CHADEMA, uislam na waislam!

CHADEMA, uislam na waislam!

Status
Not open for further replies.
Chadema kujifanya wako karibu na Waislamu wakamtetea Sheikh Ponda eti serikali inatumia nguvu nyingi na Kusema Bakwata haifai!
 
Kwa mtazamo wangu Waislamu waumini wa kawaida wala hawana tatizo na Chadema na Chadema haina tatizo na waislamu, wakristo au dini yoyote ile. Tatizo ni wale vocal muslims, akina Sheikh Ponda na wenzake wa Annuur na Radio Iman.

Hawa wangependa chama cha siasa kitangaze from day one kwamba chama kitafanya hivi kitafanya vile kwa manufaa ya waislam ndipo wakiunge chama mkono. Sasa kwa chama cha siasa ni makosa makubwa kupandikiza mbegu za udini kwa namna hiyo.

Waislam yapaswa wakiunge mkono Chadema si kwa vile wao ni waislam, bali kwa kuwa ni Watanzania kwanza. Wakristo yapaswa wakiunge mkono Chadema si kwa vile wao ni wakristo, bali kwa kuwa ni watanzania kwanza.

Chadema wanalijua hilo na ndio maana namna zao za kujenga mahusiano na makundi mbalimbali zinawabeba wote kama watanzania. Kama wadini hawaitaki Chadema, basi ni tatizo la wadini. Si la Chama.
hata akina ponda hawana tatizo na chadema wasiwasi yao ni pale wanapoona ccm pamoja na mwenyekiti wake kuwa muislam wananyanyaswa, hivyo wanadhani kwamba kwa kuwa chadema mwenyekiti wake ni mkristo watanyanyaswa zaid. lakini chadema haina udini na kama watachukua nchi watakaofaidika zaidi ni waislam.kwani ndio itakuwa mwanzo wa utawala wa haki na sheria
 
Juzi nilimwona kijana kavaa kanzu yake na katupia scafu ya Chadema na alikua natoka msikitini, nilifurahi sana.
 
Hata Nyerere alipohamia Daru ssalam na kukaribishwa na Waislam, aliacha kuvaa kaptura yaani suruali fupi na kuanza kuvaa kibaraka shehe na hata kufunga swaumu siku nzima mpaka kichwa kikamuuma na kuomba apewe aspirini lakini alinyimwa dawa na kuombwa asubiri mpaka futari na baada ya kufuturu na Waislamu Nyerere hakusikia maumivu ya kichwa tena!

Sasa viongozi wa chadema wanachotakiwa kufanya sio kula pilau na Waislamu bali kuingia mkataba na Waislamu kuwa wakishika dola basi watashughulikia kero na madai ya msingi ya Waislamu kuwa...

1. Elimu itakuwa haki ya msingi kwa kila raia na hakutakuwa na ubaguzi wa rangi, dini, jinsia au jiografia kama ilivyo sasa!
2. Shule zote za Waislamu zilizotaifishwa na Nyerere wakati wa azimio la Arusha 1967 wanarudishiwa wenyewe!
3. Mgawo sawa wa madaraka ya nchi na sio dini moja tu kuhodhi kila sehemu!
4. Waislamu wawe huru ndani ya nchi yao kutangaza dini yao bila kuingiliwa na Serikali au Kanisa! mradi wanafuata sheria!
5. na mengine mengi yatakayochangiwa!

Chadema wasijidanganye kuwa watarudisha imani ya Waislamu kwa kula nao Pilau au biriani bali wanatakiwa kutumia mbinu muafaka na mbinu kama hizi hutumiwa hata Marekani na nchi nyingi duniani! hata Kenya Odinga na ODM aliingia Mkataba na Waislamu wa Kenya ktk uchaguzi uliovurugika wa 2007!

Zubeda

hayo madai uliorodhesha umeyatowa wapi? ninamaana hizo kasoro kama zipo nani alizisababisha? japokuwa kwa mtaamo wangu hazipo.

1. umeongelea ubaguzi wa rangi fafanua kidogo hili linfanyika wapi hapa tanzania na kwa misingigani?

2. Aliyetaifisha mashule alikuwa na lengo zuri tu kwa maslah ya watanzania wote, wakirudishiwa na wakristo warudishiwe? Je tunajenga umoja wa watanzania kama taifa au tunabomoa vipande vipande kama unavyopingana katika hoja yako no 1?

3. mgao sawa wa madaraka kwa maana ya Din? vipi kuhusu makabila nayo tutafanya hivyo maana wasukuma ni wengi sana.

b) Je tutafanya usaili wetu kwa maana ya dini zetu, kama ndivyo nafasi ya taaluma ya kila mmoja wetu itakuwa wapi?

c) Endapo tutajipanga kwa maana ya uwiano wa imani zetu, unataka kuniambia Pengo atafanya operation za matumbo na Idd Simba atafanya operation za wagonjwa wa moyo? je hiyo ndiyo maana halisi ya Taaluma na ufanisi kwa fani husika?

4. Nani kakwambia waislam wa tanzania hawapo huru?, Je wapagani wa tanzania wanauhuru gani na kwanini?

5. Chadema haijawahi kushika dola hata siku moja, ccm na serikali yake ndiyo wametutawala tangia uhuru, Je kasoro unazozisema zimesababishwa na

a) chadema kwasababu ndiyo ipo, madarakani na hivyo imewagawa watanzania nakusababisha mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe!

b) CCM ambayo ipo madarakani na hivyo imewagawa watanzania na kutufikisha hapa tulipo na mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe

c) Cuf kwasababu haijawaunganisha watanzania kudai haki zao za msingi kutoka serikali na hivyo itupiwe lawama

d) ...........

Nimeonelea nikuulize haya maswali kidogo ili kuanzia hapa tuone utata upo wapi, kwa watawala wa ccm, CUF, Cdm au NCCR.
 
Katika Imani ya dini, mimi ni Muislam wa uhakika na wala sitayumba katika Imani yangu hiyo, katika masuala ya kisiasa Chama changu ni CHADEMA, nitakipigania kwa nguvu zangu zote kishike madaraka ya Dola ya nchi hii. Siridhiki kabisa na jinsi CCM inavyoendesha nchi hii, dhuluma yake kwa wananchi wa kawaida imepituka viwango. Nimeridhishwa na sera za CDM, naamini inaweza kufanya vizuri ikiingia madarakani itafanya vizuri, ikishindwa, nitashiriki tena kuhakikisha nayo inaondolewa madarakani pia na kuweka mbadala utakaofaa kwa wakati huo, (ref Zambia) CCM wakiachwa waendelee, kiburi cha wenye fedha kitazidi, mashaka ya nchi yatazidi.
 
Huu ndio ukweli halisi wa hali ilivyo kua mwaka 2010,pale Bariadi Padre wa Kizungu wa Kanisa Katoliki alisema wazi kuwa waumini wamchague mtu wa dini yao! Kuna haja ya Chadema kukubalia tatizo hili na waangalie namna ya kujipambanua kua wao sasa sio chama cha kidini tena!
Na ni ukweli ulio wazi kuwa vikaratasi hivi vilikuwa vinasambazwa misikitini kumpigia kampeni Kikwete.

attachment.php

Pia Radio Imaan na Radio Heri FM zilikuwa zinatangaza moja kwa moja kuwa waislamu mchagueni Kikwete kwa kuwa ni muislam.

Kwa kuwa CCM ndio ilianzisha kampeni za udini, ndio hiyo pia imekuwa inakuza propaganda kuwa vyama vingine ndio vina udini.

Chadema haijawahi kutumia ushahidi wa karatasi hizo hapo juu, wala wa video ya Bakwata Igunga ikitamka kuwa waislamu wasichague Chadema kujenga propaganda za kidini.

Last edited by a moderator:
Zubeda

hayo madai uliorodhesha umeyatowa wapi? ninamaana hizo kasoro kama zipo nani alizisababisha? japokuwa kwa mtaamo wangu hazipo.

1. umeongelea ubaguzi wa rangi fafanua kidogo hili linfanyika wapi hapa tanzania na kwa misingigani?

2. Aliyetaifisha mashule alikuwa na lengo zuri tu kwa maslah ya watanzania wote, wakirudishiwa na wakristo warudishiwe? Je tunajenga umoja wa watanzania kama taifa au tunabomoa vipande vipande kama unavyopingana katika hoja yako no 1?

3. mgao sawa wa madaraka kwa maana ya Din? vipi kuhusu makabila nayo tutafanya hivyo maana wasukuma ni wengi sana.

b) Je tutafanya usaili wetu kwa maana ya dini zetu, kama ndivyo nafasi ya taaluma ya kila mmoja wetu itakuwa wapi?

c) Endapo tutajipanga kwa maana ya uwiano wa imani zetu, unataka kuniambia Pengo atafanya operation za matumbo na Idd Simba atafanya operation za wagonjwa wa moyo? je hiyo ndiyo maana halisi ya Taaluma na ufanisi kwa fani husika?

4. Nani kakwambia waislam wa tanzania hawapo huru?, Je wapagani wa tanzania wanauhuru gani na kwanini?

5. Chadema haijawahi kushika dola hata siku moja, ccm na serikali yake ndiyo wametutawala tangia uhuru, Je kasoro unazozisema zimesababishwa na

a) chadema kwasababu ndiyo ipo, madarakani na hivyo imewagawa watanzania nakusababisha mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe!

b) CCM ambayo ipo madarakani na hivyo imewagawa watanzania na kutufikisha hapa tulipo na mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe

c) Cuf kwasababu haijawaunganisha watanzania kudai haki zao za msingi kutoka serikali na hivyo itupiwe lawama

d) ...........

Nimeonelea nikuulize haya maswali kidogo ili kuanzia hapa tuone utata upo wapi, kwa watawala wa ccm, CUF, Cdm au NCCR.

Wewe unaoneka ulikuwa unaishi ughaibuni maana huna habari yoyote kuhusu Waislamu! nitakujibu fanya subira!
 
Wewe unaoneka ulikuwa unaishi ughaibuni maana huna habari yoyote kuhusu Waislamu! nitakujibu fanya subira!

Zubeda
Hata la ubaguzi wa rangi walau tuambie unafanyika wapi hapa tanzania?
 
Ni kweli udini ulioasisiwa na CCM dhidi ya CUF na kisha kuujenga ipasavyo dhidi ya CDM . Udini huu umewageukia, CCM wanamjadala mkubwa na mkali kweli kweli;wamegawanyika, kuna wanaosema rais ajaye kupitia CCM lazima awe MUISLAM. Upande mwingine, kuna wale wanaotaka rais ajaye lazima awe MKRISTO.
CCM wana kazi kweli kweli safari hii kuliko wakati mwingine wowote ule.
 
Mliji changanya sana kumsimamisha Padri Mstaafu kuwa Mgombea Urais,na makanisa yakawa yanatoa approval kuwa hata kama Padri hajaoa sio tatizo kuongoza nchi! Na matamko ya Roman Catholic nayo kipindi yalizidi,siku hizi wameacha! Naona hapa ndipo mlipo jipambanua!

Mkuu Kenneth Nollo, ulitaka tukusimamishe wewe ndo ugombee nafasi ya urais kupitia CHADEMA? inaonekana akili yako inabeni inahitaji kunyoshwa. Kwa taarifa yako huyo huyo ndo tutakaye msimamisha mwaka 2015, kwani ndo kiboko yenu nyie masalia, mafisadi, majangili mnao maliza tembo wetu, na wote mnaofikiria kwa kutumia makalio.
 
Ni kweli udini ulioasisiwa na CCM dhidi ya CUF na kisha kuujenga ipasavyo dhidi ya CDM . Udini huu umewageukia, CCM wanamjadala mkubwa na mkali kweli kweli;wamegawanyika, kuna wanaosema rais ajaye kupitia CCM lazima awe MUISLAM. Upande mwingine, kuna wale wanaotaka rais ajaye lazima awe MKRISTO.
CCM wana kazi kweli kweli safari hii kuliko wakati mwingine wowote ule.

Mkuu amini usiamini nchi hii haitakaa ishikwe na muislam tena.
 
Zubeda

hayo madai uliorodhesha umeyatowa wapi? ninamaana hizo kasoro kama zipo nani alizisababisha? japokuwa kwa mtaamo wangu hazipo.

1. umeongelea ubaguzi wa rangi fafanua kidogo hili linfanyika wapi hapa tanzania na kwa misingigani?

2. Aliyetaifisha mashule alikuwa na lengo zuri tu kwa maslah ya watanzania wote, wakirudishiwa na wakristo warudishiwe? Je tunajenga umoja wa watanzania kama taifa au tunabomoa vipande vipande kama unavyopingana katika hoja yako no 1?

3. mgao sawa wa madaraka kwa maana ya Din? vipi kuhusu makabila nayo tutafanya hivyo maana wasukuma ni wengi sana.

b) Je tutafanya usaili wetu kwa maana ya dini zetu, kama ndivyo nafasi ya taaluma ya kila mmoja wetu itakuwa wapi?

c) Endapo tutajipanga kwa maana ya uwiano wa imani zetu, unataka kuniambia Pengo atafanya operation za matumbo na Idd Simba atafanya operation za wagonjwa wa moyo? je hiyo ndiyo maana halisi ya Taaluma na ufanisi kwa fani husika?

4. Nani kakwambia waislam wa tanzania hawapo huru?, Je wapagani wa tanzania wanauhuru gani na kwanini?

5. Chadema haijawahi kushika dola hata siku moja, ccm na serikali yake ndiyo wametutawala tangia uhuru, Je kasoro unazozisema zimesababishwa na

a) chadema kwasababu ndiyo ipo, madarakani na hivyo imewagawa watanzania nakusababisha mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe!

b) CCM ambayo ipo madarakani na hivyo imewagawa watanzania na kutufikisha hapa tulipo na mapungufu tuliyonayo-Ilaumiwe

c) Cuf kwasababu haijawaunganisha watanzania kudai haki zao za msingi kutoka serikali na hivyo itupiwe lawama

d) ...........

Nimeonelea nikuulize haya maswali kidogo ili kuanzia hapa tuone utata upo wapi, kwa watawala wa ccm, CUF, Cdm au NCCR.

Mbali na ubaguzi wa kidini, Ubaguzi wa rangi Tanzania upo na ushahidi ni kutaifishwa kwa nyumba nyingi za Wa TZ wenye asili za kiasia hasa India mwaka 1967 na mpaka leo nyumba zao zinaitwa msajili wa majumba! huu ni ubaguzi wa wazi kabisa tuliowafanyia wenzetu wahindi! kwanini iwe wao tu na sio wengine?

Salim Ahmed Salim ni mtanzania lakini ana asili ya uarabu! kwanini alipogombea urais 2010 alinasibishwa na asili yake ya uarabu na Kinana alipomtetea ktk kamati kuu alinyamazishwa na Mzee Ngombale Mwiru na kuambiwa kaa chini Msomali wewe!

Seifu Sharifu Hamadi ni mpemba mwenye asili ya Ushihiri mara zote alizogombea urais alishinda lakini hakutangazwa mshindi! jee, huo sio ubaguzi wa rangi? mbona Shein yeye ni mbantu na alipogombea kwa mara ya kwanza huku akiwa hana ushawishi Zanzibar alitangazwa mshindi!

Hapa ktk mtandao wa JF kumejaa post za ubaguzi wa rangi dhidi ya kiongozi yoyote wa CCM mwenye asili ya Asia, India au Somalia! lakini kama kiongozi huyo ni Chadema basi habaguliwi! mfano ni Said Arfi mwenye asili ya Kiarabu yeye ni raia halisi kwa kuwa ni Kiongozi wa chadema! cha kutia aibu Mustafa Sebodo ni Mhindi na kada wa CCM lakini kwa kuwa anaifadhili Chadema basi yeye ni raia mzuri!
lakini wengine walioko CUF au CCM wao si raia! sasa huu kama sio ubaguzi wa rangi ni nini?

Ama kuhusu ubaguzi wa kidini TZ na madhila ya liyowasibu Waislamu wa TZ nakuomba ujaribu kusoma kitabu hiki kilichoandikwa na Makamu mkuu wa chuo kikuu Morogoro Dr. Hamza Njozi Preface - Mwembechai Killings and The Political Future of Tanzania

Baada ya hapo nadhani utakuja na ujumbe mpya hapa!
 
CDM wanajua wazi bila kuungwa mkono na waislam hawawezi kuingia Ikulu ukweli ndio huo. WAISLAM ndio wanaipiga kura sana kuliko wengine.Pia wengi wao wapo katika informal sector hivyo wanamuda kwa kujiandikisha na kusimama kwa mda mrefu kusubiri kupiga kura.

Waislamu huwa hakuna utenganishi kati ya dini na siasa, kwao siasa ni dini pia. Maana religion is the way of life ( Mfumo kamili wa maisha).
 
Ni kweli udini ulioasisiwa na CCM dhidi ya CUF na kisha kuujenga ipasavyo dhidi ya CDM . Udini huu umewageukia, CCM wanamjadala mkubwa na mkali kweli kweli;wamegawanyika, kuna wanaosema rais ajaye kupitia CCM lazima
awe MUISLAM. Upande mwingine, kuna wale

wanaotaka rais ajaye lazima awe MKRISTO.

CDM hamna KAZI maana mgombea wenu ni BABU na tayari ni Padri......CCM hajulikani hadi
CCM mda ukifika. Hongereni kwa democracy yanu maana mwenyekiti kashaweka bayani sasa hakuna uchaguzi hapo ndani ya chama
 
Mi nafikiri waislamu wako smart katika kudai favour na special privileges kutoka kwa wana siasa na serkali. Wakristo tunany amaza halafu wakifanikiwa tukaanza kukandamizwa kama ilivyo sasa ndio tunazinduka na kutoa matamko. Mimi naona hii si sawa. Waislamu hata wanapojua kuwa wana lead mfano katika nafasi zote muhimu za serkali wakati huu, bado utawasikia wanapiga kelele kuwa wamekandamizwa ili wahalalishe upendeleo wanaofanyiwa. Sasa hili la kutaka nafasi maalum tena za upendeleo katika Chadema mimi naona ni hatari.

Kadi za Chadema zinauzwa hadharani na katika viwanja vya mikutano yao. Haziko makanisani wala kwa paroko. Sasa inakuwaje walalamike kuwa Chadema ni chama cha wakristo? Chadema haina MOU na wakristo wala haijafanya mawasiliano yoyote na taasisi za kikristo kuhusu uanachama au itakayofanyia wakristo kama ikishika dola. Unaona sasa waislamu wanajitanguliza kwa vile awali waliweka nguvu nyingi kwa ccm kwa vile waliingizwa kijanja na ccm kwa uroho wa kura kuwa itawapa mahakama ya kadhi. Hawakujua kama chadema itakuja kuwa na nguvu ilizzo nazo leo. Badala ya kugeuza mwelekeo na kujiunga na chadema wanaanza kulaumu ni chama cha wakristo. Hii ni kwa vile 2010 masheikh na maimamu walishikamana na ccm na kulazimisha waislamu misikitini kuwapa ccm kura. bado walishangaa kuona cdm imeshinda uchaguzi ikawa lazima ccm kuchakachua. hivyo sasa wana speculate kuwa kama sisi hatukuwapa kura bila shaka wakristo ndio waliwapa kura. Hii ni kwa vile wanashindwa kujua kuwa kuna waislamu wa ukweli waliokataa cheap propaganda na wakaasi maimamu na kuwapa cdm kura!!!!

Wake up Kama ni hivyo wakristo tuanze kudai mapema cdm ikishika dola lazima ifanye mambo maalum kwa wakristo maana sasa tumeshatukanwa vya kutosha na hiyo chadema. Kama ni kweli ni wakristo pekee waliopa chadema kura basi ijulikane kuwa hata bila kura za waislamu chadema itashinda maana hata 2010 ilishinda!!!
 
Labda ndio maana EL anakazana kutafuta kukubalika makanisani maana ana influence kubwa UWT na walikwisha mwambia kuwa ukipata kura za wakristo una uhakika wa kuingia ikulu!
 
CDM wanajua wazi bila kuungwa mkono na waislam hawawezi kuingia Ikulu ukweli ndio huo. WAISLAM ndio wanaipiga kura sana kuliko wengine.Pia wengi wao wapo katika informal sector hivyo wanamuda kwa kujiandikisha na kusimama kwa mda mrefu kusubiri kupiga kura.

Waislamu huwa hakuna utenganishi kati ya dini na siasa, kwao siasa ni dini pia. Maana religion is the way of life ( Mfumo kamili wa maisha).
Ndio maana wanafanya kampeni kama hizi:
attachment.php
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom