Hapa nimeongelea takribani masuala manne lakini badala ya watu kujibu hoja kwa hoja, baadhi yao wanaanza kuniporomoshea matusi. Nimegusia hoja zifuatazo ambazo ndizo zinapaswa kuwa nguzo ya mjadala wetu:
1. Nguvu ya CHADEMA ambayo inazidi kukua siku hadi siku kwa kuungwa mkono na makundi ya vijana na wazee ukilinganisha na chaguzi zilizotangulia-kuna baadhi ya maeneo, hasa Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma, Tabora, nk ambako CHADEMA ilikuwa haisikiki kabisa. Lakini kufuatia mikutano ya M4C iliyofanyika takribani nchi nzima, wananchi wameanza kuipa support CHADEMA. Katika suala hili hatupaswi kuelekeza macho yetu katika uchaguzi ulioisha hivi karibuni bali tuangalie mwelekeo wa CHADEMA kwa ujumla tangu mwaka 2000 hadi leo.
2. Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni ndogo sana (<25% ya wapiga kura waliojiandikisha). Hili tatizo limeathiri vyama vyote lakini CHADEMA ndio wameathirika zaidi kwa kuwa vijana wake wengi hawakujitokeza kupiga kura. Hili ni suala ambalo linapaswa kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ni kwani vijana hawapendi kupiga kura.
3. Mwamko wa kisiasa miongoni mwa wananchi (hasa yale makundi nyanyaswa-walimu, polisi, magereza, wakulima, etc) bado upo chini sana. Watu wengi hawajapata kutambua uhusiano uliopo kati ya umasikini na maisha duni wanayoishi na udhaifu wa serikali iliyoko madarakani.
4. Ushauri wa jumla kwa serikali, tume ya uchaguzi na vyama vya siasa kuhusu namna ya kufanya wananchi wapende kushiriki siasa kwa maendeleo yao. Umuhimu wa kupiga kura na thamani ya kura kwa kila mpiga kura inapaswa kuelezwa kwa umma ili kuwafanya raia wapende kushiriki katika chaguzi mbalimbali.
Haya ndiyo mambo ninayotaka tuyaongelee hapa badala ya kuleta kejeli za ‘chopa 3 kata 3' na upuuzi mwingine kama huo. Tatizo ni kwamba kuna baadhi ya watu wanadhani kwamba CCM kuendelea kukaa madarakani (for no reasons) ni muhimu kuliko kuzingatia usatwi wa watanzania walio wengi wanaotaabika na ufisadi, udhalimu na utapanyaji mali unaofanywa na CCM na serikali yake huku maisha ya watanzania walio wengi yakizidi kudidimia.
Turudi kwenye mjadala.:israel: