CHADEMA waanzishe na kumiliki News Media zao

Mjadala mzuri sana huu na pia idea ni nzuri na nafikiri inabidi ifanyie kazi na mjasiriamali au wajasiriamali wenye nia na ujuzi kwenye hii nyanja.

Ila ningependa kusahihisha matumizi ya neno moja ambalo naona baadhi ya watu wamelitumia. Nafikiri neno "KUCHANGIA" inabidi liwe open zaidi. Labda tungesema kuwa tuko tayari "KUNUNUA HISA" ili uongozi uwe responsible katika uendeshaji wa kila siku.
 
Mawasiliano ni muhimu, na kutegemea tu vyombo vinavyomilikiwa na serikali na watu binafsi hakuna uhakika wa habari kuwafikia walengwa kwa wakati muafaka. Na pengine habari kuchakachuliwa na hivyo kupoteza maana na umuhimu uliokusudiwa.

Pia uelimishaji wa elimu ya urai na haki za raia kwa wananchi itarahisishwa. Kuegemea tu vyombo vinavyounga mkono hoja za Chadema na jitihada za kulikomboa taifa toka kwa mafisadi si hakika kwa vile vyombo vingine tumeshuhudia mara nyingi vikiyumba katika msimamo wao wa kutetea haki za wananchi.

Kwa kuanza wangekuwa na kituo kimoja cha kurushia matangazo ya television na redio, na pia kuwa na gazeti linalotolewa walao mara moja au mbili kwa mwezi.

Huu ni ushauri wangu binafsi kwani mawasiliano ndio njia pekee ya haraka na kwa gharama nafuu kuwafikia wengi kwa haraka.

Hii ni njia mojawapo muhimu katika kuimarisha uhai wa Chadema.
 
Cha msingi, vyama vya siasa pamoja na serikali vizuiliwe kabisa kumiliki chombo chochote cha habari.

Watumia vyombo vya habari vilivyopo. Vyama vya siasa wakati wote ni serikali ilioko katika chumba cha kusubiria wageni, serikali kwa kipindi hiki cha soko huria ni MUWEZESHAJI TU. Sasa watatekelezaje huo wajibu wa uwezeshaji kama huku JK anafikiria kumdhoofisha Mengi na ITV yake kumuibia kkikundi cha akina Masanja.

Hebu angalia mpaka sasa CCM inayo vyombo vyake vile, inayo vyombo vya serikali vinavyopashwa kuwa ya wote na vile vile inavyo vyombo vya Rostam Azizi; vyote vikifanya kazi moja tuu kutetea UFISADI na UDHALIMU kwetu sisi wananchi.

Naomba nitofautiane kabisa kimawazo katika hoja hii. Kwenye katiba hili nalo lishughulikiwe.
 
Ndugu zangu nimekuwa nafuatilia matangazo ya radio na tv zetu naona nyingi zipo upande wa chama tawala, kama hii Clouds ya Kibonde ni full CCM, jamani tunahitaji kuwa na radio makini ambayo itakuwa inatupasha ukweli wa mambo bila kufunika, watanzania wengi zaidi wanasikiliza radio kuliko kutazama tv au kusoma magazeti. Tunahitaji nasema tena tunahitaji na ninaamini tunaweza kuwa nayo kabla ya mwisho wa mwaka huu. Wakuu naomba kuwakilisha!
 
angalau wengine tuna fursa ya kuingia humu jamvini na kupata ukweli lakini watanzania wengi bado wanalishwa sumu za magamba kupitia katika hizi redio zetu zenye rangi ya kijani, ili mabadiliko yatokee hasa kwaa ajili ya ushindi wa kishindo 2015 swala la media lazima tulipe uzito, lazima hata yule wa kule kijijini afahamu kuna chama makini na sasa kinafanya nini sio tu hadi wakati wa kampeni ndio wasikie kuna CDM. NAOMBA WAKUU TULIPE UZITO WA KUTOSHA, hata kama itabidi tuchangie tutachangia hata kwa M-pesa n.k.
 
Clouds, TBC, Zote zinatusikitisha sana habari za CDM hazimo yaani kama kuonja wakati CCM
ndio zinaanza kama hot news, while CDM inakuja mwisho as if is nothing.
itabidi mbadilishe mpige kura wenyewe. la kama ni wananchi hatukubali
 
Nimesikia good news kwamba Chadema wameanzisha kituo cha television, naomba mwenye data atujulishe, je kimejengwa wapi? na pengine kitaanza lili? hii itakua habari njema sana kwani tumechoka na TBC .
 
Ndugu wana JF

Wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo:
1. Mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. Upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3. Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget

Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.

Napendekeza uongozi wa CHADEMA waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CHADEMA kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CHADEMA kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. Katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.

Nawasilisha
 
Huo ni ushauri unaotakiwa kufuatwa chama cha wananchi hugharamiwa na wananchi na sivinginevyo watu wako tayari kuchangia kazi kwenu kuanzisha na kutangaza kwa watu wote kupitia media mbalimbali
 
Ndugu wana JF

wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo
1.mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3.Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget

Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.
Napendekeza uongozi wa CDM waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CDM kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CDM kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.

nawasilisha
Haya sasa, ndio michango ya kulipa deni la hela mlizokopa za kampeni ya Igunga. Hao wa vijijini mtawanunulia na TV pia?
 
Huo mfuko msimkabidhi Mbowe kwasababu mtakuta hela zote zipo counter Bilicanas
Wakati watu wanaongea mambo ya msingi kuhusu ukombozi wewe unaongelea ushoga. hakika pesa za nape zitawapa ujauzito hata mkitumiwa kwa nyuma.
 
Nakubaliana na hoja yako mkuu. wote tumejionea kuwa CDM ni chama kinachokuwa na kupendwa na watu wengi wanaotaka mabadiliko hasa hasa maeneo ya mijini ambako kunauelewa mkubwa. kuna haja kubwa ya kuhamia vijijini ambako wananchi wengi bado hawana elimu ya uraia ambao ndiyo imekuwa mtaji mkubwa wa CCM. wananchi hao waelimishwe kuwa kuna maisha hata pasipo CCM, na wajue CCM siyo mama wala baba yao ambaye wakiachana/kutofautiana nacho ni dhambi. waambiwe CCM ni chama ambacho kinaenda kufa na wananchi wenzao wa mijini wamekikataa kwa kulea mafisadi na kuzorotesha maendeleo ya nchi hii ambayo hayalingani na umri wa miaka 50 wa taifa.

naomba kutoa hoja.
 
Ni mawazo mazuri sana yanayohitaji kuungwa sana mkono!wako wapi viongozi wa cdm,nini mikakati ya kuikuza chama maeneo ya vijijini,nini mikakati ya kuanzisha media ikiwemo radio,magazeti na tv ya chama!?Tupeni tamko enyi viongozi!Wapi Dr Slaa,wapi Mbowe na makamanda wengine!tupeni neno na mikakati!mna support kubwa kutoka kwa wananchi na wadau!Fanyieni kazi wazo hilo.
 
Back
Top Bottom