CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Waku taarifa ya itv imeonyesha vijana wa chadema maarufu Kama redbrigade wakiwa na visu viatu vya jeshi Pamoja na kiganja Cha albino hakika hii imenisikitisha sana

Mwanangu kweli safari hii mbinu zote zimegoma, kuna sijui uzalendo, siasa safi zote zimegonga mwamba. Yaani habari ya kipuuzi kweli, eti wanaonyesha vitu vilivyokamatwa kwenye sijui ofisi ya cdm, mara wanachomekea habari ya albino. Hivi bado wanadhani watu ni wajibga hivyo? Hizo mbinu za kizee kwa sasa zimepitwa na wakati.
 
Mnaanza kazi yenu policcm,chadema sio chama mfu mbinu zote tutawanasa tu na propaganda mnazotumwa na ccm
 
Tabia ya chadema ni kufanya vurugu kwenye mikutano yao ,kisha kuropoka kwenye vyombo vya habari kuwa polisi wamewafanyia fujo, pumbavu sana hawa watu.
 
T-shirt, kofia na manati ni vifaa vya kijeshi? Ama kweli kumbe police ni chombo cha ccm. Ndio maana hata raia wanawabandikiza misokoto ya bangi na mengine mengi. Lakini police mtambue mwezi wa 11 mtakua chini ya CDM.
 
Hahahaaa. Siasa za kitoto. Kama za chuoni...
 
CHADEMA hila zenu dhidi ya Amani na utulivu wa taifa hili zinaendelea kubainika!Watanzania wapenda Amani hatutakubali upuuzi huu!
Hivi na umri wako huo ulio nao, nawe unajiunga na wapuuzi wanaotaka kudhalilisha TPDF kuwa inatumia manati kulinda nchi. Eti wamekamatwa na silaha , silaha zenyewe manati, ambayo hata mimi ninayo, tena nina visu hapa nyumbani kwangu, kana kwamba hilo halitoshi nina panga. Ina maana nami ni mtuhumiwa wa kumiliki silaha za kivita kwa mjibu wa sheria za Tanzania, if it is true tutakuwa ni one of the strange nation on earth, Watu waache kudhalilisha nchi
 
Yaaani ni kichekesho siasa zimewashinda ccm wanakimbilia kukamata manati hahahaaaa
 
Huyu Rpc nazani hayuko sawa jamani inabidi wanabodi tufikirie kwa kina zaidi,hivi huyu Rpc mse..nge si ndiye alisifiwa na mwigulu kwenye email zilizokuwa hapa jukwaani kwenda kwa zito akimpongeza kwa kuendesha kikosi kilichomuua dr.mvungi? Kama ni kweli basi damu ya dr.mvungi imemkalia kichwani sio bure...
 
Hivi na umri wako huo ulio nao, nawe unajiunga na wapuuzi wanaotaka kudhalilisha TPDF kuwa inatumia manati kulinda nchi. Eti wamekamatwa na silaha , silaha zenyewe manati, ambayo hata mimi ninayo, tena nina visu hapa nyumbani kwangu, kana kwamba hilo halitoshi nina panga. Ina maana nami ni mtuhumiwa wa kumiliki silaha za kivita kwa mjibu wa sheria za Tanzania, if it is true tutakuwa ni one of the strange nation on earth, Watu waache kudhalilisha nchi
Sasa CHADEMA wanazitumia kufanya nini kama sio uhalifu!?
 
Watanzania tumeshatambua kuwa CHADEMA wanatumika na kufadhiliwa na maadui zetu kuvuruga Amani ya Nchi!

.... Labda Wewe Kilaza. Mim Kwangu Nina Panga, Kisu, Buti, Nondo, Rungu Na Buti, Njooni Mnikamate
 
Ujinga ujinga. Nilitegemea kuona siraha za kijeshi kutokana na Heading.kila rpc ana yake mwingine yupo busy na gwagima,huyu mawani ya piki piki vifaa vya jeshi kazi ipo,,tutaendelea kusikia bado mwanza na arusha.
 
sio ile sinema ya cuf ya omari mahita kweli?mungu atusaidie pilis watende haki la sivyo mwaka huu ni majuto
 
Sijaona vifaa vya kijeshi hapo, nilitarajia kukuta MG, LMG, RPG, mabomu ya kutega ardhini na ya kutupa, kifaru nk, ninachokiona hapo ni nguo za mitumba za mtaa wa kongo wanazovyaa wasanii huko marekani na buti za migodini...teteteh....kama hizo ndo taarifa za kiinterejensia tutashuhudia mengi mwaka huu

vipi zile alizovaa diamond naye ni gaid
 
Hahahahaaaaa! Uongo mwingine bhana! Unafikiri watanzania wote ni wajinga? Walikamatwa na mavazi ni wengine na waliokamatwa na kiganja nako ni wengine.Ila vyote vilikua kwa Kamanda Msangi.Mwogope Mungu mkuu,wewe ni reporter fake.

Hivi mbona ndani ya Chama tawala naona bado kuna watu makini ambao wangeweza kuwashauri juu ya mbinu sahihi kwa kizazi hiki? Nimesikitishwa sana na mbinu za ki-primitive ambazo haziwezi kuwa na tija hata chembe ku twist akili za watanzania wa leo! Kweli Mungu akitaka kuangusha ufalme anawapofusha wote macho! Lol!
 
Ukitoa vifaa vya kijeshi hizo manati na visu chadema mnawinda ndege siku hizi?
 
Siku hizi chadema wana migodi?

Hivyo visu na manati nazo za nini kwenye siasa?

kama kuwa na kisu ni ugaidi Tanzania nahama mwaka huu,manake hatabaji hata mtu mmoja salama hii dhambi ya kukamata watu na visu na kuwaita magaidi itatumaliza wote
 
1. Mohamed Msangi

2. Ramadhan Ighodu

Hawa wawili ikumbukwe ndiyo waliomteda Ulimboka nabaada yapo wakapandishwa vyeo.

Naona msangi kanogewa na zoezi la kuteda watanzania kwa matarajio ya kupata madaraka zaidi.
 
Back
Top Bottom