CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Ccm hali mbaya,wamalize kwanza sintofahamu ya makundi ya wagombea urais waliyonayo ndo waanze hayo maigizo yaliyowahi kuigizwa hata na IGP mahita kuhusu cuf
 
Hiki chama wana magamba wenzangu ni cha kigaidi sasa karata pekee iliyobaki ni kuwahusisha na alqaeda na alshabab ili viongozi wake wapelekwe the hague tupumue maana ishakuwa taabu..mbinu zote tumeshindwa na taarifa iliyopo hawa jamaa wanazd kututeketeza wamesambaa kama nyuki hata ile mbinu tuliyotegemea ya kutumia third part ili nguvu zipungue inaonekana ndo kwanza inawaimarisha sasa hapa kuna mambo mawili either kifutwe au turushe taulo uwanjani kama mchezo wa masumbwi kukubali kushindwa kabla ya uchaguzi
 
propaganda za ccm. ccm wanahalibu jeshi letu la polis kwa kuliingiza kwenye malumbano ya kisiasa yasiyo na maana.
 
Asanteni Mods kwa kutupatia uhuru wa kujadili hii taarifa.

JF is where we dare to talk openly!
 
Marekani waje bongo watukague kama Iran na Iraq make tunamiliki manati ambayo ni silaha za maangamizi na za kivita.
 
nadhani hili ndio swali la kichovu kuliko yote yaliyoulizwa
tangu mwaka huu uanze .

Huyo Molemo kaja ni kihabari chake eti cha kusahihisha! Sasa anasahihisha nini wakati wasomaji wana macho na wanaona kabisa Makamanda wa CHADEMA wakiwa wameshikiliwa na polisi na vifaa vyao vya kuasi vipo hapo mezani tena ofisini. Sasa hapo tena watu wanahitaji ushahidi wa ziada?
 
Hivyo vifaa vyote ni uongo na mbinu chafu, njaa na unafiki vikimkaa mtu kichwani ni hatari sana. Wakati mwingine tufanye vitu huku tukitambua hapa duniani si makazi yetu ya kudumu.
 
mbona uzi wa mlemo umeunganishwa?

Habari ya Molemo ni ya uzushi na yeye hana mamlaka yoyote CHADEMA hivyo sio mtu sahihi kusahihisha jambo lolote kwa niaba ya CHADEMA humu JF.

Hiyo ndiyo sababu uzi wake umetupiliwa mbali.
 
Ni ujinga uliopindukia kudhalilisha jeshiu letu, toka lini manati na kisu vikawa vifaa vya kijeshi jamani? Ni nyumba gani au familia gani isiyomiliki kisu kwa ajili yakukata nyama, vitungu na nyanya. Mnataka kutangazia numma na mataifa ya nje kuwa sisi vifaa vyetu vya kijeshi ni manati na visu? Ujinga mwingine haupaswi kuandikwa humu ndani na aliye post huu upuuzi ni mjinga kweli wa kupindikia
 
Huu Uzi ulikuwa umefungwa sijui kwanini wamefungua tena.
 
Mbona polisi wamekosea walitakiwa waweke na rangi ya chadema kwenye visu kama kipindi kile cuf ,washakosea tena halafu wameweka visu vidogo bora wangeweka vikubwa.
Hivi kumbe tuna jeshi la hovyo namna hii?? Hadi moja ya vifaa vyake ni manati? Bora Malawi watupige tu.
 
ccm ifeke mahali waache ujinga,mm huwa nawapigia kura wagombea wa ccm kila uchaguz ila kwa hili nitabdlisha uamuzi,viongozi wangu ni kama hawafkrii tena ilmradi siku ziende.
 
Simbakibogoyo sasa unaelekea kuwa simba poyoyoyo!. Waambie familia yako wakuwahishe milembe. Inauonekana umepata umewehuka baada ya kuona ccm imepoteza namba. Sasa kinatokelezea kwenye miiko, vyungu, mikasi, na bendera za CHaDEMA.

Poleni sana wauguliwa!.

Juzi juzi magaidi wa kule Morogoro walikutwa na vifaa kama hivyo vya CHADEMA yakiwemo: Manati, Visu, Majambia na bendera nyeusi.

Mimi sio gaidi na siwezi kujua matumizi ya kila kimoja wapo kati ya hivyo, labda CHADEMA watueleze ni nini kazi ya manati na hivyo visu hapo ofisini kwao.
 
Back
Top Bottom