CHADEMA vs CCM: Nani Mbabaishaji?

Eh!!! Kumbe CHADEMA mkwara wote huo chadema ni CCM B!!! nimwage data?

Waridi, je hiki ni kisasi baada ya NCCR kuitwa CCM B? Mbona walioita hivyo si washabiki wa CHADEMA? Je, chama chenye msimamo kama huu kinaweza kuwa CCM B? naona ukieendelea kuitetea NCCR juu ya kashfa yake ya kupewa fedha za EPA badala ya kuanza kuishambulia CHADEMA. Nakumbuka NCCR mliwahi kuja Zanzibar kuiwekea pingamizi CUF naona mmefanya hivyo tena Tarime lakini mkaumbuka.

CHADEMA: Hatutakoma
na Mwandishi Wetu

 

Asha,
Nikimwaga data utaujua ukweli nao ukweli utakuweka huru. kasirikeni kisawasawa kwanza kabla sijalipua bomu
 
Eh!!! Kumbe CHADEMA mkwara wote huo chadema ni CCM B!!! nimwage data?
Dada Waridi,

Itapendeza ukiandika hoja moja kwa moja kuliko hivi unavyofanya. Kama ni joke basi naomba topic ihamie sehemu husika. Lete data acha utani!
 

alaa, kumbe huyu waridi ndio wale wale mamluki wa demokrasia!!!
ahsante sana bi.asha, mi nilikuwa sijamfahamu ati!!!!
sasa nimemgundua, hana data yoyote isipokuwa anataka kuanzisha majungu, maana hawa NCCR ni kawaida yao kupika majungu na fitna dhidi ya vyama mbadala.wao wamechoka sana kiasi kwamba kadri siku zinavyosogea ndivyo wanazidi kufutika kwenye ramani.
hebu waridi badala ya kupoteza muda kupiga majungu,jipangeni upya ili muweze angalau kurudisha heshima na hadhi ya chama chenu.
 
Dada Waridi,

Itapendeza ukiandika hoja moja kwa moja kuliko hivi unavyofanya. Kama ni joke basi naomba topic ihamie sehemu husika. Lete data acha utani!

Invisible,
Una haki ya kunidai data, get ready.. lakini wakati huo huo nakuomba utafakari ni kwa nini hata kabla sijaleta data watu washarukia eti ni NCCR inataka kulipa kisasi. Hapa JF kama kweli kuna watetezi wa haki basi idaini CHADEMA nayo ilete ushahidi wa madai yake kwamba NCCR ni CCM B. za kwangu naleta, wala usihofu,ila nina maana yangu kuwaulizeni kwanza
 
Dada waridi,

Mimi sina ubaya na allegations wanazorushiana vyama, ila topic ikianza ikiwa fupi hivi inakuwa inachanganya sana. Aidha, hata majibu ya Asha ya kuihusisha NCCR na CCM inanifanya nicheke tu, yani mnaifanya topic ionekane ya kidaku kwani uthibitisho wa kauli unakuwa mdogo. Topic hii naiunganisha na nyingine ambayo pia inaihusisha CHADEMA na CCM.

Ahsante mamangu
 

Mwitaaa!
safi sana kwa kuonesha unalalia upande gani, harakaharaka umemwamini bi Asha kuliko waridi, hujui hapa JF juma aweza kuwa ndiye Joseph, shauri lo
 
Nimekuwa msomaji wa JF karibia miezi 4 sasa, nimechogundua, watu humu, sina uhakika kama ni wote ila asilimia kubwa ni wanachadema, ona tu likiletwa neno lolote kuhusu chadema itakavyo tetewa, arafu iletwe kuhusu ccm inavyo unngwa mkono. nadhni mtuweke wazi hapa je JF ni ya wanachama wa chadema au?
 
Hata wewe uliyeandika utakuwa CHADEMA sio? Sikulaumu, umeandika mara moja na kutoweka haraka! Jiamini, simamia hoja mkuu. Usihame katika hoja ya msingi. Topic inayoongelea ulichoandika ipo.

Kwa post yako ya kwanza napenda kukukaribisha JF, ni ukweli na uwazi tu.

Wenye hasira huwa tunawatuliza wakienda mrama!
 

Mhe.Gosheni,
unasema ukweli, hii JF imeingiliwa sana na CHADEMA. Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.Vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.

Lakini ukweli ni kwamba;
Freeman Mbowe na Wilbroad Slaa ni wanachama hai wa CCM, sasa hivi wanahaha kwa sababu kuna mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama unapelekwa bungeni, mswada huo unapiga marufuku mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti, waheshimiwa hao wanalengwa hapo.

Aidha katika ishu ya Tarime, Chambiri kada wa CCM alikuwa financier mkuu wa kambi ya CHADEMA. unajua nini, ndani ya CCM wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, CCM B yao
kanusheni basi wanachadema
 

Hata mwanangu akija kusoma hapo atashangaa sana maana ni udaku tu!lete Data na kadi zao za CCM!
 


JF is open to everyone, kila anayeingia humu ni lazima ana itikadi yake hiyo hakuna mtu awezaye kubisha, Sasa kuna kosa gani wana CHADEMA wengi wakiwa humu? Nani amekataza TLP, UDPP, UDM, PONA, CCM humu? Wewe kama unahisi kuna wanachama wa CHAMA Fulani wamejazana humu hilo sio kosa la JF, Nimesoma kwa umakini rules za JF sijaona hata moja ambayo inavutia Wanachama wa Chama Fulani.
USHAURI WANGU!
Kama wewe ni PONA nk, nenda kahamasishe wenzako waje wajoin cha msingi waje kujenga HOJA na si VIOJA
 

thibitisheni
 


Pamoja na kutumia mabavu yote na mapesa ya kuwashangaza hata wao wenyewe (Rejea kauli ya M/Mwenyekiti wao P. Msekwa) Tarime ni mfano wa karibuni zaidi, and its likely to happen in Biharamulo nad Mwibara if the elections are to be done.
 

Wala huna haja ya kulalamika.....waalike watu wako wa NCCR wajae hapa nao, halafu mupambanishe hoja tu na CHADEMA, CCM n.k .Tupo wengi ni neutral tutapambanua tu yupi mwenye hoja kuliko mwenzake na kuamua.

Kuhusu mods ....kuna jukwaa la malalamiko,advice etc ....wewe post lalamiko lako hapo ukiona unafanyiwa isivyo haki.
 
Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.Vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.
Waridi wala haijahamishwa kwa sababu ya eti inaigusia CHADEMA, hoja ya CCM vs CHADEMA ilikuwa ipo hivyo MIMI nikaonelea ni vema tukiiendeleza hapahapa. Wenye jazba hawajui siasa, lakini penye wengi pana mengi pia!

Waridi, dadangu hapo umegonga patamu haswa. Hii inaweza kuibomoa CHADEMA endapo unaweza kunisaidia kitu kimoja dadangu, kama una vivuli vya kadi zao za uanachama ama uthibitisho wa kauli hii utakuwa umewasaidia wengi haswa wale waliokuwa wakitizamia kuwa wanachama wa chama hiki kujinasua kabla ya kutumbukia!

Binafsi nitafurahi sana kuona mambo yako exposed hapahapa! Bring em dataz mama...

Aidha katika ishu ya Tarime, Chambiri kada wa CCM alikuwa financier mkuu wa kambi ya CHADEMA. unajua nini, ndani ya CCM wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, CCM B yao
kanusheni basi wanachadema
Dada ndizo data hizi? Please kama kuna proof ya haya ya Chambiri naomba tupe nyeti hizo hata kwa picha au vivuli (scanned copies) mambo haya. Wanafiki wa siasa hawafai kuvumiliwa, kama umedhamiria kuwaumbua basi toa na uthibitisho mkuu waridi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…