andrewk
JF-Expert Member
- Apr 13, 2010
- 3,102
- 488
CHADEMA 'THINK-TANK' MAKAO MAKUU HUSIKENI MOJA KWA MOJA NA MAWAZO YETU SISI WENYE CHAMA CHETU ILI KUNAWIRISHA ZAIDI AZMA YETU YA KUWAKABIDHINI DOLA 2015.
Tulia mtoto DubiousBrain, acha kupiga mayowe bure hapo chini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wana-CDM msihangaike naye sana huyu kwani kila soko kuna kichaa wake na sisi hapa JF tunao wendawazimu 9 ambao mmoja wao ni huyu na yule Nape. Twende nao hivo hivo maana nao wana haki ya maoni hata kama ni upupu.
Wewe mtani DubiousBrain, sasa naanza na SERIOUS BUSINESS kwa wana-CDM, kwako wewe subiri kidogo utaona utamu wa chama kupendwa; hakuna kugasi wafanyabiashara kupitia siasa za TRA bali hapa ni sisi wenyewe wananchi ndio tunakiomba CHADEMA tukichangie kwa ajili ya kupatikana vituo vya kweli vya televisheni ya TAIFA pamoja na radio.
Kuendeleza elimu ya uraia kote nchini hasa vijijini maana CCM huwa wamewekeza zaidi katika umbumbumbu wetu wananchi.
Na kwa kuwa tumegundua siri kubwa ya CCM ni kutumia mabalozi wa nyumba kumi kama nguzo kuu ya KUCHAKACHUA KURA kama walivyokamatwa wakifanya kule Igunga, lengo letu vijana sasa ligeukie kunyakua viti vya utawala vyote vijijini vikiwa ni pamoja na kiti cha:
1. Mwenyekiti wa Kijiji,
2. Kiti cha Udiwani,
3. Kiti cha Balozi wa Nyumba Kumi
4. Mashina ya Chama katika kila kata na kijiji (kuwepo watu wa kuhiari kutumikia chama na wa wa kuhiari kufadhili uendeshaji wa ofisi husika).
5. Benchi la Matawi ya CDM katika vyuo vikuu kote nchini.
6. Kuwaomba wenzetu walioko huko ughaibuni nao kufungua matawi huko huko.
7. Matawi yanayoratibu Maendeleo ya akina Mama CHADEMA vijijini.
8. Kubadilisha haraka USIMAMIZI WA UCHAGUZI usifanywe na wakurugenzi wa halmashauri za miji ambao siku zote makada wa CCM, badala ya kazi ifanywe na taasisi huru kabisa kama vile NGO.
9. CHADEMA kianzishe mfumo wa kepembua vijana maalum (Young Turks - wasichana kwa wavulana) katika ngzi ya kila Kata na waandaliwe vizuri sana kuwa MA-KADA watarajiwa wa chama n waunganishwe ndani ya BAVICHA.
10. Mawasiliano rasmi nazisizo rasmi kati ya makao makuu ya chama na mashina na vyombo vyote vya CDM bila kusubiri ha siku za uchaguzi tu.
Da Regia, ni vema kutumike teknolojia za kisasa zaidi, zenye tija zaidi, haraka zaidi, na yenye kuleta uwepo wa maafisa wa juu CDM kuwa karibu zaidi na waongozwa mashinani. Kwani tujue kwamba kujenga mtandao mzito kama hivi sasa CDM ni jambo moja na kulihudumia huo mtandao kuendeleza uhai wake ni jambo lingine kabisa.
Mpaka leo hii kila mmoja anaju ni mchangu muhimu kiasi gani kilichofanywa na viongozi wetu BAVICHA kule Igunga - kweli BAVICHA ni mashine kubwa mnooo!!!!!!!!!!!!!!!
Huu ndio wakati mwafaka wa kukipa CHADEMA nguvu kweli kweli ILI KIENDELEE KUPAA zaidi na zaidi. Hakika maeneo hayo saba yakitekelezwa vizuri basi nawahakikishieni kwamba watu tutaona moto mkubwa ajabu wa mabadiliko nchini. Siku zote vita bila mikakati endelevu ni kazi bure twende sasa!!!!!!!!!!!!
NB: kwa kuwa umemaliza kusoma mawazo yetu haya hapa hebu sasa malizi kwa kusema maneno haya hapa:
'MABADILIKO YA KWELI NCHINI KUPITIA CHADEMA SIKU ZOTE YANAANZA NA MIMI NA NI JUKUMU LANGU KUWA SEHEMU NA CHACHU WA MABADILIKO HAYO NINAYOYATAMANI.'
Mawazo mazuri sana, hao wanaosema cdm imepoteza hele bure kule igunga...... naazikdi kupoeta imani na CCM, kwani kama hao ndio watete wa CCM, basi ... kuna msemo unasema ukiona paka kakubali kulala chali.......shughuri imekwesha