa na mabadiliko miongoni mwa wananchi ni mdogo sana. Kuna watu wazima wenye elimu ya kutosha lakini utakuta mwamko wao wa kisiasa upo chini sana au uko tofauti sana na jinsi unavyoweza kuwafikiria. Walimu na POLICCM bado wana mawazo mgando ya kuiunga mkono CCM pamoja na kwamba CCM imekuwa ikiwakandamiza, kuwafukarisha na kuwanyima haki kwa muda mrefu. Hili kundi la watumishi ni kama vile limedumazwa akili na CCM. Zinahitajika jitihada za kufa mtu ili kulikomboa kundi hili kwani linaonekana kama vile limelemazwa akili na ugumu wa maisha wanaokandamizwa na CCM na serikali yake ya kifisadi. Mwamko wa kisiasa miongoni mwa wananchi wa kawaida ni mkubwa sana ukilinganisha na watumishi wa umma wanaonyonywa na kubebeshwa magunia ya misumari na CCM kwa muda mrefu sana. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba hata POLICCM huonyesha mapenzi yao kwa CCM waziwazi bila kificho huku wakisahau kwamba CCM hiyo hiyo ndiyo huwalipa mishahara duni na kuwalaza kwenye mabanda ya mbwa yasiyostahili kukaliwa na binadamu. POLICCM ni miongoni mwa kada za watumishi wanaoishi maisha duni sana na ambao hulipwa mishahara isiyowatosha kujikimu hata kwa siku 10! Lakini utashangaa sana ukifika wakati wa uchaguzi wanakuwa waaminifu na watiifu kwa CCM kama vile mbwa anavyomtii bwana wake—hata kama akimlisha mifupa ya mawindo yote huku yeye (bwana) akila minofu na kusaza!

USHAURI KWA CHADEMA NA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI
Vyama vya siasa hasa CHADEMA vinapaswa kuwa mstari wa mbele kugawa elimu ya uraia kwa wananchi ili wajitambue na kuachana na CCM na wanatakiwa kuanza mchakato huu tangu sasa—saa ya ukombozi ni sasa—wasisubiri hadi wananchi wakajisahau mpaka uchaguzi ujao watakapogawiwa ubwabwa na CCM na kuichagua kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. CHADEMA hawatakiwi kulala usingizi hata kidogo kwani wana kazi kubwa ya kuwaelimisha vijana juu ya umuhinu wa kupiga kura.

Vijana wengi bado hawajajua umuhimu wa kupiga kura. Yaani eti kijana hutoka nyumbani siku ya kupiga kura akiwa na rungu lake anasimama hatua 100 kwa ajili ya kulinda kura huku akijua fika kwamba yeye na vijana wenzake (wanaolinda kura za CCM) hawajapiga kura! Ni ajabu iliyoje! Utalindaje sanduku la kura za watu wengine huku wewe mwenyewe hujajitokeza kupiga kura? Dawa ya ushindi ni kupiga kura sio kulinda masanduku ya kura ambazo hazikuhusu. Vijana tubadilike tuwe na ufahamu juu ya umuhimu wa kupiga kura kwa kuwa kura ndizo humpelekea mtu kushinda, si vinginevyo. Rungu la kulindia kura ni mzigo tu! Haliwezi kuchangia ushindi hata siku moja. Piga kura kwanza kisha uzilinde. Huwezi kulinda kura ambazo hujazipiga huku ukitegemea miujiza ya ushindi. Vijana wote amkeni kutoka usingizi wa pono mliolala na kuleta mabadiliko chanya sasa na baadaye. Ukombozi wa nchi hii kutoka utawala wa kikoloni wa CCM upo mikononi mwenu. Haya yote yatawezekana ikiwa kila mtanzania mpenda maendeleo atacheza nafasi yake ipasavyo.

Nawatakia mabadiliko mema na ya haraka.:israel:

mkutano chadema.jpg
 
Mahadhara ya kunywa gongo ungali bado mdogo.
Bila shaka hiki ni kizunguzungu cha makonde 23 kichwani.

Kunywa Panadol ukalale, maandishi marefu hatusomi.
 
Ni kweli, hata uchaguzi wa 2010, Dr Slaa ndiye aliyeshinda, halafu NEC wakachakachua matokea kura za Dr. Slaa wakampa JK, na za JK wakampa Dr. Slaa ndio maana mpaka leo Dr. Slaa ndio rais wa kweli wa Tanzania!, JK ni rais wa NEC tuu!. Ndia maana Chadema ilitangaza rasmi, haimtambui JK kama ndie rais wa Tanzania!, rais ni Dr. Slaa, na mpaka leo, Chadema hawajawahi kutangaza kumtambua JK, ila zile chai na juice za ikulu, chadema walikuwa wanakwenda tuu ili kufanya rehesal ya 2015!.

Pasco.
 
Imekaa vizuri CCM wanajifia wakati hakuna jipya waliloongeza.
 
Pamoja sana kamanda
Ujinga mwongine mbaya sana.... endelee hivyohivyo et chama pendwa umati wa watu kwenye mikutano sio ndo wapiga kuru.... ccm kata 23 chadema 3 ndo kimeshinda acha ujinga wewe
 
Siku zote nasema elimu ndogo ya Watanzania wengi ndiyo kipingamizi cha mabadiliko. Kamwe Tanzania hayatatokea yaliyotokea Kenya. Katika conspiracy theory zangu naona kuangukaa kwa elimu TZ ni makusudi na haya ndiyo matokeo yake.
Kwa matokeo haya nimekata tamaa ya 2015 (maana dalili ya mvua.... hawa madiwani ndiyo mhimili wa watu wa mashambani walio wengi) unless upinzani waungana na kuanzia sasa waanze countrywide civic education.
Ah, laakini huo upinzani tunaouzungumzia ndio huo huo ulionyimwa elimu ila wachache. Hawawezi kuungana na kwa hiyo hakuna hope.
 
tpaul Ulitakiwa kuleta takwimu za idadi ya kura na si brabra, unawalaumu vijana ulitaka wasifike kwenye mikutano kwa sababu tu hawana vitambulisho vya kupigia kura? Unajua tatizo la kukosa vitambulisho ni pamoja na kutokurekebishwa kwa daftari la wapiga kura.
 
Last edited by a moderator:
Ujinga mwongine mbaya sana.... endelee hivyohivyo et chama pendwa umati wa watu kwenye mikutano sio ndo wapiga kuru.... ccm kata 23 chadema 3 ndo kimeshinda acha ujinga wewe

watanzania mil 5 unusu wanasubiri kuandikishwa kwenye daftari , BORESHA DAFTARI UONE KAZI !
 
Ni vizuri kuendelea kujifariji maana hakuna msiba usiokuwa na mwenyewe, sasa mbona bado huendi kutoa hiyo elimu ya uraia kwa hao unaodhani wana elimu duni ya uraia na uelewa hafifu ?
 
Ujinga mwongine mbaya sana.... endelee hivyohivyo et chama pendwa umati wa watu kwenye mikutano sio ndo wapiga kuru.... ccm kata 23 chadema 3 ndo kimeshinda acha ujinga wewe

CCM kimepoteza kata 4 (27-4=23). Hata mtoto wangu wa chekechea anakuzidi akili!
 
Wakati mwingine kuna haja ya kuwa na Daktari wa magonjwa ya akili ili atumie kifaa maalumu cha kupimia akili kwa wanaotaka kupost. Mtu anaandika makala ndeeeefu na kupoteza muda mwiiingi kuleta post yenye hoja dhaifu kabisa na haina ukweli wowote. Hebu fikiria kudai kuwa kote CVM ilikoshinda tatizo ni wapiga kura wanaelimu ndogo sana ya uraia! Wakati huo huo anadai CDM imeungwa mkono na watu wengi sana baada ya kupigiwa kura na watu wengi hivyo kupelekea tofauti ya kura iwe ndogo! Hivi maana yake nini basi? Kwa sababu watu ni walewale, walioichagua CCM ni wale wale na eneo ni lile lile, pia baadhi yao wakachagua CDM na wakazidiwa na wa CCM. Kwanini kuwatukana walio wengi walipoikataa CDM? Huoni kuwa hawa wametimiza haki yao ya Kikatiba? Je mleta posti anafahamu kuwa kuwalazimisha wananchi walioipiga stop CDM ni kuvunja katiba? Namusihi aache watu wachague kile wanachokipenda. Demokrasia ya kweli ni pamoja na kutofautiana kimawazo. To agree to disagree.
 
CCM kimepoteza kata 4 (27-4=23). Hata mtoto wangu wa chekechea anakuzidi akili!

Na Chadema wameongeza Kata ngapi?Hii analysis ndiyo kwanza naiona kwenu.Sijawahi kuiona sehemu nyingine yoyote duniani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom