CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Propaganda za kizamani.Kama kweli IGP Mangu amekubali kutumiwa na maccm ajue kuwa mbinu hii ambayo ilipata kutumiwa na Mahita huko nyuma haikufua Dafu na haitofua dafu.Atashindwa kama walivyoshindwa wenzake
 
Jamani utetezi wenu ni dhaifu sana. Kwanini hamuelezi zana hizo zinafanya nini ofisini mwa CHADEMA?

Au ni kawaida kukuta zana za aina hiyo kwenye maofisi!?! Ingekuwa Somalia sawa, Tanzania watu wanakaa na visu, beto na majambia pamoja na nguo za jeshi ninyi mnaona ni kawaida tu?

Nguo za jeshi ziko wapi hapo?na zana za kijeshi ziko wapi hapo?acheni maneno yenu ya kwenye kahawa
 
Ngoja Tuende Ila Tusipovikuta Tutakuitaji Polic, Kwa Ajili Ya Kuisaidia Polic.

Hizo sinema za Policcm tumeshazizoea! Kuelekea Uchaguzi Mkuu kesho yake mwaka 2000, Mkuu wa Jeshi la Polisi wa wakati huo, IGP Omari Mahita alitutangazia kuwa CUF wameingiza makontena ya majambia kwa lengo la kuvuruga Uchaguzi, na pia alituonesha sample ya majambia hayo yakiwa na nembo za CUF! Kwahiyo propaganda na maigizo mnayotufanyia hayauziki! Hata mkimtumia huyo Yuda wenu!
 
stanlthecreator

Naona mmepoteza mwelekeo wa kuongoza Nchi mpaka Mwenyekiti wenu wa chama pia kapoteza mwelekeo.
Kajisahau kutoa heshima kwenye kikosi cha bendera! Na kupitiliza mpaka alipojiona km yuko mwenyewe, ndo akarudi.
Imetokea leo alipokuwa anakagua gwaride kwenye sherehe za muungano..
 
Last edited by a moderator:
Sasa tatizo moja mimi huwa siongei na mijitu miongo. Nyoosha maelezo yako ile bendra ilikuwa ni ya kundi gani na linasifa gani. Bainisha silaha walizokutwa nazo hao watu, na ueleze wasifu na mazingira yao, utofautishe na hili ulilolipika na kutaka kufa nalo hapa.

Kama wewe ni kada wa uwongo, basi wewe ni mtumishi wa shetani na nitajua hili utakaposhindwa kunyoosha maelezo kama nilivyokuamuru. Na kama ndivyo, nitakutenga sawa na mijuha mingine niliyoitenda humu. Uwe mkweli ili tuongee.


Juzi juzi magaidi wa kule Morogoro walikutwa na vifaa kama hivyo vya CHADEMA yakiwemo: Manati, Visu, Majambia na bendera nyeusi.

Mimi sio gaidi na siwezi kujua matumizi ya kila kimoja wapo kati ya hivyo, labda CHADEMA watueleze ni nini kazi ya manati na hivyo visu hapo ofisini kwao.
 
Kama ingekuwa rahisi hivyo wangeanza na gaidi number moja Tanzania.

Hivi hii ni Uniform ni ya jeshi gani?
Hiyo Kofia je?
Hilo Buti je?

attachment.php

View attachment 246887

Ukiwa CCM sheria haikugusi. Manati ambazo asilimia 50 ya watoto vijijini na familia nyingi wanazimiliki leo kuna mtu anataka kutuaminisha kuwa ni silaha za kijeshi.

Wawakamate sungusungu wa CCM kwaza. Wasituletee propaganda za kutunga.
 
Watanzania umefika wakati tuwe makini, maana mwelekeo si mzuri tuwapime watu malengoyao nini
 
Siku hizi chadema wana migodi?

Hivyo visu na manati nazo za nini kwenye siasa?

Sikuhizi ukienda dukani unauziwa assemblies zenye umma, visu, na openers. Na tunavyo vingi madukani. huku mitaani kuna kunguru wengi na ngedere. tumeshauriwa ili kuwapa scare hao viumbe ni kuweka manati zikininginia juu ya miti.Je, sisi tutakamatwa na kuwa in possession na vifaa vya kijeshi?
 
Ni ujinga uliopindukia kudhalilisha jeshiu letu, toka lini manati na kisu vikawa vifaa vya kijeshi jamani? Ni nyumba gani au familia gani isiyomiliki kisu kwa ajili yakukata nyama, vitungu na nyanya. Mnataka kutangazia numma na mataifa ya nje kuwa sisi vifaa vyetu vya kijeshi ni manati na visu? Ujinga mwingine haupaswi kuandikwa humu ndani na aliye post huu upuuzi ni mjinga kweli wa kupindikia

Mkuu hii ni comedy ambayo haijawahi kutokea sehemu yeyote duniani,eti visu viwili na manati ni vifaa vya kijeshi hii ni kujiaibisha bure
 
Ccm ni mwakilishi wa Shetani na ndio maana matatizo ya Watanzania yanendelea kukua siku hadi siku. Ccm badilikeni na mfanye mambo ya msingi.
 
Hii inafanyika tanzaniaa tuu sijawah ona mahalaa pengine karika hali isiyo ya kawaida kamanda wa polisi mkoa wa mbeya ahmed msangi amesema amewakmata watuhumiwa wawili wanaoaminika ni wanachama wa chadema wakiwa na silaha na baruaa silaha hizo ambazo ni manati na visuu

My take
Kama watuhumiwa wamekamatwa maana ake zile.silaha ni ushahidi tosha ambazo zitatumika kama kizibiti
Sasa kizibit k inaonyesha live na mwandishi wa habari ana kamanda anashika bila kuvaa groves.kuzuia finger print
Hii ikoje wanajamvi
 
Ile habari sijui imeripotiwa vipi, maana nimeshindwa kutofautisha habari ya mkono wa Albano na hizo zinazoitwa silaha za kijeshi.
 
Ni maneno ya umati mkubwa wa watu waliolipuka kwenye ukumbi mmoja wa starehe kufuatia taarifa ya habari ITV kuhusiana na kukamatwa kwa silaha na vifaa vingine kwa mwanachama wa CHADEMA. Wameng'aka na kuonekana kuitaja ccm kama mhusika mkuu wakilinganisha kubambikiziwa CUF Miaka ya nyuma vifaa kama hivyo. Hakika kama ccm wakiendelea hivi sidhani kama tutafika.
 
Utumbo mtupu! manati ni silaa? sheria gani inazuia mtu kuwa na kisu? angeanza na wamasai wote
 
Back
Top Bottom