Mimi nadhani tuingalie zaidi CCM na uhusiano wake na waislam hasa tukianzia TANU ilivyoanzishwa, viongozi wake, na wanachama wake alafu tuangalie ilivyobadilishwa kutoka TANU mpaka kuwa CCM na uongozi wa CCM ilipoanzishwa mpaka sasa, majibu yote utayapata hapo ndani ya TANU mpaka kuzaliwa kwa CCM. Someni HISTORIA kwa makini.
Mpole
Kama lilivo jina lako naamini utakuwa mpole wa amani bali si kwa kikundi cha watu kupora haki yako. (wanasiasa walio madarakani)
Tunasoma historia ili kujiepusha na kurudia makosa ya awali na pia kudumisha yaliyo mema.
Huku nyuma tulikuwa maskini nchi kibao duniani, lakin wenzetu wanabadilika na wametuacha tunalia na historia.
Mfano, katika kipindi kifupi cha Paul kagame wa Rwanda madarakani, nchi imebadilika na inakimbia kimaendeleo.
Tunatakiwa kubadilika kulingana na wakati badala ya kugeuka nyuma na kuilalamikia historia dunia inasonga mbele, angalia malysia, china nk
Tunapokuwa na serikali inayoongoza kwa hisia na kushindwa kuwajibika kwa watu wake kwa visingizio kila asubuhi hatuwezi kuendelea, Watakwambia majambia ya CUF, watakwambia, Ukristo wa Dr slaa, watakwambia, sheria za uswis ngum kurejesha fedha, watakwambia, Richmond sio ufisadi, watakwambia, ukabila wa wanasiasa, watakwambia ushahida rushwa rada hawana nk
Cha ajabu hao watu wanatuibia haki zetu wazi wazi, ukiiba kuku au mbuzi unafungwa fasta lakini wezi wa Rada, EPA, Meremeta, usafirshaji wa pembe za ndovu wote hao hawafungwi zaidi ya kupandishana vyeo.
Mikataba mibovu ambayo inatughalim fedha nyingi watanzania IPTL, Net group solution nk
Ni jukum letu watanzania kufaham kwamba wanasiasa wanatumia njia mbalimbali kuhakikisha wanabakia madarakani kama vile
- kuchonganisha wananchi kwa maana ya din zao tunapogawanyika wanapata nafasi ya kutuibia kura na hatimae .........
-Kuchonganisha wananchi kwa maana ya makabila yao na kanda wanazo toka, tukigawanyika kwao neema maana wamefanikiwa nk
Bila sisi raia kujitambua tutaishia kupigana na kuwacha wao na familia zao wanajaza matumbo kwa amani sisi tukitekete. Hatuwezi kuirudisha tanganyika ya TAA na TANU.